26 Oct 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kusema kwamba utovu wa usalama nchini Kenya umekuwa jambo la kuhuzunisha. Umeumiza watu wengi katika jamii nyingi. Hivi tunavyozungumza, tumepoteza watu wengi kwenye visa vya wizi wa mifugo, hali ambayo imesababisha kudorora kwa usalama katika nchi hii. Tunapozungumzia Kerio Valley, na haswa maeneo ya Tot, Marakwet, Pokot, Tiaty na Pokot Magharibi, tunafaa kufahamu kwamba haya ni maeneo ambako usalama umedorora. Nimeishi katika sehemu hiyo, na ninaelewa jinsi hali vilivyo. Kuuawa kwa watu kiholelaholela ni jambo la kuhuzunisha sana. Kifo ni tukio la kawaida. Kifo kinapowatembelea kulingana na mpango wa ...
view
26 Oct 2016 in National Assembly:
haupo? Matokeo ya mitihani ya wanafunzi katika shule za Tot na Chesegon yatalinganishwaje na matokeo ya mitihani ya wanafunzi katika sehemu nyingine humu nchini? Hakuna atakayekumbuka kwamba watoto wengine walifanya mitihani kwenye mazingira ambayo hayakuwa na usalama. Matokeo ya mitihani ya watoto kote yatasawazishwa kutumia vigezo sawia bila ya kujali kwamba watoto wengine waliathirika kwa sababu ya kukosekana kwa usalama. Tunaomba usalama uimarishwe katika sehemu hizo kwa sababu wakazi hawana utulivu ama usalama. Hatuwezi kukosa suluhu. Ninaamini ya kwamba tuna uwezo wa kumaliza shida hiyo. Watu wengi wameuchangia mjadala huu, wakiwemo wakazi wa sehemu hizo wenyewe. Kwa hivyo tunaomba sheria ...
view
26 Oct 2016 in National Assembly:
Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii ili masuala ya usalama yaweze kupewa uzito unaostahili.
view
12 Oct 2016 in National Assembly:
Thank you very much, Hon. Temporary Deputy Speaker. First, I congratulate Hon. Odanga for bringing this timely Motion to this august House.
view
12 Oct 2016 in National Assembly:
Chaplains are trained people who have the word of God in their hearts. Having the background of a teacher and having learnt the psychology of children, I know that from conception to the age of going to school, a child learns something from the parents. If this continues in school, where we have chaplains, it will make a child a whole person.
view
12 Oct 2016 in National Assembly:
Chaplains have to be trained and qualified people so that they can handle children at different stages, especially in primary and secondary schools. Children have to be taught the word of God and social life lessons as they grow up. It is really important for us, as a country and as a nation, to bring up our children in the right way. Hon. Temporary Deputy Speaker, these days you can bear me witness that most of our children get spoiled mainly in schools. The character of a child can be good at home but immediately he or she joins secondary ...
view
4 Oct 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika, ningependa kuungana na wenzangu kutoa pole zangu pamoja na jamii yangu na Wapokot wote kwa jamii ya Mhe. Marehemu Litole. Najua Mhe. Marehemu Litole alihudumia nchi hii katika nyanja mbali mbali ya mwisho, katika Bunge la Kumi. Alifanya kazi nyingi zaidi katika Kaunti ya Pokot ambayo amewacha alama. Kwa hivyo, natoa pole zangu na Mungu amurehemu.
view
23 Jun 2016 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, ningependa kukushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili niungane na wenzangu kuunga mkono Mswada huu wa barabara. Barabara ni muhimu katika nchi yetu ya Kenya. Maisha ya mwanadamu yanaenda pamoja na barabara. Ninasema hivyo kwa sababu pasipokuwa na barabara nzuri hata ugonjwa ukitokea watu wengi huangamia. Ninaposema hivi asilimia kubwa ya barabara katika nchi hii ziko katika hali mbaya. Tunapoangalia sehemu nyingi katika Kenya, tunaona kwamba watu wengi hutatizika na hata vyakula kuharibika wakati wa mvua kwa sababu ya barabara mbaya. Unakumbuka kwamba mara nyingine mitihani inachukua muda na inakosa kufanywa siku ile imepangwa kwa sababu ...
view
23 Jun 2016 in National Assembly:
eneo hilo na hivi sasa, tuna usalama baina ya Turkana na Pokot. Ninaamini tutapata barabara nyingi zaidi. Ningependa kuzungumzia juu ya wale ambao wanapewa kandarasi. Kazi nyingi zinarudiwa kwa sababu wale ambao wanapewa kandarasi hawafanyi kazi nzuri. Tunaporudia ile kazi tunatumia pesa za Serikali. Inafaa wale ambao wamepata kandarasi watengeneze hizo barabara kwa njia ambayo itafanya barabara zidumu kwa muda. Barabara nyingi hutengenezwa kiholela na mvua inaponyesha, zinaharibika na pesa za nchi zinatumika kuzirekebisha.
view
23 Jun 2016 in National Assembly:
Serikali ya Jubilee imejaribu na ninatumai tutaendelea kufanya kazi nzuri zaidi kuliko ilivyo sasa. Kule Pokot, tumeahidiwa kutengenezewa barabara tatu na ninaamini kuwa zitatengenezwa kwa muda mfupi ili zisaidia wananchi kusafirisha vyakula vyao. Katika eneo la Pokot Kusini, kuna vyakula vingi haswa maziwa. Maziwa na matunda huharibika kwa urahisi. Barabara inapoharibika na magari yanapokwama, vyakula vyote vinaharibika na jambo hili husababisha hasara na uchumi kuharibika. Wananchi wanaumia kwa sababu wanategemea mapato kusomesha watoto wao. Barabara ni maisha ya wananchi na wasipotengenezewa barabara, nchi haiwezi kusonga mbele. Wananchi hawawezi kufanya biashara kama barabara ni mbaya.
view