15 Oct 2013 in Senate:
Bw. Naibu Spika, wakati Sen. Kiraitu Murungi alipokuwa akiongea kwa Lugha ya Kiingereza, nilidhani Kiingereza chake ni tofauti kabisa na cha Sen. Kajwang. Matamshi ya lugha yoyote hutegemea mazingira anamokulia mtu. Si makosa yangu kuwa na ulimi mzito. Mimi sijui mnavyotamka jina la kwanza la Bi. Serem. Mimi namjua kama Hasara Serem. Kwa hivyo, ni juu yenu kutafakari ninaongea juu ya nani. Hilo ndilo jina nilalolijua. Nikiliandika jina lake chini ni Sarah Serem. Lakini ninapolitamka linakuwa ni Hasara Serem. Hauwezi kuongea mambo ya commission bila kuongea mambo ya Hasara Serem. Tunamjua kama mama aliye na watoto na familia yake, lakini ...
view
15 Oct 2013 in Senate:
Ninakushuru sana, Bw. Naibu Spika. Pengine utaniongezea muda wangu. Mbunge wa mashinani au Bunge la Kaunti anapata mshahara wa Kshs40,000 kwa mwezi. Pesa hizi ni za mahitaji yake yote. Wabunge wa mashinani hutembea umbali wa kilomita nyingi ili wafike katika bunge zao. Sehemu fulani wanatembea zaidi ya kilomita 200 na kila siku ni lazima wahudhurie vikao katika bunge zao. Tunajua sheria vizuri; ni lazima kulipa unapokula. Hakuna cha bure katika nchi hii. Ni aibu iliyoje kuwa mwisho wa mwezi, hawana chochote cha kupelekea familia zao. Tume ya SRC imekosa heshima kwa viongozi waliochaguliwa na wananchi kule mashinani. Tume hii hughugulikia ...
view
15 Oct 2013 in Senate:
Naunga mkono yote yaliyosemwa na mwenzangu aliyenitangulia hapa. Sisi tunafaa kupitisha Hoja ya kutokuwa na imani na Tume ya SRC. Makomishna wa Tume hii ni watumwa. Watumwa hawana makosa lakini wale wanaowatuma ndio wenye uamuzi juu ya mishahara. Ikiwa waliweza kusuluhisha suala la mishahara ya Wabunge siku moja kwa nini wasifanye hivyo huko mashinani? Kwa nini hawaoni jambo na kulisuluhisha mara majo? Wamekuwa vipofu na hawasikii. Kwa hivyo, Bi. Serem ametumwa na Serikali ya Jubilee. Kwa nini hamtaki tuseme ukweli? Pengine kiongozi wa walio wengi hapa Seneti ambaye ametoka upande wa Serikali ya Jubilee ataleta Mswada hapa wa kusuluhisha janga ...
view
15 Oct 2013 in Senate:
Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono.
view
9 Oct 2013 in Senate:
Bw. Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kuunga Hoja hii na kumpongeza mwenzangu, Sen. Karaba, kwa kuleta jambo ambalo ni la hekima, haswa kuangalia mazingira sehemu tofauti tofauti nchini, sehemu zingine za nyanda za juu na zikiwa na milima mingi. Jambo hili linaweza kutekelezeka kwa kuleta Hoja ya kuomba Serikali Kuu ili iweke halmashauri ya kuangalia jambo la kutengeneza gari za waya. Ningependa kuunga mkono na kusema kwamba hili jambo laweza pia kufikiriwa na Serikali ya Ugatuzi. Hivi leo mkiangalia kwa magazeti na vyombo vya habari, serikali za ugatuzi zimeshindwa kutumia hela. Hela zimefurika kwa benki, sijui ni ...
view
9 Oct 2013 in Senate:
Nashukuru, Bwana Naibu Spika. Naunga mkono Hoja iliyoletwa na mwenzangu, Sen. Daniel Karaba. Anaiomba Seneti hii ifikirie na kutafakari kuunda njia za ziada katika barabara za jiji letu la Nairobi. Wahenga walisema; “kwa sababu ya kukosa mikono, ng’ombe alijikunia ulimi.” Tunajipata katika hali hiyo tunapokuwa na shida ama majonzi tukitaka kufika katika kituo cha usaidizi hapa jijini. Shida hii haimo hapa tu bali katika miji yote nchini. Jiji la Nairobi lilijengwa kuanzia 1901 wakati wa ujenzi wa reli. Wakati wa ujenzi wa hoteli ya Norfolk, ilitabiriwa kwamba kungekuwa na magari 300 ndani ya jiji hili. Kwa hivyo, jiji lilijengwa kwa ...
view
9 Oct 2013 in Senate:
Nashukuru Serikali iliyopita kwa sababu aliyekuwa Rais Mzee Kibaki aliiteuwa Wizara ya Maendeleo ya Jiji la Nairobi. Sijui kama mawazo hayo yamefunikwa na Serikali ya sasa. Kama yamefunikwa na Serikali ya sasa, basi yanafaa kufunuliwa. Hayo yalikuwa mawazo mazuri. Jiji hili na miji mingine kama vile Kajiado, Machakos na nyingine inafaa kufanyiwa mipango mipya ya ujenzi. Nafasi inafaa kuwepo ya kujenga barabara ambazo zinaweza kutimiza maendeleo ambayo nchi hii imefikia. Nchi kama vile Amerika na zingine zimeshafanya hivyo. Twahitaji uchumi wa kutosha lakini Mungu si adhumani. Ametuangazia nafasi ya kupata mafuta, makaa na sasa hivi tunapata hata dhahabu Migori. Uchumi ...
view
9 Oct 2013 in Senate:
Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika. Je, ni haki kwa mwenzangu kuchanganya Kiswahili na Kiingereza? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
9 Oct 2013 in Senate:
On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. Is the Leader of the many in order to take your role, by telling a fellow Senator that she is out of order?
view