15 Aug 2018 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nachukua fursa hii kuunga mkono Hoja ambayo imeletwa na Mhe. Baya, kuhusu fidia kwa wakuzaji wa mnazi. Tunataka tufanyie suala hili marekebisho kiasi cha kwamba fidia hii isielekee katika sehemu ya Kilifi ambayo imelengwa na aliyeleta Hoja, lakini ilenge wakulima wa mnazi wote kwa jumla katika nchi ya Kenya na hasa eneo la Pwani. Hii ni Hoja nzuri sana. Tunahitaji msukumo mkubwa kwa Wizara ya Kilimo na Mifugo. Tukiwa tunaelekeza mwelekeo wetu kulipa fidia kwa wakulima wa mnazi, ni lazima ifahamike kwamba wakuzaji wakubwa wa mnazi wanatoka sehemu ya Kwale katika eneo Bunge ...
view
15 Aug 2018 in National Assembly:
Vile vile, tungeomba na kuiambia Wizara ya Kilimo iweke mfuko fulani ambao kila mwaka, utakuwa unaangalia wakuzaji wote wa mnazi kuwe kuna sehemu fulani ambayo wanapewa msukumo. Kama sasa, tunajua iko mbegu mpya ambayo imekuja katika Wizara hiyo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
15 Aug 2018 in National Assembly:
Kwa lugha ya kimombo, inaitwa dwarf coconut . Mnazi huo, kwa mwaka unatoa mazao mara tatu, ambapo ni faida kubwa kwa mkulima. Naunga mkono Hoja hii lakini ilenge wakuzaji wa mnazi wa eneo lote la Pwani na Kenya yote kwa jumla.
view
1 Aug 2018 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuchangia Hoja ambayo Mhe. Owen ameleta juu ya masuala ya korosho. Ufufuzi wa korosho ni jambo ambalo litasaidia sana sehemu ambazo kwa mara nyingi zimekuwa zikikuza mmea huu kwa muda mrefu kisha ukaachiliwa. Katika sehemu hizo, hali ya umaskini imetanda. Wale wakuzaji wamerudi chini kimaisha. Kwa hivyo, ikiwa Serikali itafufua upandaji wa korosho ninayo Imani kuwa umaskini katika sehemu hizi utapungua. Aidha, moja kwa moja, kutabuniwa ajira katika sehemu ambazo zinakuza mmea huu. Isitoshe, ikiwa ukuzaji wa mkorosho utapewa kipaumbele na uzingatiwe kama mimea mingine inayokuzwa Pwani kama vile miembe na minazi ...
view
1 Aug 2018 in National Assembly:
wingi. Itakuwa vema ikiwa Wizara ya Kilimo itatenga pato maalum la kuhakikisha kila sehemu katika nchi hii, kwa mfano, Tharaka Nithi, Pwani na kwingineko kunakokuzwa korosho kujengwe viwanda vidogo vidogo na wakulima wawezeshwe kuuza mapato yao. Kupitia Wizara ya Kilimo tunafahamu kwamba kuna mbegu maalum ambazo zimeletwa ambazo wakulima watapatiwa. Mbegu hizo ni za mkorosho na mnazi. Aidha mbegu hizo zikipandwa zinakua kwa miaka mitatu. Wizara ya Kilimo ikifaulisha upeanaji wa mbegu hizo, tuna imani kuwa katika miaka mitatu hali ya maisha ya watu wetu itabadilika. Nikimalizia, Mhe. Mbogo wa Kisauni amesema kwamba korosho zinaliwa katika ndege lakini nataka nitofautiane ...
view
29 Nov 2017 in National Assembly:
Asante sana Mheshimiwa Spika. Nimesimama kuhusu orodha kamili ya majina yaliyotolewa, ambayo yanawakilisha mrengo wa NASA kwenye uongozi wa Bunge hili. Msimamo wangu ni kwamba ninaupinga moja kwa moja. Kwanza, suala la jinsia halikuzingatiwa kabisa. Pili, hii imeashiria wazi kwamba uongozi wa chama umeelekezwa Nyanza pekee na sehemu nyingine zote zimeachwa nje.
view
29 Nov 2017 in National Assembly:
Hali hii inatuonyesha wazi kwamba uongozi wa muungana wa NASA unapopangwa ni lazima wanachama waitwe kwenye kikao. Ni wazi kwamba taratibu inayotakikana ifuatwe wakati kunapangwa uongonzi haikufuatwa. Nilazima wanachama waitwe kuhudhuria kikao, kwa lugha ya kimombo cha Parliamentary Group (PG). Na hii haikufanyika. Kwa hivyo, mimi kama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
29 Nov 2017 in National Assembly:
mwenyekiti wa wabunge wa Pwani hili swala tunalipinga kwa sababu sisi kama Wapwani tumechangia sana mlengo wa NASA. Mhe Spika, hii ni wazi kwamba sisi kama Wapwani na watu wa sehemu zingine hatutambuliwi katika hii chama. Tunasema wazi kwamba kama Wapwani tunayapinga haya majina kikamilifu na tutasimama kuyapinga na hatuyatambui tuta resist kama vile wao wana resist . Asante sana.
view
3 Aug 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ninataka kukupongeza kwa uchaguzi wako katika Ofisi ya Spika. Pili, ninataka kuunga Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Mwadime. Maji ni muhimu sana kwa mwanadamu, na sisi tuna jukumu katika suala la maji. Ni lazima tuhakikishe shule zimepata maji, na tusiangalie suala hili kama ambalo limegatuliwa. Ni jukumu la Serikali kuu pamoja na serikali za ugatuzi kuangalia suala hili kwa utaratibu kwa sababu watoto wetu wanaadhirika kwa ukosefu wa maji.
view
20 Jul 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii nichangie Hoja hii ambayo ni muhimu sana na inahusu wazee wetu wa vijiji. Kwanza, nataka kutoa hongera kubwa zaidi kwa Mheshimiwa Malulu kwa kuokoa ndoto ambayo imesumbua sana wazee wetu wa vijiji. Kwa hakika, wazee wa vijiji ni watu muhimu sana katika taifa letu la Kenya. Kwa maoni yangu, nataka niseme ya kwamba, wazee wa vijiji ni wana muhimu zaidi ya machifu na manaibu wao, ambao wanawakilisha ofisi za utawala. Nataka niunge mkono Hoja hii moja kwa moja. Mimi ndiye muathiriwa mkubwa. Wazee wa vijiji wameathirika katika hali ya utendakazi ...
view