Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 356.

  • 14 Nov 2024 in Senate: Najua kuwa mnachangia sana kulipa karo za wanafunzi kwa kupeana bursary . Tumeongea sana kuhusu jambo hilo. Kuna Mswada unaonuia kufanya elimu kutoka kiwango cha chekechea hadi chuo kikuu bila malipo. Mswada huo ukiwa sheria, hakuna mtu atatuita kwenda kuchangisha pesa ya watoto kwenda shuleni. Kwa nini tusianze na kutengeneza sheria ambazo nimetaja? Kule kwetu, kuna msemo kuwa anayekula kwa kijiko huwa hajui kuchomeka kwa anayekula kwa mikono. Kama sisi tuna bima, hatuna matatizo na hatutaki kuchangiwa, tusisahau kwamba wanaoitisha msaada wana shida na wanafaa kusaidiwa. Bw. Spika wa Muda, kwa kumalizia, nilipokuwa nimeketi hapa, nilipata jumbe kadhaa za watu ... view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Mimi kama Seneta wa Kirinyaga, kwa sababu ya watu wa Kirinyaga na Kenya nzima, kwa wale wote ambao nimeongea nao na wale wanaoketi katika mabaraza kuongea shida zao na kutualika sisi kwenda kuwapa msaada, kwa ajili ya akina mama na wale ambao wamejiunga katika vikundi kule Kirinyaga ili kuchangisha pesa kusaidia waliofiwa, sitaunga mkono Mswada ulio mbele yetu. view
  • 13 Nov 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Ili nifike hapa mapema nilitoka nyumbani kumi asubuhi. ndio nipate nafasi ya kujadili kuhusu mengi hususan yanayohusu Wizara ya Afya ambayo ni muhimu sana katika nchi hii. Tunaweza jenga barabara na mambo mengi lakini hatuwezi yatekeleza majukumu haya kwa wafu. Wanaotumia hizo huduma ni waliohai. Namwombea Daktari Hon. Barasa apone haraka na apate nafasi ya kuja kujibu maswali. Waswahili husema kiserema hulima kuliko jembe jipya. Yeye ni daktari, kwa hivyo ni mzoefu wa mambo yanayolingana na hospitali na basi majibu ambayo tungepata saa hii yanafaa kusuluhisha maswali yote yaliyoulizwa. La kutatanisha sana ni majibu ya Waziri ... view
  • 13 Nov 2024 in Senate: Hon. Rebecca Miano. Samahani nimepewa taarifa isiyo ya kweli na rafiki yangu hapa. Bw. Naibu Spika, Hon. Miano hakuwa mgonjwa lakini ameamua kuenda kuweka vifaru, vifaa vya ufuatiliaji katika hifadhi ya wanyama pori. Katika taratibu ya wanaombeba na uzito, anatuchukulia kwa bei rahisi kama bei ya chumvi. Ameweka vifaru kwanza halafu Bunge la Seneti linafuata. Kwa nini hangempa mwengine jukumu hilo? Nina uhakika kuwa sio yeye anaweka vifaa hivyo. Tumepoteza nafasi ya kuongea kuhusu kinachoendelea katika serikali. Waswahili husema ukikalia kuti kavu kuanguka sio ajali na--- view
  • 13 Nov 2024 in Senate: Bw. Naibu Spika, kusiwe na mazoea ya Mawaziri kukataa kuja hapa baada ya kualikwa. Waswahili pia husema kuti la mazoea humwangusha mgema. Mawaziri hawa wataanguka kwa sababu ya kuzoea kukosa kuja hapa. Asante. view
  • 12 Nov 2024 in Senate: Asante sana Bw. Spika. Kulingana na Kanuni ya Kudumu ya 159(1) ya Bunge la Seneti, naomba kuondoa katika Ratiba, The Rice Bill (Senate Bills No.19 of 2023). Sababu kuu ni ili tushauriane na wahusika wakuu wakiwemo wakulima na wote wanaohusika ili kuwasilisa huu Mswada katika Seneti kwa safari moja. Asante sana. view
  • 17 Oct 2024 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Kwanza ningetaka kumuombea afueni haraka Naibu wa Rais. Ningependa kusema hivi, fisi anapotaka kula mwanawe, husema kwamba ananuka kama mbuzi. Ni dhahiri shairi kuwa, mashtaka iliyo mbele yetu leo ni fisi anayetaka kumla mwanawe. Wakati Sen. Thang’wa alikuwa anaongeo hapa, leo ulimwambia uombe msamaha. Alikuwa amemwambia Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Jinai kwamba anapojibu, ajibu na wanao. Mashtaka ambayo imekuwa na kampuni zote zilizokuwa hapa, mingi zilikuwa za watoto wake Rigathi Gachagua. Ama kweli, chambilecho, mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu. Kwa sababu hakuwezi kuwa na ubaguzi wa wanawe Naibu Rais, lakini kusiwe wale wengine ... view
  • 17 Oct 2024 in Senate: Mimi nimetoka Kirinyaga na ninajua mashtaka yote 11 ambayo yako hapa. Kuna jambo moja ambalo mpaka ufanye kama utadhihirisha hayo mashtaka na ni ushiriki wa umma ambao tuko na ushahidi mbele yetu. Katika ushirika wa umma ambao tuko nao mbele yetu, isipokuwa picha za maofisi za National Government – Constituency Development Fund (NG –CDF) na takwimu ambazo zimetoka katika Bunge la Kitaifa. Hii ni kwamba wale wote ambao walikuwa wametia sahihi kumuondoa Naibu wa Rais ndio walio ongoza katika ushiriki wa umma. Bw. Spika, ningeuliza itakuwaaje na itawezekanaje mtu ambaye ametia sahihi kumuondoa Naibu wa Rais anaongoza katika ushiriki wa ... view
  • 17 Oct 2024 in Senate: kuzingatia ushahidi na kuangalia kila jambo na maombi ambayo tuko nayo katika Seneti kuwa wenye haki na uaminifu. Asante sana. view
  • 17 Oct 2024 in Senate: Asante, Mhe Spika. Swali langu litaeenda kwa Bw. Abdi. Kwa sababu anayehukumiwa hapa ni Naibu wa Rais, tungetaka kujua ya kwamba kwa sababu mlifanya uchunguzi, ni kesi ngapi ama kuna kesi yeyote ambayo EACC imepeleka mahakami ili Naibu wa Rais ahukumiwe? Jambo la pili, wakati Naibu wa Rais alikua anachunguzwa katika Bunge la Kitaifa, kuna ushaidi wowote ambao wewe uliwasilisha? Kama hukuwasilisha, kwa nini umeamua kuwasilisha hapa Bunge la Seneti na sio Bunge la Kitaifa? Swali la mwisho, katita zabuni ambayo ilikuwa ni ya vyandarua vya mbu ambayo inasemekana Naibu wa Rais alihusika nayo, ile zabuni ilikuwa imeghairiwa na KEMSA, view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus