8 Jun 2016 in National Assembly:
On a point of order, Hon. Temporary Deputy Speaker.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Naibu Spika wa Muda. Kulingana na wakati, inaonekana ya kwamba wengi wetu hatutapata fursa ya kuchambua Hoja hii. Ningeomba dakika zipunguzwe mpaka dakika tatu.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Ahsante, mhe. Naibu Spika wa Muda. Moja kwa moja, ninaiunga mkono Hoja hii, ambayo imeletwa na mhe. Lay. Kabla sijaendelea, ningependa kumpa Mbunge wa Kisauni, mhe. Bedzimba, dakika moja na nusu ya. Mhe. Naibu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Spika wa Muda, Wakenya wengi wanaitambua lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, ni muhimu, kama viongozi, kutambua umuhimu wa Hoja hii. Mfano nzuri ambao nitauzungumzia leo ni tofauti zinazoibuka wakati tunapoleta Bungeni Miswada iliyobuniwa kwa Kiswahili na ile iliyobuniwa kwa Kiingereza. Kwa hakika, kule mashinani, wananchi hutiririka kwa wingi kutazama runinga mjadala unapofanywa kwa Kiswahili. Kwa hivyo, ninawaomba viongozi wenzngu; tuipe kipa umbele Hoja ili tuhakikishe kwamba Kiswahili kimeimarishwa humu nchini.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii na kumpa fursa mhe. Bedzimba.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Ahsante, mhe. Naibu Spika wa Muda. Kiswahili ni lugha ambayo ina umuhimu kwetu sisi Wakenya. Ni lugha ambayo inatuelekeza katika shughuli zetu za kila siku. Kwa hakika, idadi kubwa ya Wakenya hutumia Kiswahili katika kila jambo wanalolifanya kwa sababu hiyo ndiyo lugha ambayo inafahamika vyema. Kwa hivyo, tunapotunga sheria na kufanya jambo lolote, ni lazima tufahamu kwamba wakenya ndio muhimu. Tunafaa kuhakikisha kwamba jambo hili limefahamika.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Kwa hivyo, ninaiunga mkono Hoja hii.
view
26 Nov 2014 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama ili kuchangia suala la usalama. Mwanzo natuma risala za rambirambi kwa familia zilizoathirika na mambo ya usalama. Ni jukumu letu sisi Wabunge kuangalia mambo muhimu ya usalama na kuyaelekeza kwa wananchi wetu. Kwa hakika, wakati umefika kwa Bunge hili kuacha maslahi ya kisiasa ambayo yametanda na kuangalia maslahi ya nchi hii. Ni jukumu letu sisi viongozi kuhakikisha tumelinda usalama wa nchi hii. Kama tunavyojua, Bunge lina kazi tatu; ya kwanza ni kuwakilisha, ya pili ni kutunga sheria na ya tatu ni kuwa macho ya Serikali. Suala la usalama limetatiza. Kila wiki tunakuja ...
view
26 Nov 2014 in National Assembly:
walio wengi, tunasema kwamba, ikiwa suluhisho ni majopo haya mawili yaungane ili nchi yetu itapate uokozi, tuko tayari kuungana. Lakini tusichukue suala la makosa ya wale walio kwenye uongozi tukaanza kulaumu upande ambao hauwezi kufanya lolote. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni jukumu letu, kama viongozi, kuhakikisha tumelinda Wakenya. Tusije hapa kila wiki ikawa tunazungumzia mambo ambayo hayaleti mwelekeo wowote kwa Wakenya. Wakenya wametuchagua. Wakenya wana imani na viongozi na ni lazima tuwatendee kazi Wakenya. Misikiti ambayo imefungwa, nyumba za maombi ni nyumba ambazo ni lazima zipatiwe heshima. Ni nyumba dini zote mbili zinaamini ni nyumba takatifu. Kwa hivyo, tusiingize ...
view
27 Aug 2014 in National Assembly:
Thank you, hon. Speaker. On behalf of hon. Awiti, I wish to request a Statement from the Chairperson of the Departmental Committee on Administration and National Security regarding housing conditions of the regular and Administration Police (AP) officers in the country.
view
27 Aug 2014 in National Assembly:
Hon. Speaker---
view
28 May 2013 in National Assembly:
Hon. Deputy Speaker, I just wanted to bring to your attention the mood in the House. I support this Motion and say that we need to bring it to an end.
view