26 Nov 2024 in Senate:
pale Sagana. Kwa muda mrefu sana imefikisha hadhi ya kupewa JuniorSecondary ambayo kwa sasa wamekuwa cleared . Nilikuwa nimetuma barua hata kwa waziri na kwa sababu mambo ambayo inasemwa, mwenye kuenda pale kufanya kazi ya mkono ni hao mawaziri na makatibu katika zile wizara. Pia ni vizuri waangalie na kuhakisha ya kwamba zile shule zinahitaji kupandishwa hadhi zipandishwe ili watoto wasikuwe wakienda safari ndefu sana kuenda kutafuta Elimu. Nikimalizia, nitasema kwamba mimi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uchumi wa Baharini katika kamati ya Seneti, mkulima ni mtu wa maana sana. Tunahitaji mkulima asubuhi tunapotafuta staftahi. Saa nne ...
view
20 Nov 2024 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Ningependa kuongea dakika moja kuhusu Taarifa zilizoulizwa na Sen. Mundingi na Sen. Nyutu. Kwanza, polisi ni muhimi sana katika nchi hii ingawa watu wengi wanalalamika na pia nyuki hapigwi busu, polisi pia ni watu. Ukiangalia polisi wanaohamishwa kutoka mahali pamoja kupelekwa pengine, wako na familia zinazovunjika. Polisi anapochukua mtaji na kuweka katika ujenzi wa nyumba mahali pamoja, halafu anatolewa na kupelekwa mahali pengine anapofaa kulipa kodi, inaleta gharama ya ziada ambayo polisi wengi wameshindwa kukimu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained ...
view
20 Nov 2024 in Senate:
Ndio maana mara nyingi unaona polisi wengi wakiwa na matatizo ya kiakili. Hilo ni jambo la maana sana. Polisi wanapohamishwa kutoka sehemu moja kupelekwa nyengine, wanafaa kuridhika na mahali wanapopelekwa na wapewe ridhaa ya kukaa mahali pale. Jambo la pili ni kuhusu Taarifa iliyoulizwa na Seneta wa Kaunti ya Murangá. Katika kikao kilichoisha katika Kamati ya Ukulima, Uvuvi na Uchumi Samawati ambacho mimi ni Mwenyekiti, tulikaa na Waziri na kumwambia kwamba angeongeza makataa ili macadamia iuzwe kwa nchi za ng’ambo. Lakini tangu makataa ilipoisha tarehe mbili, mwezi wa kumi na moja, hakuna jambo limefanyika hadi sasa. Bw. Spika, wakulima wanafaa ...
view
20 Nov 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I beg to ask the Cabinet Secretary for Land, Public Works, Housing and Urban Development the following Question. (a) Could the Cabinet Secretary state the number of persons classified as landless, commonly referred to as squatters in Kirinyaga Central Constituency, Kirinyaga County? (b) What measures has the Ministry put in place to ensure that all squatters across the county, in particular those in colonial settlement villages along Mount Kenya Forest in Kirinyaga County, are resettled? (c) Could the Cabinet Secretary confirm when these squatters will be settled, including when they shall be issued with title ...
view
20 Nov 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ninamshukuru Bi. Waziri pia kwa kujibu yale maswali nimeuliza, lakini niko na maswali mengine mawili. Kirinyaga upande wa Mwea, watu wameishi huko bila hati miliki kwa miaka na mikaka. Nyanyangu nilimzika akiwa na miaka 115 na bado hakuwa na hati miliki kwa sababu ya sheria gandamizi ya kunyunyizia mashamba maji. Swali langu la kwanza, ni juhudi zipi ziko kuhakikisha kwamba wakaazi wa sehemu za Mwera Irrigation Scheme na South Ngariama wamepata hati miliki na ni lini? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained ...
view
20 Nov 2024 in Senate:
Swali langu la pili, katika takwimu Bi. Waziri ameleta siku ya leo, kuna vijiji 5,260 vya ukoloni. Waswahili husema, “mgala muue na haki yake umpe.” Toka zile vijiji za ukoloni mpaka wa leo, wale watu hawana hati miliki ila Bi. Waziri amesema ashapeana takwimu kwa Serikali la Gatuzi la Kirinyaga waanzishe mpango rasmi wa kupeana hati miliki. Mimi mwenyewe niko na kijiji niliachiwa na babu yangu na hakina hati miliki. Huenda nikafa kama sina hati miliki kwa miaka hiyo yote. Ningetaka kuja, hizi hati miliki zitapeanwa lini.
view
20 Nov 2024 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumshukuru Kiongozi wa Walio Wengi kwa sababu ya wazo nzuri. Mswada huu ni wa maana sana. Katika maisha yangu ya awali nimekuwa mwakilishi wa wadi na pia nilikuwa Kiongozi wa wengi katika Kaunti ya Kirinyaga. Kwa hivyo, naelewa masaibu yanayowafikia mawakilishi wadi ama MCAs ambao ni mengi. Kama kuna viongozi ambao wanachukuliwa kwa urahisi, mashinani wako na watu kila siku, wanaobeba mizigo, ambao inafaa wasaidiwe ni wawakilishi wadi ambao ni MCA. Mimi nilihudumu kwa kipindi cha miaka tano; kuanzia mwaka wa 2017 hadi 2022. Katika kile kipindi bado nilikuwa na marafiki wengi. ...
view
20 Nov 2024 in Senate:
Baadhi ya wale madiwani ama councillors ambao wako Kirinyaga mpaka siku ya leo, baada ya Mswada uliopitishwa Bungeni ili walipwe pesa zao za uzeeni. Wengi wameaga dunia na shida nyingi za kiafya. Hawakuweza kujikimu ama kujitunza kwa sababu hawakulipwa pesa zao za uzeeni. Hata kama tunasukuma walipwe pesa zao, leo hii nasimama hapa kusema kuwa wazo hili ni nzuri kuhakikisha kwamba viongozi wetu baada ya kustaafu ama kukamilisha vipindi vyao vya huduma kwa wananchi hawapitii shida ambazo wengi wanapitia. Bw. Spika wa Muda, leo hii mimi kama Seneta nahudumu kwa kipindi cha miaka mitano. Nikibahatika kurudi katika Bunge hili, nitakuwa ...
view
19 Nov 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I beg to give the following Notice of Motion- THAT, the National Assembly amendments to the Cotton Industry Development Bill (Senate Bills No. 5 of 2023) be now considered. I thank you.
view
14 Nov 2024 in Senate:
Asante sana, Mstahiki Bw. Spika wa Muda. Ingekuwa ni kongamano la walala hoi, maskini ama la makata, Mswada kama huu haungeona mwanga. Lakini katika kongamano la wanaojiweza, madingi na matajri, ni rahisi sana Mswada huu kupita bila shida yoyote.
view