12 Mar 2025 in Senate:
Seneta wa Busia ni rafiki yangu lakini wakati mwingine ana cheche. Kwa hivyo, nitamruhusu kidogo aniambe anachotaka kusema.
view
26 Feb 2025 in Senate:
Asante sana Mstahiki Bw. Naibu Spika. Ningependa kumuuliza Waziri kama amesikia kilio, masikitiko na uchungu wa walimu. Walitozwa ada ya Bima ya Afya ya Taifa, lakini ada hiyo ikaenda kwa Hazina Kuu ya Serikali na hazikufikia zile hospitali wanazofaaa kuenda kutibiwa. Bado wako na kandarasi na bima zingine zinazofaa kuwasaidia katika mambo ya matibabu. Je, anajua haya? Na kama anajua zile shida zilizo na walimu, amefanya nini ili kusuluhisha ili waalimu wapate huduma? Asante sana.
view
26 Feb 2025 in Senate:
Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. My question is very short. I am contented with the answer that I got from the Cabinet Secretary. However, I will go ahead and read it. (1) Could the Cabinet Secretary highlight the programmes in the health sector that will be affected by the decision by the American Government to withdraw funding from aid-funded health care programmes in the country with particular focus on how such withdrawal affects the health sector in Kirinyaga County? (2) Could the Cabinet Secretary provide a breakdown of the budget for the affected programmes in the country? (3) What ...
view
26 Feb 2025 in Senate:
Mr. Temporary Speaker, Sir, I have no supplementary question. Thank you.
view
25 Feb 2025 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Ni jambo la fedheha wakati wakulima wanapanda, kupalilia mimea na wanapovuna hawapati walichokuwa wanatarajia. Hili ni jambo linalotokana na makadirio ya bajeti ambayo yanafanywa na Bunge la Kitaifa. Sasa hivi ukiangalia fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kununua mahindi utapata kiasi. Ukiangalia fedha kwenye bajeti ambazo zimetengwa kwa sababu ya ngano, utapata hakuna. Pia hakuna pesa zilizotengwa kusaidia wakulima wa mimea mingine. Wakati wakulima watavuna, hata Mhe. Rais wa nchi atasema nendeni mnunue ngano. Hata hivyo, kwa sababu wakulima hawa hawana soko, utapata kuwa hakuna bajeti. Jambo la kusikitisha ni kuwa hakuna mahali Seneti inahusishwa kikamilifu ...
view
12 Feb 2025 in Senate:
Asante sana Spika wa Muda. Nitakuwa mchache wa maneno na mzito kwa hoja. Naomba kutoa tasfida na kauli yangu kuhusu Taarifa ambayo imewasilishwa na Seneta wa Nairobi City County, Sen. Sifuna. Wiki jana nilipatana na mawimbi makubwa sana wakati nilikuwa nakosoa utendakazi wa Gavana wa Kirinyaga, kwa sababu ya ukosefu wa matibabu na kunyanyasa maafisa wa ugani ambao wanatembea wakiangalia wagonjwa vijijini. Tabibu wale wa ugani wanatembea kwa mguu kama mawakala wa ng’ombe. Hawana njia yeyote ya usafiri ya kuwafikisha vijijini ambapo watu wetu kama vile nyanya zetu wanaishi. Wamepewa kazi na mikoba mizito ambayo wanafaa kuzunguka nayo. Wamebeba mizigo ...
view
12 Feb 2025 in Senate:
Bw. Spika wa Muda naomba usaidizi wako kwa sababu kuna tasfida inayoendelea hapa---
view
12 Feb 2025 in Senate:
Sen. (Dr.) Khalwale, unaitwa na Spika wa Muda.
view
12 Feb 2025 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda. Wale maafisa wa ugani wamepewa kazi ngumu na mikoba mizito ambayo wanabebeshwa mithili ya punda wakizunguka wakiangalia wagonjwa katika vijiji vyetu ilhali hawajalipwa kwa miezi mingi. Hili ni jambo la busara kuhakikisha kwamba wengine wanapolipwa, hawa pia wanalipwa ili wafanye kazi yao kwa ufasaha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
12 Feb 2025 in Senate:
Ni sawa ata kama Gavana hatajenga barabara. Afadhali akose kutoa mbegu au pembejeo za kilimo lakini ahakikisha kuwa afya imefikia kila mtu, kwa sababu aliyekufa hatumii barabara zilizoundwa wala kulima. Wanafaa kuwachana na mambo yote ile wanayofanya na wahakikishe kuwa wakaazi wote wako hai. Baada ya kuleta taarifa ambayo tulituma kwenye Kamati ya Afya ambayo inaongozwa na Sen. Mandago, kumekuwa na mambo mengi ambayo yanafanywa kuonyesha kwamba sisi hatujui tunachofanya. Pale kwenye mlango pamewekwa mama na mzee ambao wanakupiga pambaja na kukushika mashavu ili picha zile zirushwe katika vyombo vya habari ionekana kana kwamba magavana wanafanya kazi. Kweli sisi huchaguliwa ...
view