26 Feb 2025 in Senate:
Mr. Temporary Speaker, Sir, I have no supplementary question. Thank you.
view
25 Feb 2025 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Ni jambo la fedheha wakati wakulima wanapanda, kupalilia mimea na wanapovuna hawapati walichokuwa wanatarajia. Hili ni jambo linalotokana na makadirio ya bajeti ambayo yanafanywa na Bunge la Kitaifa. Sasa hivi ukiangalia fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kununua mahindi utapata kiasi. Ukiangalia fedha kwenye bajeti ambazo zimetengwa kwa sababu ya ngano, utapata hakuna. Pia hakuna pesa zilizotengwa kusaidia wakulima wa mimea mingine. Wakati wakulima watavuna, hata Mhe. Rais wa nchi atasema nendeni mnunue ngano. Hata hivyo, kwa sababu wakulima hawa hawana soko, utapata kuwa hakuna bajeti. Jambo la kusikitisha ni kuwa hakuna mahali Seneti inahusishwa kikamilifu ...
view
12 Feb 2025 in Senate:
Asante sana Spika wa Muda. Nitakuwa mchache wa maneno na mzito kwa hoja. Naomba kutoa tasfida na kauli yangu kuhusu Taarifa ambayo imewasilishwa na Seneta wa Nairobi City County, Sen. Sifuna. Wiki jana nilipatana na mawimbi makubwa sana wakati nilikuwa nakosoa utendakazi wa Gavana wa Kirinyaga, kwa sababu ya ukosefu wa matibabu na kunyanyasa maafisa wa ugani ambao wanatembea wakiangalia wagonjwa vijijini. Tabibu wale wa ugani wanatembea kwa mguu kama mawakala wa ng’ombe. Hawana njia yeyote ya usafiri ya kuwafikisha vijijini ambapo watu wetu kama vile nyanya zetu wanaishi. Wamepewa kazi na mikoba mizito ambayo wanafaa kuzunguka nayo. Wamebeba mizigo ...
view
12 Feb 2025 in Senate:
Bw. Spika wa Muda naomba usaidizi wako kwa sababu kuna tasfida inayoendelea hapa---
view
12 Feb 2025 in Senate:
Sen. (Dr.) Khalwale, unaitwa na Spika wa Muda.
view
12 Feb 2025 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda. Wale maafisa wa ugani wamepewa kazi ngumu na mikoba mizito ambayo wanabebeshwa mithili ya punda wakizunguka wakiangalia wagonjwa katika vijiji vyetu ilhali hawajalipwa kwa miezi mingi. Hili ni jambo la busara kuhakikisha kwamba wengine wanapolipwa, hawa pia wanalipwa ili wafanye kazi yao kwa ufasaha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
12 Feb 2025 in Senate:
Ni sawa ata kama Gavana hatajenga barabara. Afadhali akose kutoa mbegu au pembejeo za kilimo lakini ahakikisha kuwa afya imefikia kila mtu, kwa sababu aliyekufa hatumii barabara zilizoundwa wala kulima. Wanafaa kuwachana na mambo yote ile wanayofanya na wahakikishe kuwa wakaazi wote wako hai. Baada ya kuleta taarifa ambayo tulituma kwenye Kamati ya Afya ambayo inaongozwa na Sen. Mandago, kumekuwa na mambo mengi ambayo yanafanywa kuonyesha kwamba sisi hatujui tunachofanya. Pale kwenye mlango pamewekwa mama na mzee ambao wanakupiga pambaja na kukushika mashavu ili picha zile zirushwe katika vyombo vya habari ionekana kana kwamba magavana wanafanya kazi. Kweli sisi huchaguliwa ...
view
3 Dec 2024 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kwanza naunga mkono taarifa kuhusu wakulima wa miraa. Ningependa kuwafahamisha kwamba kuna miraa inayotoka eneo la Meru na muguka kutoka kaunti za Embu na Kirinyaga. Wakati soko la hiyo bidhaa linatafutwa, ni vizuri wakulima hawa wawakilishwe. Tumeongea kuhusu wakulima wa miraa kwa sababu ni muhimu. Lakini ni vizuri pia tukae pamoja kama viongozi kuzungumzia usafirishaji wa miraa. Kama viongozi, tunafaa kuongea na wale wanaosafirisha miraa ama muguka kwa sababu wanasababisha harasa kubwa sana katika eneo la Kirinyaga. Wiki hii tumezika watoto wawili waliogongwa na gari linalosafirisha miraa. Kila mwaka takwimu inaonyesha wazi kwamba wale wanaobeba ...
view
3 Dec 2024 in Senate:
Lakini gari zinazosafirisha miraa zinaovertake mpaka ambulance zinayopeleka watu hospitali. Ni vizuri kuwe na airport itakayojegwa karibu na maeneo ya miraa ili iwe inasafirisha miraa kwani itaokoa muda na uhai.
view
3 Dec 2024 in Senate:
Ni vizuri viongozi kutoka Meru, Embu na mahali muguka inakuzwa kukaa na vitengo vya usalama na polisi wa trafiki wanaokaa katika zile barabara ili tupunguze hasara kubwa za ajali zinazosababishwa na gari za miraa. Mimi ni mkereketwa mkubwa wa kuunga mkono ukulima sanasana wa miraa. Lakini tunaona kuna hasara na vilio na vizuri tuangalie mambo hayo pia.
view