Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 41 to 50 of 1994.

  • 1 Oct 2024 in Senate: On a point of order, Mr. Temporary Speaker, Sir. view
  • 1 Oct 2024 in Senate: Nimemsikia Sen. Cherarkey akisema kuwa yeye ni wakili mkuu. Lakini, mimi nakumbuka tukiwa Bunge hili mwaka wa 2020 au 2021 ndio Sen. Cherarkey aliapishwa rasmi kama wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya. Je, inawezekana wakili wa miaka mitatu ajiite wakili mkuu wakati hapa katika Bunge hili tuna mawakili ambao wana vyeo vya senior counsel wakiongozwa na Sen. Omogeni na Sen. (Rtd.) Justice Madzayo wakati sisi tulikuwa hapa na tukaona Sen. Cherarkey akiapishwa? Sisi ndio tulimpeleka Mahakama Kuu kwenda kuapishwa. Asante, Bw. Spika wa Muda. view
  • 26 Sep 2024 in Senate: Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii kujiunga nawe kumpa kongole dada yetu, Esse, kwa kazi nzuri anayofanya. Esse ni mmoja wa wale wanamichezo wetu ambao wamebobea kucheza katika ligi za kimataifa. Mwingine ni Bi. Mwanahalima Adam Jereko ambaye anacheza kule Marekani sasa hivi. Bi. Mwanahalima ni msichana aliyelelewa Likoni, mjini Mombasa. Kwa hivyo, Sen. Aaron Cheruiyot, usifikiri kwamba haya mambo yanatokea Kilifi peke yake. Mombasa pia kuna mambo kama hayo. Bw. Spika, nilipata fursa ya kutembea mpaka kule Bamba katika Uwanja wa Moving the Goalposts (MTG). Nafikiri ni mradi mzuri ambao kaunti zetu zote zinafaa kuiga. Kuna Mswada wa ... view
  • 26 Sep 2024 in Senate: Thank you, Mr. Speaker, Sir. I rise pursuant to Standing Order No.53 (1) to seek a statement from the Standing Committee on Roads Transportation and Housing on the imminent eviction of civil servants from the Hobley Road Estate near Mombasa Municipal Stadium in Mombasa County. The civil servants are due to be evicted from 1st October, 2024 ostensibly to pave way for the construction of a new housing estate in the Affordable Housing Plan. Since we are alive to what happened to Buxton where to date the former tenants have not been resettled despite a resolution of this House, I ... view
  • 25 Sep 2024 in Senate: Thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir, for giving me this opportunity. I also want to join my colleagues in congratulating the Cabinet Secretary for her appointment to the Cabinet in the tourism docket. Hon. Cabinet Secretary, I want to confirm when the Ministry will likely return the Mama Ngina waterfront to the Mombasa County Government. This property belonged to Mombasa County. The Government came in and improved it, but after the improvement, they took away the title deed. So, we need our title deed back for the Mombasa Mama Ngina waterfront. Thank you. view
  • 24 Sep 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii nichangie Mswada wa marekebisho ya sheria ya DORA. Kwanza kabisa naunga mkono ripoti ya Kamati ya Fedha na Bajeti ya Bunge hili kuhusiana na kuangalia kwao kwa Mswada huo wa marekebisho ya DORA. view
  • 24 Sep 2024 in Senate: Sheria ya DORA ilipitishwa mapema mwaka huu. Kiwango cha pesa zinazotakikana kwenda kwa kaunti zetu kwa mwaka huu wa 2024/2025 ni shilingi bilioni 400.1. Lakini kutokana na kuondolewa kwa Mswada wa Fedha wa 2024/2025 katika Bunge la Kitaifa, imebidi kufanywe marekebisho ili zile pesa zingekwenda kwa kaunti zetu zipunguzwe kulingana na ukweli kwamba Serikali haitaweza kukusanya pesa kama vile walivyokuwa wanatarajia. view
  • 24 Sep 2024 in Senate: Mswada huu basi unataka kupunguza pesa kutoka shilingi bilioni 400.1 hadi shilingi bilioni 380. Mwaka uliopita, Bunge hili pamoja na Bunge la Kitaifa lilipitisha shilingi 385.45 bilioni kama pesa zilizotakikana kwenda katika kaunti zetu. Ni Masikitiko ya kwamba pesa zilizofika kwa kaunti zetu zilikuwa shilingi bilioni 355 pekee. Shilingi bilioni 30 hazikufika kwa kaunti zetu. Mpaka sasa, Serikali haijatoa maelezo ya kwa nini haikupeleka pesa hizo. view
  • 24 Sep 2024 in Senate: Jambo lingine la kusikitisha ni kwamba kutoka mwezi wa sita mwaka huu, kaunti zetu hazijapata hata ndururu kutoka kwa Serikali kuu. Nimesikia Seneta aliyetangulia akisema kufikia mwisho wa mwezi watapelekewa shilingi bilioni 32. Pindi pesa zinapochelewa, serikali za kaunti zinapata shida ya kukithi mahitaji yao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate. view
  • 24 Sep 2024 in Senate: Inasikitisha kwamba jana daktari mmoja alijitoa uhai kwa sababu ya kucheleweshwa mishahara. Hivyo basi, hangeweza kukithi mahitaji yake ya kibinadamu. Mambo haya ya kucheleweshwa kwa fedha yanachangia pakubwa malimbikizi ya madeni katika kaunti zetu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus