14 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bw, Spika, kwa kunipa fursa hii. Kimsingi ni kwamba mawakili wa gavana wanataka masuala haya yaamuliwe kabla ya kusikiliza mashtaka ambayo yameletwa hapa na Bunge la Kaunti ya Kericho. Seneti inapokaa kuaamua masuala ya Impeachment, ni kama mahakama. Katiba yetu katika kifungu cha 159 inasema kwamba mahakama zinapokaa, haki iamuliwe bila kuzingatia masuala magumu ya procedure na t echnically . If I may read it in English is, that justice shall beadministered without a---
view
14 Oct 2024 in Senate:
For the benefit of the two parties---Samahani, Bw. Spika.
view
14 Oct 2024 in Senate:
Samahani Bw. Spika. Suala lililoko mbele ya Seneti ni kwamba Seneti iamue Hoja iliyofikishwa mbele yake bila kuzingatia mambo ya technicality kwa sababu tutapoteza fursa ya kutenda haki ya kimsingi. Pili, Seneti inapiga kura kwa delegation . Hili ni suala ninaloathiri kaunti na masuala yote yanayoathiri kaunti, uamuzi huwa ni kupiga kura kwa wawakilishi 47 waliopo katika Bunge hili. Bw, Spika, kwa hivyo wewe kutoa uamuzi kwamba quorum haikutimia katika Bunge la Kaunti ya Kericho, hapo utakuwa umekiuka Katiba na Kanuni za Kudumu zetu zinazosema kuwa uamuzi ufanywe na wawakilishi wa Kaunti waliopo Katika Bunge hili. Asante sana.
view
9 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa marekebisho ya Sheria ya makosa ya uchaguzi. Sheria hii na marekebisho haya yamekuja kupitia kwa ile Kamati ya National
view
9 Oct 2024 in Senate:
Kwenye Bunge letu la Seneti iliwakilishwa na Sen. Cheruiyot ambaye ni Kiongozi wa Wengi na vile vile Sen. Omogeni ambaye aliwakilisha upande wa wachache. Ni muhimu kwamba sheria zetu za uchaguzi zipigwe msasa mara kwa mara, kwa sababu, kuna mambo yanayoibuka katika uchaguzi ambayo mengine labda hayakuweza kuangaziwa katika sheria iliyoundwa. Bi. Spika wa Muda, haifai kuwa na vituo gushi vya uchaguzi ambapo unaambiwa matokeo yanatoka katika kituo fulani ambacho hakiko kwenye orodha. Hivyo basi, Sheria hii itaharamisha matokeo ya vituo vyovyote ambavyo haviko katika orodha ya vituo vya kufanyia uchaguzi. Swala la pili linahusu wale wanaosimamia uchaguzi.
view
9 Oct 2024 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, kuna mabarobaro wawili hapa wanaocheka kwa sauti. Naomba wacheke wa sauti ya chini kwa sababu mzee anazungumza. Kwa hivyo, ni muhimu kunisikiliza.
view
9 Oct 2024 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, wale wanaosimamia uchaguzi lazima sheria iwaangazie. Kukiwa na ukiukaji wa sheria wakati wa uchaguzi, ni muhimu wanaohusika wapelekwe mahakamani na kushtakiwa kwa makosa hayo. Haiwezekani msimamizi wa uchaguzi akatae kuhesabu kura halali iliyopigwa na mwananchi wa Kenya. Haiwezekani msimamizi wa uchaguzi kutangaza mtu aliyeshindwa kuwa mshindi bila kuchukuliwa hatua yoyote kwa mujibu wa sheria. Kwa hivyo, sheria hii itasaidia kuwachukulia hatua watakaopeleka matokeo yasiyo sawa wakati wa uchaguzi nchini Kenya. Kwa hayo maswala mawili, naunga mkono marekebisho ya Sheria ya Makosa ya Uchaguzi.
view
2 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Mimi najiunga na Maseneta wenzangu kumkaribisha Waziri, Mhe. John Mbadi katika Bunge la Seneti na pia kumpa kongole kwa kuchaguliwa kuwa Waziri katika Serikali. Dukuduku langu ni kuhusiana na swala la ucheleweshaji wa fedha kwa kaunti zetu kwa sababu baada ya kuondolewa kwa Mswada wa Fedha wa Mwaka 2024/2025, kumekuwa na sintofahamu ni vipi watapeleka pesa katika kaunti zetu. Ninakumbuka mwaka 2019 tulikuwa katika hali hii, lakini kwa wakati ule Serikali iliyekuwa mamlakani ilipeleka asili mia fulani ya fedha kwa kaunti zetu. Ninaomba Waziri atueleze, ni sababu gani kaunti haziwezi kupewa asili mia fulani mpaka asili mia ...
view
1 Oct 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, roho yangu imetulia kuona Sen. Munyi Mundigi ameketi kwa sababu alikuwa anarusha ngumi na mikono ungefikiri yuko uwanja wa miereka.
view
1 Oct 2024 in Senate:
Kitendo kama hicho cha Sen. Munyi Mundigi hakiongezi sifa katika Bunge hili kwani inaonekana kama anapigana Bungeni. Watu huzungumza kistarabu hapa. Sen. Munyi Mundigi, siku nyingine usijaribu kuonyesha vidole.
view