Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 1581.

  • 19 Sep 2023 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa hii fursa ili nichangie Mswada huu wa lugha ya ishara ambao umeletwa chini ya ‘collabo’ ya Sen. Crystal Asige na Sen. (Prof.) Kamar. Mswada huu utasaidia pakubwa--- The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 19 Sep 2023 in Senate: Madam Temporary Speaker, she was raising her hand to get your attention. view
  • 19 Sep 2023 in Senate: Bi. Spika wa Muda, neno ‘collabo’ linatumika kwenye lugha ya Kiswahili. Hivi sasa niko tayari kujibu hoja ya nidhamu ya Kiongozi wa walio Wachache kwa kuondoa neno hilo. Pengine nitapata fursa siku nyingine kulijadili neno hilo kwa kina. Mswada huu tunaoujadili ni muhimu sana. Katiba yetu imetoa haki nyingi ambazo wananchi wanastahili kupata, lakini kwa sababu ya kutokuwa na sheria za kurahisisha haki hizi imekuwa ngumu wananchi kuzipata. Moja ya zile haki ni kupata lugha ambayo itaeleweka kwa yule ambaye anazungumziwa ama anayezungumza ili mawasiliano yawe rahisi. Kumekuwa na ongozeko la matumizi ya watu wanaohitaji lugha ya ishara. Ijapokuwa wazungumzaji ... view
  • 19 Sep 2023 in Senate: Bi. Spika Wa Muda, nimesimama kwa Hoja ya nidhamu kuambatana na Kanuni Nambari 37 ya Bunge la Seneti kuomba kwamba Bunge lihairishe ratiba yake ili kujadili swala ambalo ni la muhimu na lina umuhimu kwa taifa, ambalo ni hali ya usalama katika Kaunti ya Lamu ambayo imesababishwa na matokeo ya hivi majuzi ya mashambulizi ya majangili Al Shabaab. Bi. Spika wa Muda, kwanza kabisa ningependa kusema kwamba japo kuwa maswala haya yanatendeka Lamu, mjadala au maelezo yangu hayahusiani kwa vyovyote na siasa za Lamu. Ni muhimu ieleweke kwamba hatuzungumzii siasa za Lamu hapa. Tunazungumzia maswala ambayo yanatendeka Lamu lakini yanaleta ... view
  • 19 Sep 2023 in Senate: mmoja wa miaka 22. Mwingine alizikwa sehemu za Tiribe katika Kaunti ya Kwale na pia alikuwa wa umri huo huo. Kumekuwa na ongezeko la visa vya mashambulizi ya kundi la kigaidi la Al shabaab katika eneo la Lamu. Itaeleweka kwamba Kenya ilikwenda Somalia mnamo mwaka wa 2011, mwezi wa kumi ili kuzuia kundi hili la Al shabaab kuweza kufanya mashambulizi katika nchi ya Kenya. Lengo lilikuwa kuweka buffer zone kati ya mpaka wa Somalia na wa Kenya ili mashambulizi yasiweze kufanyika Kenya. Shambulizi lililokuwa limefanyika Lamu wakati huo ni kuwa mtalii mmoja aliuwawa na bibi yake kutekwa nyara na majangili ... view
  • 19 Sep 2023 in Senate: hapa kwetu na hatuwezi kujilinda. Watu wengi wamepoteza maisha ambayo yangeweza kulindwa. Hivi majuzi, Bibi ya Mbunge wa Eneo Bunge katika Kaunti ya Lamu, alipoteza maisha na yeye mwenyewe kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la hao majangili. Kaunti zetu, kama Kaunti ya Lamu inafanya biashara kubwa na Mombasa. Mazao mengi yanatoka Lamu kuja kuuzwa Mombasa na kuna vitu ambavyo vinatoka Mombasa na kuuzwa katika Kaunti ya Lamu. Kwa mfano, mchele, mafuta ya kupikia na vinginevyo. Mashambulizi haya yanalemaza biashara baina ya Kaunti ya Mombasa na Kaunti ya Lamu. Vile Vile, wakulima wameweza kutatizwa na mashambulizi kama haya. Kwa hivyo, kauti zetu ... view
  • 19 Sep 2023 in Senate: Madam Temporary Speaker, I do not wish to interrupt my brother, Sen. Wamatinga, but he should not make allegations which he cannot substantiate. Nobody has mentioned any governor. The Senator for Lamu never mentioned any governor in his contribution to the debate. So, he should not mention a person who The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 19 Sep 2023 in Senate: cannot be called here to defend himself. If he has evidence that he is involved, let him bring a substantive Motion. He shall be debated here and the Governor will be given an opportunity to defend himself. He should not throw allegations on somebody who cannot come to this House to defend himself. He should ignore those remarks. view
  • 29 Aug 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa kuchangia Hoja hii ya mjadala wa kitaifa. Najiunga na wenzangu kuwapongeza viongozi wa nchi na wa Azimio, Mheshimiwa ‘Baba’ Raila Amolo Odinga, kwa kuweza kuwa na makubaliano kuhusiana na maswala haya. Wakati kulitangazwa kwamba kutakuwa na mjadala wa kitaifa, nchi ilipumua, biashara zikafunguka na amani ikarudi katika nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, ni masikitiko kwamba wenzetu hapa wanaweza kuzungumza kwamba ilikuwa haifai kwa viongozi hawa kuwa na mjadala. Tukiangalia hata uhuru uliopatikana katika nchi hii, baadhi ya ndugu zetu walikufa lakini baada ya mazungumzo, kukapatikana mwafaka kule Lancaster na uhuru katika nchi yetu ... view
  • 29 Aug 2023 in Senate: Tuliona jana katika vyombo vya habari akitishia kupeleka watu mbinguni. Yeye sio Yesu wala mtume. Sisi sote ni wananchi na binadamu wa Kenya. Iwapo kuna mambo yoyote ambayo yanatakiwa kuzungumzwa, yazungumzwe kwa njia ya mijadala view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus