Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 356.

  • 14 Nov 2024 in Senate: Asante sana, Mstahiki Bw. Spika wa Muda. Ingekuwa ni kongamano la walala hoi, maskini ama la makata, Mswada kama huu haungeona mwanga. Lakini katika kongamano la wanaojiweza, madingi na matajri, ni rahisi sana Mswada huu kupita bila shida yoyote. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Sisi wote tulioko hapa kama Maseneta bila kuogopa kwamba sisi sio maskini. Mshahara tunao na bima ya afya tunayo. Lakini tusisahau ya kwamba chanzo kubwa cha harambee zinazofanywa kule mashinani ni kwa sababu ya ukosefu wa afya, karo ya shule ama kwa wale waliopatwa na msiba na hawawezi hata kulipa fedha ili wapewe miili ya wapendwa wao waende wakaomboleze kwa amani. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Waswahili husema, aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa mimi kumbi. Aliyenipa kiti nilichokalia leo kufanya uamuzi katika Mswada ndio pia amewapa wale maskini tunaowawakilisha kumbi ambalo ni ganda la nazi waweze kukalia. Kwa hivyo, tusisahau hilo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Mambo yale sisi hapa tunaweza kufanya bila shida yoyote ndio inawatatiza wananchi kule mashinani. Kama tutakuja kutengeneza Mswada, kama tutawabomolea daraja, lazima kwanza tuwafunze kuogelea. Ni lazima kwanza tutatue shida za afya kwa kuhakikisha kwamba Social Health Insurance Fund (SHIF) inafanya kazi, malipo ya shuleni kuanzia shule ya chekechea hadi chuo kikuu yapo. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Najua hakuna atakayetusumbua na mambo ya kutoa fedha katika harambee. Waswahili husema, “Kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.” Hakuna anayelazimishwa kwenda kutoa. Mtu hutoa kwa hiari yake. Swali nauliza, mzigo ulio kichwani, kwapa lakutokeani jasho? Kama sijalazimishwa mimi kutoa fedha, kwa nini nianze kutengeneza sheria ya pesa ambayo inatolewa na mtu anayetoa kwa hiari? view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Matatizo ambayo yako hapa yanamkumba sana mwananchi wa kawaida. Na siku ambayo mbwa anatua katika sehemu nyeti, hiyo ndio siku mtu hujua sio kila tatizo huwa linatatuliwa kwa fimbo au nyundo. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Shida tuliyonayo saa hii sio lazima itatuliwe kwa sheria. Ni tatizo ambalo linafaa kutatuliwa kwa kuweka miundo msingi mbele ili wananchi waweze kuendelea. Sheria kama hizi ndio wakati mwingine hufanya wananchi wajiulize kama waliweka chui zizini. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Wakati tunapoomba viti, wanaotushikilia ngazi ni wale wananchi wa kawaida. Unajua, mtu anayehusika kupandisha wengine ngazi hupigwa teke kwa meno kwa sababu anayemshikilia anaenda juu ilhali miguu iko chini. Kwa hivyo, ni rahisi sana kumpiga teke kwa meno. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Hivyo basi nasema ya kwamba, mimi kama Seneta wa Kirinyaga, nikikaa katika baraza, wale wanaokalia kumbi na vigogo, vile wanavyoongea kuhusu shida walizonazo, mimi nitakuwa kama mtu wa kuwapiga teke kwa meno nikisema huu Mswada unafaa kwa wakati tulionao kwa sasa. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Mambo ambayo mimi nimeyapitia, na wengi wanaokaa katika Seneti, naweza kudhihirisha ya kwamba wanaoketi hapa wengi walipita na kusoma kwa sababu watu walikuja pamoja kwa harambee wakawachangia pesa. Kwa hivyo, ile njia iliyowapitisha kuwafanya walivyo siku ya leo, mimi naomba tusije tukaifunga. Kwa nini? Angalia mtu aliyefiwa kwa sababu ya kukosa matibabu. Mwili unafungiwa makafani kwa sababu familia haina pesa ya kuutoa. Labda mwendazake alikufa kwa sababu ya ukosefu wa matibabu. Kama tungelainisha maneno na kuhakikisha kuwa matibabu yanapatikana, pengine tungezuia vifo na hakuna mtu angeitishwa pesa. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus