Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 61 to 70 of 2095.

  • 18 Feb 2025 in Senate: APPRECIATING the lasting legacy that he leaves in the media industry and the high esteem in which he was held by colleagues and persons from all walks of life; NOW THEREFORE the Senate expresses its deep sadness at the death of Mr. Mbotela, records its celebration and appreciation of his remarkable life and extends its heartfelt sympathy and condolences to his family, friends and the nation. Thank you. view
  • 13 Feb 2025 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Mimi nasimama kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu Nambari 53(1) ya Kanuni za Seneti, kuomba kauli kutoka kwa Kamati ya Afya kuhusiana na kuzorota kwa huduma za afya katika Kaunti ya Mombasa. Kaunti ya Mombasa inajivunia kuwa jiji la pili nchini na pia kuwa na bandari inayohudumia, kando na nchi yetu, nchi kadhaa za ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo maziwa makuu; Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Sudani Kusini na vile vile Ethiopia. Mombasa ndiyo jiji lenye uwanja wa ndege wa kimataifa katika eneo nzima la kanda ya Pwani na ndiyo makao makuu ya ... view
  • 13 Feb 2025 in Senate: Bw. Naibu Spika ninaomba unilinde kwa sababu ninasoma taarifa hapa na ninaona kuna majadiliano ya watu wa ODM. view
  • 13 Feb 2025 in Senate: Lakini Bw. Spika kuna Maasai hapa nyuma yangu. view
  • 13 Feb 2025 in Senate: Katika Kauli hii, ninaomba Kamati hiyo - (1) Iorodheshe hatua ambazo Serikali ya Kaunti ya Mombasa imechukua kusuluhisha tatizo la hali mbaya inayoendelea, kudorora kwa utoaji wa huduma za afya ikizingatia kuwa kuna upungufu wa madaktari, wauguzi, wachunguzi wa mahabara na view
  • 13 Feb 2025 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate. view
  • 13 Feb 2025 in Senate: hata walinzi wa milango na maeneo ya hospitali na zahanati nyingi za Kaunti ya Mombasa. (2) Ibaini sababu zilizopelekea Serikali ya Kaunti ya Mombasa kupuuza uboreshaji wa huduma kwa kutoshughulikia miundo mbinu kama vile ukarabati wa majengo ya vituo hivyo, hususan Hospitali ya Tudor ambapo hivi majuzi mgonjwa aliangukiwa na dari wakati anasubiri huduma katika hospitali hiyo. Vile vile, zahanati za Maweni na Ziwa la Ngomo ambazo huvuja na pia hufurika maji wakati wa mvua pamoja na usambazaji wa maji safi ya mifereji. (3) Ieleze hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali ya Kaunti kununua na kuboresha vifaa vya kuhudumia wagonjwa kama ... view
  • 13 Feb 2025 in Senate: (4) Ieleze sababu zilizochangia kutokupatia vituo vya afya mapato wanayokusanya kwa matumizi yao yaani Facility Improvement Fund pamoja na sababu zilizofanya kutoa agizo kwamba vituo vya afya havina ruhusa kuajiri vibarua, licha ya kwamba vibarua hao wamekuwa wakihudumu kwenye vituo hivyo kwa mda mrefu. (5) Ifafanue mantiki ya kulipa mishahara ya wahudumu bila kununua dawa wala kujenga chochote ikiwa ni pamoja na kushindwa kuchukua hatua ya kubadilisha paa za view
  • 13 Feb 2025 in Senate: Bw. Spika wa Muda, jana kulisomwa taarifa kwamba asbetors inasababisha saratani. Paa za asbestors zilipigwa marufuku humu nchini kwa kuhofia kusababisha ugonjwa wa saratani, ilhali kuna pesa zilitengwa kwa kusudi ya kutoa huduma hizo za afya kwa wakaazi wa Pwani na Mombasa. (6) Ifanye uchunguzi ili kubainisha chanzo cha kudorora huku na ichukue hatua zinazofaa ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zinazostahili, pamoja na kuchunguza sababu zilizochangia kutotumika kwa hospitali ya Shonda katika eneo la Likoni na Marimani katika sehemu ya Kisauni, zilizomalizika kujengwa mnamo mwaka 2022. Bw. Spika wa Muda, asante kwa fursa hii. view
  • 12 Feb 2025 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa elimu ya uraia ulioletwa katika Bunge na Seneta Okenyuri. Ninampongeza Sen. Okenyuri kwa Mswada huu kwa sababu ni Mswada ambao una mambo mengi mazuri ambayo yatasaidia nchi yetu kuelimisha raia kuhusiana na haki zao, mambo ya kiserikali na majukumu ya viongozi wanaochagua kila baada ya miaka mitano. Katiba mpya ilipokuja mwaka 2010, ilikua ni matarajio ya wengi kua serikali itaanzisha elimu ya uraia, hususan kuelimisha wananchi juu ya haki zao kikatiba na pia yale mambo mengi mapya yaliyokua katika katiba hii yetu. Lakini, ni masikitiko kwamba, haikufanya hivyo. ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus