11 Dec 2014 in National Assembly:
Mhe. Spika, nitaomba uniongezee dakika mbili ambazo zimepotea hapo. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Huu ni wakati wa kushughulikia mambo ya usalama. Miezi kadhaa iliyopika, kunashambulizi ambalo lilitokea kwa matatu katika Barabara ya Thika na miongoni mwa waliokufa ni kijana mmoja aliyekuwa ametoka kwangu. Alikuwa na mke wake ambaye aliumia miguu mpaka sasa hivi, hawezi kutembea. Kila siku anaenda hospitali na imetubidi kurudi kwa mifuko yetu ili tumchangie. Amewachwa mjane na mlemavu kwa wakati huu. Juzi, tulihudhuria mazishi ya dada huko Kieni ambao waliuawa. Ungekuwa miongoni mwa wale waliohudhuria hayo mazishi, haungejaribu kuzipinga sheria hizi. Miezi kadhaa iliyopita, Kiongozi wa ...
view
11 Dec 2014 in National Assembly:
Ilisemekana kuwa Serikali imekataa.
view
11 Dec 2014 in National Assembly:
Mhe. Spika, haya mapendekezo ambayo yameletwa na Serikali ya Jubilee; ni mapendekezo gani ambayo yameletwa katika Bunge hili na ule upande ambayo yamepingwa na Serikali ya Jubilee? Hakuna mapendekezo ambayo yameletwa na Upinzani.
view
11 Dec 2014 in National Assembly:
Mhe. Spika, jambo la pili ni kuwa huenda kuna mapendekezo ambayo yanatashwishi hapa. Ni nani amekatazwa kuleta mabadiliko ili kubadilisha na kutengeneza hii sheria wakati ufaao? Hakuna mtu ambaye amejaribu kufanya hivi. Wale ambao wanapinga haya mapendekezo wameguzia vifungu kama vitatu. Kwa kweli, tumesikia maoni yao. Mwenyekiti wa kamati ya Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani amesikia. Ataangalia kuhusu mambo ya mikutano kama hiyo ambayo iko na shida na kutaletwa mapendekezo ya kubadilisha mambo haya. Kwa hivyo, ninawaomba wenzangu wote tushikane ili tuyashughulikie mambo ya usalama katika nchi hii. Mwaka jana, tuliipatia Serikali pesa nyingi sana kwa upande wa ...
view
11 Dec 2014 in National Assembly:
hongo, anastahili kufungwa. Hivi majuzi nilikua Mombasa, nikaongea na jamaa mmoja akaniambia ametoka Rwanda lakini akatoa kitambulisho akaniambia alikinunua hicho kitambulisho kwa Kshs10,000 pekee. Mnasema yule ofisa ambaye alipeana kitambulisho tusimhukumu? Mnasema huyo mtu mwenye kitambulisho hicho tusimnyang’anye? Hizi sheria ambazo ziko hapa ni muhimu sana. Tupatie Rais na askari wetu uwezo wa kushughulikia hawa maharamia. Wacha wamalizwe kabisa. Hivyo ndivyo ninasema.
view
10 Dec 2014 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Speaker, I will also begin by congratulating my colleague. We are in a security crisis in this country and just as the National Police Service (NPS) itself is being put under a microscope, it is important that we also look at the Commission. The duty to provide security to this country has been given to two institutions; the National Police Service and the National Police Service Commission. Since they have failed, just as we are carrying out a radical surgery in the National Police Service, it is also important that we carry out radical surgery in the ...
view
10 Dec 2014 in National Assembly:
I support the intention to deal with that Commission.
view
10 Dec 2014 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono huu mjadala na Mswada ambao mhe. Lekuton ametuletea. Huu Mswada umeletwa wakati muhimu na unanihusu kwa sababu mwaka jana, niliwapoteza wanafunzi wanne wa St. Peters katika eneo langu la Bunge la Kipipiri. Wanafunzi hao waligongwa na gari ambalo lilikuwa linaenda kwa kasi sana na likatoka barabarani na likawakuta kando ya barabara na wakafariki. Ulikuwa ni wakati wa majonzi sana. Katika mwaka huu pia, tumewapoteza mwanafunzi wengine wawili kule Manunga. Kwa hivyo, sheria hii itakuwa muhimu sana kuhakikisha kuwa watoto wetu hawauawi, haswa kwenye barabara za lami ambapo magari huenda kwa ...
view
10 Dec 2014 in National Assembly:
Nimeangalia sheria hii na inasema kuwa mahali popote ambapo kuna shule au kituo cha afya, madereva wasizidishe kilomita 30 kwa saa. Pia, wanaohusika na barabara waweke ilani na ishara kuwajulisha madereva kuwa kuna shule au kituo cha afya. Pia, ilani hizi zitaonyesha kiwango cha mwendo ambao madereva wanafaa kuendesha magari yao. Shida ambayo tuko nayo ni kuwa kila wakati, hizo ishara na tarifa zinawekwa lakini wezi wa vyuma wanazing’oa. Madereva wanashindwa kujua ni wapi kuna shule karibu. Katika sehemu ya pili ya sheria hii ambayo Mhe. Lekuton amependekeza iwe hatia kwa madereva, ningeomba tuseme kuwa ni hatia kupitisha kiwango cha ...
view
10 Dec 2014 in National Assembly:
walimu huko na wanaenda kuvuka barabara peke yao. Hawa ni watoto wadogo kabisa. Sisi kama jamii, tusiwache majukumu yote ya usalama wa watoto kwa Serikali. Tunafaa kuyabeba majukumu yetu ili tuhakikishe kuna usalama. Naunga mkono Mswada huu.
view