27 Oct 2024 in Senate:
Tunafanya hivi kwa sababu katika gatuzi zetu ndiko umaskini mwingi uko. Watu wengi wanaishi kwa kaunti zetu. Hivyo basi, huko mashinani ndiko tunahitaji barabara nyingi, maji, ukulima na madaktari. Jambo la kwanza ambalo sisi kama Seneti tunapaswa kufanya ni kuhakikisha tumemuuliza Rais kwa heshima ahakikishe kuwa amegatua fedha na yale majukumu ambayo yamegawiwa kaunti. Pili, magavana wamekuwa wakisema kila wakati kuwa hawajapata pesa kutoka kwa Serikali na pia mishahara haijawafikia. Lakini, tungependa kuwaambia ndugu zetu magavana kuwa Wakenya sio wajinga sasa. Wakenya wanajua ni wakati gani Serikali inatoa pesa na wakati ambao fedha hizi hufika kwa gatuzi zetu mashinani. Magavana ...
view
27 Oct 2024 in Senate:
katika Kaunti yangu ya Kisii, kuna shillingi bilioni tisa na laki tatu. Lakini, Gavana wangu amekuwa akiambia watu hakuna pesa. Waliokuwa wakandarasi hawajalipwa, wafanyikazi wa kaunti wanafutwa kazi na wengine kuajiriwa. Hakuna mambo yanaendelea. Hakuna barabara na mvua kwa sasa imenyesha. Ukiangalia zile shida ziko kwa kaunti zote kama vile Sen. Cherarkey alikuwa anasema, kwa heshima utamwambia Gavana wako ya kwamba pesa mimi ndimi nimeuliza, nikazichunga, zikaja na sasa ziko kwa account . Tafadhali, tumia hizi pesa usaidie watu wetu. Ukifanya hivyo, anakutafutia goons . Wanakuja na panga na wengine na bunduki. Ooh, huyo Seneta anataka kutunyang’anya ugavana wetu, ooh, ...
view
27 Oct 2024 in Senate:
zingine bilioni kumi na sita ama kumi na mbili ndizo hubaki za kuwafanyia wananchi kazi. Hamna madawa hospitalini, miradi iliyokuwa inaendelea ya maji haifanyiki, pesa zote zinazotoka kwa donors zimesimamishwa katika Kaunti ya Kisii, kwa sababu vigezo vyote ambavyo vimekwa na wafadhili vimekiukwa. Gavana alipoingia huko alitoa wale waliokuwa wakitia signature na kuweka watu wake. Hakujua sheria inasema hawezi kufanya hivyo. Ukiuliza walimu wa shule za chekechea, hawajalipwa mishahara. Wengine mishahara yao ni minimum wage . Utamuajiri aje mtu afunze mtoto wako kutoka darasa la kwanza hadi la tatu au la nne, ilhali unamlipa shilingi elfu saba? Huyu ni mtu ...
view
27 Oct 2024 in Senate:
. Baada ya kuingiza ujumbe katika IFMIS, CoB na Ministry of Finance and Economic Planning wanafanya
view
27 Oct 2024 in Senate:
kisha wataeleza kazi aliyofanya yule anayetaka kulipwa. Vile vile, wataeleza
view
27 Oct 2024 in Senate:
na development budgets. Magavana wanafunga watu hao wasilipwe, halafu wanaleta kampuni ambazo wanataka. Wanaleta watu wanaojua na jamaa wao kupewa kandarasi na kuwalipa na kuacha waliofanya kazi miaka mitatu, minne au mitano iliyopita. Shida iliyo Kenya ni hiyo. Kuna maendeleo ambayo tunazungumzia. Katiba yetu ya 2010 ilinuia kuleta usawa katika nchi yetu. Ilinuia kuondoa ufisadi katika maendeleo ya Wakenya, ili tuweze kumaliza umaskini nchini mwetu. Kwa sasa, Serikali ya Kitaifa inachukua asilimia 85 na kupora na kuwapa magava asilimia 15 iliyosalia ambayo pia wanapora. Jiulize ni kina nani wana majumba makubwa kule Kilimani. Magavana wengine wanadhani kuwa wananchi ni wajinga. ...
view
27 Oct 2024 in Senate:
wanayomiliki, lakini hatuwezi kuwa na huruma kwa watu wetu? Ni zaidi ya miaka 60 tangu tupate Uhuru, lakini watu wengine hawana maji ya kunywa. Tulikwenda kule Turkana ambako anatoka Sen. Lomenen. Kufikia sasa, Turkana imepata shilingi bilioni 110, ilhali watu hawana maji ya kunywa mijini baada ya miaka kumi tangu kuwa na ugatuzi. Ni kinaya kuwa hali ni hiyo ilhali kuna maji mengi kutoka Mto Turkwel. Kinachotakikana ni maji kusambazwa kwa wananchi. Wamepata shilingi bilioni 110, ilhali watu hawana maji! Kwa miaka miwili sasa, Kaunti yangu ya Kisii imepata shilingi bilioni 32. Hata hivyo, ukienda kule hamna chochote. Uwanja wa ...
view
27 Oct 2024 in Senate:
kutoka kwa hospitali ndogo ndogo na kubwa kubwa kwa sababu wananchi hawana njia nyingine. Gavana wa Murang’a amefanya kazi nzuri. Anatumia teknolojia kukusanya ushuru kutoka kwa wale ambao wanajenga ama wana nyumba na wale ambao wana-park magari huko. Aliongeza mapato yake kutoka shilingi milioni 200 mwaka uliopita hadi shilingi bilioni 1.5. Sababu ni kuwa wale walio katika kamati ya maendeleo ni vigogo ambao wamekuwa wakifanya biashara kama vile mmiliki wa Benki ya Equity. Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii.
view
17 Oct 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I have two questions to hon. Mutuse. I hold you highly and I do not think you are as idiotic as our colleagues will say. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
17 Oct 2024 in Senate:
Between the time when the Deputy President was a Member of Parliament (MP) and the time when he became the Deputy President, were you able to see whether there was a deliberate variation in the amounts of money that he was handling? Did you see whether the money that he was handling as an MP, for example, changed then to the money that you brought in, where you are saying that there is some money laundering taking place? Are you able to show that distinction in order for you to make your case? The second question is on the same ...
view