12 Feb 2025 in Senate:
hamsini na moja. Hizo zote ni haki ambazo wananchi wanatakikana wazijue na kuzifuatilia. Kwa sasa wengi watakuambia kuwa haki waliyonayo ni haki ya kuishi, Haki ya Elimu na Haki ya Kujieleza (Freedom of Expression). Zile zingine zote arobaini na nane wananchi hawazijui. Kwa mfano, sasa hivi kuna vyakula vingi ambavyo vinauziwa wananchi wetu lakini hawajui vipi wataweza kujitetea haki zao iwapo vitu walivyovinunua vina madhara kwa binadamu. Vile vile, Mswada huu utasaidia wananchi kutaka huduma nzuri zaidi kutoka kwa viongozi. Hii ni kwa sababu, ukishajua haki yako, utaweza kujua ni njia gani ambayo utatumia kufuatilia haki zile ili ziweze kutekelezwa. ...
view
12 Feb 2025 in Senate:
kikamilifu. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu utakuwa wa manufaa makubwa. Utasababisha wananchi waelewe zaidi Katiba yetu na sheria zinazotungwa. Hii itawasidia wakati watakapohusishwa katika utunzi wa sheria ama mjadala wa bajeti ama mjadala wowote mwengine kutokana na ile elimu watakayokuwa wamepata. Itawawezesha kuchangia kwa mswada ama mambo yanayowakabili katika maisha yao. Mhe. Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu. Asante kwa kunipa fursa hii.
view
11 Feb 2025 in Senate:
Bw. Naibu Spika, nilikuwa nimebofya ili nimjuze Seneta wa Kaunti ya Kitui alipokuwa akijadili hoja. Kwa sasa singependa kuchangia Hoja hii. Asante.
view
5 Dec 2024 in Senate:
Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Hoja ya Kiongozi wa Wengi kuhusu kuahirishwa kwa Bunge hili kwa msimu wa Krisimasi na Mwaka Mpya. Ni kweli kwamba tumefanya kazi nyingi mwaka huu na kulikuwa na mambo mengi ikiwamo mzozo wa Generation Z waliongia katika Bunge letu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
5 Dec 2024 in Senate:
Cha msingi ni kwamba, ijapokuwa Seneti inafanya kazi yake, kuna mambo yanayofanyika yanayozidi kurejesha nyuma ugatuzi, kwa mfano, utendakazi wa serikali zetu za kaunti. Kuna malimbukizi ya madeni kila mwaka yanayosababisha hasara kwa kaunti zetu. Ikiwa kwa mwaka kaunti zinashindwa kulipa madeni na kuongeza mengine, ina maana kwamba yataendelea kuongezeka. Bi. Spika wa Muda, nachukua fursa hii pia kuwakaribisha nyote na Wabunge wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Kaunti ya Mombasa kwa michezo ya---
view
5 Dec 2024 in Senate:
Mheshimiwa yeyote ambaye pengine atakuwa ametumia pesa na kumaliza, mimi niko Mombasa. Nitahakikisha kwamba nimemlipia nauli ya treni ili arudi nyumbani.
view
4 Dec 2024 in National Assembly:
Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ambayo imeletwa na Sen. Kibwana; taarifa kuhusiana na siku 16 za kupambana na gender-basedviolence yani vita dhidi ya dhuluma ya kijinsia. Ni siku kumi na sita ambazo zinaadhimishwa kuanzia tarehe 25 mwezi uliopita mpaka tarehe 10 Decemba. Kwa kusema kweli, mwaka huu katika nchi ya Kenya, tumeona visa vimeongezeka vya ukatili dhidi ya wasichana, kina mama na vile vile pia watoto wadogo wa kike. Polisi walipotoa tarakimu zao mwezi uliopita, ilikuwa karibu wanawake 100 ambao walikuwa wameuliwa mikononi mwa watu kwa sababu za kikatili. Hilo ni swala ambalo kwa sasa Kenya ...
view
4 Dec 2024 in National Assembly:
Bw. Spika Taarifa ya pili ambayo nilikuwa nataka kuchangia ni taarifa ambayo imeombwa na Naibu wa Spika, Seneta wa gatuzi la Meru, kuhusiana na mambo yalivyo katika University of Nairobi ambacho ni chuo ambacho mimi niliwahi kupitia. Ni jambo la kusikitisha kwamba vyuo vyetu sasa vina kuwa ni mahali ambapo uongozi haufanyiki au uongozi umekuwa duni kiasi ambacho migogoro na mizozano haishi. Ikumbukwe jumatatu ya wiki iliyopita, kulikuwa na maandamano ya wafanyikazi Kenyatta University Teaching and Refferal Hospital (KUTRH ) ambapo ikasabisha kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Jopo ya hospitali ile, Profesa Mugenda. Vile vile, mkurugenzi msimamizi Dr. Adan pia ikabidi ...
view
3 Dec 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni Ya Kudumu No.53(1) ya Kanuni za Seneti kuomba kauli kutoka kwa Kamati ya Leba na Ustawi wa Jamii, kuhusu kucheleweshwa kwa malipo ya uzeeni ya wafanyikazi wa Shirika la Kenya Aerotech, waliostaafu. Bw. Spika, katika kauli hiyo- (1) Kamati itoe orodha ya majina ya wafanyikazi wa Shirika la Kenya Aerotech waliostaafu kutoka mwaka wa 2002 mpaka leo, ikionyesha ni wangapi wamepata malipo yao ya uzeeni na wangapi hawajapata. (2) Ieleze sababu za kucheleweshwa kwa malipo hayo kwa wafanyikazi waliostaafu, hususan Bw. Mohamed Abdala Harusi ambaye alistaafu mnamo 31/12/2022. ...
view