6 Mar 2024 in Senate:
Dakika moja tu nimalize. Kitu nilichokuwa nataka kiibuke wazi ni kwamba Mawaziri hawa wanapata nafasi ya kufanya mambo mengine lakini shughuli ya Seneti hawazipatii kipaumbele. Alikuwepo kwenye mazishi. Nimetoka kwenye stesheni ya radio ya Kenya Broadcasting Cooperation (KBC) na wakaniambia walikuwa naye jana katika kituo hicho. Kama anapata nafasi ya kuhudhuria mazishi na kuwakemea viongozi wengine na pia kwenda katika vyombo vya habari, kwa nini asije hapa na sisi tupate fursa ya kuzungumza naye? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard ...
view
6 Mar 2024 in Senate:
Sen. Gloria Orwoba wiki iliyopita alitukemea sana, haswa viongozi wa vyama ambao walishiriki katika Kamati ya Maridhiano ya Kitaifa iliyokuwepo. Aliteta kwamba tuliwacha masuala ya akina mama nyuma. Nilikuwa nataka Bi.Waziri aje hapa adhihirishe kwamba sio kwa kukosa kuwasilisha hoja zetu kama viongozi wa Orange Democratic Movement (ODM ) bali kuna masuala ambayo yalikuwa yanafanyika ndani ya Wizara yake. Kwa hivyo, ni yeye pekee alikuwa anaweza kuniondoa kwa mtego uliokuwa umetegwa na Mhe. Gloria lakini sasa hayupo hapa. Kwa hivyo, mimi ninakemea vikali kukosa kuja mbele ya Bunge kwa Mhe. Aisha Jumwa, haswa kwa sababu wenzake wengine walikuwa na ile ...
view
6 Mar 2024 in Senate:
Heshima! Asante, Bw. Spika. Walikuwa na heshima kwa Seneti kuandika barua kusema kwamba---
view
6 Mar 2024 in Senate:
Ama katesi . Naambiwa unaweza sema katesi .
view
6 Mar 2024 in Senate:
Wakaandika barua kujulisha Wabunge kwamba hawangefika. Bw. Spika, nataka nikuombe ombi moja tu. Wakati tulipokuwa katika mkutano wa SBC, niliuliza swali hilo. Je, kuna njia gani ya kuwajulisha wale ambao wameuliza Maswali mapema kwamba hayatapata kujibiwa kwa sababu Waziri ameandika barua? Nilielezwa kwamba kutakuwa na ugumu kwa sababu wenzetu hawa wakiambiwa kwamba Waziri hatakuja, nao pia hawatakuja. Tungependa Mhe. Kathuri Murungi apambane na hali yake kule Ngong Road afike hapa hata kama Waziri hayuko tuweze---
view
6 Mar 2024 in Senate:
Niko kwa hoja ya Nidhamu
view
6 Mar 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kuniokoa kutoka kwa mikono ya Seneta wa Meru. Kwa kweli mimi ni mwakilishi pale SBC wa hawa wenzangu hapa. Ni muhimu kwamba yote yanayoendelea pale tuwajuze kwa sababu kama vile umesema wewe mwenyewe, hakuna siri. Kwa hivyo, mimi naomba kuwe na mfumo hata kama arafa itaandikwa kwa yule Seneta aliyekuwa ameuliza mwenyewe pasina kuweka paruwanja kama vile ulivyosema. Mwenye kuuliza maswali haya ajulishwe kwamba kwa bahati mbaya ama kwa sababu moja ama nyingine, yule Waziri aliyekuwa anataka kumuuliza maswali hatafika ili watu waweze kujipanga. Ni vizuri tuwe hapa kwa ajili ya shughuli zingine za Seneti. Natumai ...
view
6 Mar 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, for the record, for the avoidance of doubt and to shame the devil, I did, in fact, attend the University of Nairobi for four years.
view
6 Mar 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, you must protect me from the hecklers from lesser institutions, so that I can undertake the mandate you have given me of welcoming the students from the University of Nairobi.
view
6 Mar 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, you can clearly see those who went to school properly and those who did not.
view