24 Sep 2024 in Senate:
Tukiangalia kimsingi, fedha zinazokwenda katika kaunti, hazipaswi kupunguzwa kwa namna yoyote. Serikali ya kuu iko na uwezo wa kukopa katika soko la hisa hapa nchini na vile vile nje. Lakini, kaunti zetu hazina fursa kama hiyo ya kukopa. Kukopa kunahitaji udhamini wa Serikali kuu. Udhamini huo hauwezi kupatikana kwa sababu Serikali kuu iko na madeni kupita kiasi. Imepitisha kiwango cha deni kiliyowekwa ya asilimia 55 ya pato la kitaifa.
view
24 Sep 2024 in Senate:
Pesa zinacheleweshwa kutoka kwa Serikali kuu kwenda kwa serikali za kaunti. Hata zile wanatarajia baada ya kupitishwa kwa disbursement schedule, vilevile haziwezi kufika kwa wakati. Kwa hivyo, haiwezekani kwamba fedha za serikali za kaunti zipunguzwe wakati serikali kuu ina uwezo wa kukopa na kukusanya fedha zaidi ya zile zinazohitajika kukusanywa kwa ule mwaka unaofuata. Bw. Spika wa Muda, jambo la tatu ni kwamba tunapozungumzia asilimia ya fedha zinazoenda kwa kaunti, tunatumia hesabu za miaka minne nyuma. Kwa sasa, tunatumia mwaka wa 2020/2021 kugawa fedha zilizokusanywa mwaka huu wa 2024/2025. Hiyo inatoa taswira mbaya kwa sababu fedha ambazo tunazungumzia ni zile ...
view
24 Sep 2024 in Senate:
Kwa hivyo, hii ni taswira mbovu kabisa. Serikali inatarajia shililingi trilioni 2.6 kwa sasa. Kwanza, ilikuwa inatarajia shilingi trilioni 2.9 lakini iliporekebishwa ikafika shilingi trilioni 2.6, ilhali zile accounts zinazotumika kwa mipango hii ni za 2020/2021 wakati ambapo mapato ya serikali ilikuwa shilingi trilioni 1.9.
view
24 Sep 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kwa hivyo, ipo haja ya kurekebisha Katiba ili ile asilimia inayotumika iwe ya mapato ya mwaka wa sasa. Hii ni kwa sababu serikali imenuia kukusanya hizi pesa katika kaunti. Kwa hivyo, hatuoni sababu ya takwimu za mwaka huu kutotumika kuhakikisha kwamba pesa zinapatikana.
view
24 Sep 2024 in Senate:
Tukiangalie zile sheria ambazo serikali kuu ilipitisha kupitia Bunge hili na Bunge la Kitaifa, utapata kwamba zimeongeza gharama katika kaunti zetu. Kwa mfano; sheria ya afya, Social Health Insurance Fund (SHIF) inaongeza gharama kwa serikali za kaunti kwa sababu mfanyakazi analipiwa na vile vile, pia kaunti inachangia katika pesa zile.
view
24 Sep 2024 in Senate:
Tukiangalia pia sheria ya National Social Security Fund (NSSF), pia inaongeza gharama kwa sababu, tajiri na pia mfanyakazi wanalipa. Kwa hivyo, itabidi serikali za kaunti ziingie mifukoni zaidi ili walipie hizo tofauti zinazotakiwa kulipwa kwa wafanyakazi wao. Tukiangali masuala ya wafanyakazi wa afya ya umma, Community Health Promoters (CHPs), ni jambo ambalo serikali imetilia mkazo. Kwamba, kaunti zetu ziajiri hawa watu ili wapate ajira na wasimamie hii sheria mpya ya afya. Kwa hivyo, hii pia ni gharama inayo ongezeka bali na ile nyongeza ya mishahara ambayo iko katika makubaliano kati ya vyama vya wafanyakazi wa kaunti na serikali za kaunti. ...
view
24 Sep 2024 in Senate:
Kwa hivyo, hatuwezi enda na mfumo kwamba hizi pesa zipunguzwe. Hii ni kwa sababu zikipunguzwa, mambo mengi ambayo yamepangwa kufanyika katika kaunti zetu hayatafanyika.
view
24 Sep 2024 in Senate:
Kwa sasa, kaunti nyingi zinatumia asilimia kubwa; karibu asilimia 50 ya mapato ya kaunti zetu ya fedha kwa mambo ya matumizi ambayo sio ya maendeleo, yaani,
view
24 Sep 2024 in Senate:
. Ikiwa hakuna fedha za kutosha zinazoenda katika miradi ya maendeleo ina maanisha kwamba hatutakuwa na miradi yoyote ya maendeleo ambayo itafanyika katika kaunti zetu. Hivyo basi, tutakuwa siku zote tunatumia pesa kwa mambo ya recurrentexpenditure kuliko kutumia kwa maendeleo katika kaunti zetu.
view
24 Sep 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ningependa tu kugusia mambo mawili ambayo yameangaziwa leo katika vyombo vya habari. Pesa nyingi zinatumika kwa mambo mengi ambayo siyo ya msingi kimaendeleo katika kaunti zetu. Tumeambiwa, kwa mfano, Kaunti ya Kakamega, chai na mandazi na mambo mengine yasiyo muhimu, yametumia karibu shilingi milioni 522; Kaunti ya Nakuru imetumia shilingi milioni 400 na Bungoma vilevile. Ijapokuwa sikuiona ya Mombasa County labda sisi hatutumii mahamri sana.
view