Moses Masika Wetangula

Parties & Coalitions

Born

13th September 1956

Post

Employment History:
Advocate of the High Court of Kenya -
Wetangula & Co. Advocates of Kenya

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

mwtangula@gmail.com

Telephone

0722517302

Link

@wetangulam on Twitter

Moses Masika Wetangula

Speaker of the National Assembly in the 13th Parliament.

He was the Bungoma Senator (2013 - 2022; Leader of Minority in the Senate (2013 - 2017)

By virtue of his position as co-principal in NASA he was retained as Minority Leader in the 12th Parliament but later replaced by his Siaya counterpart after 19 senators who attended Nasa's Parliamentary Group meeting at Parliament Buildings in Nairobi unanimously voted to replace him with Senator James Orengo on 15th March, 2018.

All parliamentary appearances

Entries 91 to 100 of 6535.

  • 22 Dec 2021 in Senate: Bw. Spika, asante sana kwa kunipa fursa hii kuchangia yale wenzangu wamesema tunapofikia kikomo cha muhula huu wa mwaka huu. Kwanza ni kukushukuru wewe Bwana Spika na kikundi chako, wakiwemo Naibu Spika, Sen. (Prof) Margaret Kamar na wale wenzetu waliomo kwa jopo la Spika na ambao mara kwa mara huchukua nafasi ya kukaa katika kiti chako na kuongoza mijadala ya Seneti hii kwa njia ya heshima na ambayo inastahili sifa. Mwaka huu wote hatujawai kuwa na taharuki yoyote katika Bunge hili; hata wakati ambao tulikuwa tumeganyika kuhusu ugavi wa pesa, ilifanyika kwa njia ya heshima. Kila mtu alitoa maoni yake, ... view
  • 22 Dec 2021 in Senate: kuwa hata tukibishana kutafuta viti vya uongozi, mwisho wa mabishano lazima tulinde amani ya nchi yetu. Tuhakikishe ya kwamba akina mama, watoto, walemavu na wale ambao kwa njia moja au nyingine hawajiwezi au ni wanyonge, wawe na nafasi ya kulindwa na sisi sote. view
  • 22 Dec 2021 in Senate: Bw. Spika, mwaka huu umekuwa na changamoto haswa kwangu na wewe pia kwa sababu tunatoka kaunti moja. Unajua kuwa tulimpoteza Mbunge wetu wa Kabuchai. Nashukuru Maseneta ambao walituma pole zao. Tulimzika na kwenda kwa uchaguzi mdogo ambapo tulimchagua mrithi wake na sasa tunaendelea vizuri. view
  • 22 Dec 2021 in Senate: Kibinafsi pia nilimpoteza ndugu yangu mdogo kwa huu ugonjwa wa Korona. Kwa hivyo, tukizungumzia Korona, mjue kwamba wengine wetu tumefikiwa na ugonjwa huu. Nilimpoteza mama ndogo na nawashukuru sana nyote mliotuma rambirambi zenu. view
  • 22 Dec 2021 in Senate: Bw. Spika, Mungu yuko na Mungu hubaki Mungu, hana jina lingine. Wale wakorofi waliotaka kuvuruga chama chetu cha FORD-Kenya, walishindwa vibaya. Tukikutana na wale ambao walikuwa wanawaunga mkono, wana haya na hawataki kutusalimia. Wanatoroka wakituona kila mahali tukienda. view
  • 22 Dec 2021 in Senate: Nataka kuwashukuru hawa ndugu zetu wote hapa Seneti ambao kwa njia moja au nyingine walikuwa wakija kwangu pole pole kuniambia: “tuko pamoja na wewe, tunakuombea na hii utashinda.” Na tulishinda! view
  • 22 Dec 2021 in Senate: Bw. Spika, wale ambao wameshindwa tunawaambia tumewasamehe lakini hatutasahau, kwa sababu wamejifanya kuwa vibaraka wa wengine na kwa siasa ya nchi yetu hatutaki vibaraka. Tunataka watu wenye msimamo, heshima na wale wanazingatia demokrasia katika maisha yao kibinafsi, katika vyama vyao na katika nchi yetu. view
  • 22 Dec 2021 in Senate: Bw. Spika, tukielelekea katika uchaguzi mkuu, tunakuunga mkono vile umekuwa ukisema mara kwa mara ya kwamba tunahitaji uchaguzi wenye usawa, haki, ukweli na amani. Hii ni kwa sababu nchi yetu imepitia changamoto kubwa ya mabishano ya uchaguzi mwaka wa 2007 mpaka tukapoteza maisha na mali ya Wakenya. view
  • 22 Dec 2021 in Senate: Bw. Spika, tukiangalia nyuma, ile funzo tumesoma ni kujua ya kwamba katika mabishano ya kisiasa, uchaguzi ukiisha tunabaki kuwa Wakenya na lazima tuendelee kufurahia na kujivunia kuwa Wakenya. view
  • 22 Dec 2021 in Senate: Kwa polisi wetu, tunaenda kwa hafla za Krisimasi. Tunawaomba mfanye kazi kusaidia wananchi ili tusiwe na misongamano isiyo na maana katika barabara zetu. Tupunguze ajali ili Wakenya wanaotoka hapa jijini kwenda mashinani, iwe ni Pwani, kaskazini au magharibi na popote pale, waweze kusafiri bila kuhangaishwa na majambazi barabarani au bila kurundikana na milolongo ya magari kwa sababu ya kutoajibika kwa polisi wanaolinda trafiki kwa barabara. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus