Willy Mtengo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 21 to 26 of 26.

  • 17 Mar 2016 in National Assembly: Nawahakikishia watu wa Malindi kwamba nitakufa nao kuhakikisha tumeleta maendeleo Malindi ili watoto wa Malindi wasome, wakulima wa Malindi wafanye kilimo chao wanavyotaka, wavuvi wavue samaki watakavyo, akina mama wetu waende kwenye hospitali na zahanati zetu na kupata huduma muafaka, usalama udumike, barabara zijengwe na maendeleo yakithiri. Hayo ndiyo yaliyonileta ndani ya Bunge hili. Mhe. Spika, nasema kuwa sheria zilizoundwa ama zinazoundwa ndani ya Bunge hili la Kitaifa ni sharti zifuatiliwe. Tuliona vitimbi wakati wa uchaguzi mdogo wa Malindi. Mambo hatujawahi kuyaona. Tuliona vitisho, kupigiwa kifua na pesa nyingi, lakini tulichukua msimamo na tukasimama. Nawaambia Wakenya enzi za kuona vitimbi ... view
  • 17 Mar 2016 in National Assembly: Naomba ulinzi wako Mhe. Spika. view
  • 17 Mar 2016 in National Assembly: Mhe. Spika, singetaka mji wetu wa Malindi ambao ni uchumi wetu, uchumi unaotegemea utalii, uharibiwe sifa. Sasa, ukichukua askari na kuwaweka ndani ya mji wa utalii, si ni kuwatisha? Ujumbe ambao tunatuma upande ule mwingine ni ujumbe wa kutatanisha. Haya ni maswali ambayo ningependelea na kuomba tupate majibu ndani ya Sakafu hii ya Bunge, kama Mbunge wa eneo Malindi. Wale watu walikuja kwa minajili gani? Vifaru vya jeshi siku ya kura tena kando ya vituo vya kupiga kura vililetwa kwa minajili gani? Baada ya vituo kufunga, askari wote walitoroka. Vifaru vingi viliondoka na vichache vikabaki kwa vituo vya kupiga kura. ... view
  • 17 Mar 2016 in National Assembly: Mhe. Spika, natoa kongole kwa ofisi nyingine mbali na ofisi yako. Hapa Bunge wamenipokea vizuri. Nimefanyiwa mapokezi mazuri na bado naendelea kama Waheshimiwa wengine. Nashukuru. Nashukuru Wakenya na kuwaomba watusaidie. Kwa ule muda nimekaa hapa, nimeona kazi ya kutunga sheria ni ngumu. Nawaambia wenzangu wa upande ule mwingine kwamba ni sharti tushirikiane kwa sababu tuko hapa kuwapa Wakenya huduma. Nataka kuingia mlengo wa historia njema. Tuwape Wakenya huduma ili tuwe na sura ya kuangalia wananchi wetu tutakaporudi mashinani kuomba nyadhifa za uongozi. view
  • 17 Mar 2016 in National Assembly: Ahsante. view
  • 17 Mar 2016 in National Assembly: Mhe. Spika, nataka niwaambie wale wachache walio wanafiki waliofikiria vibaya na waliokuwa wakisambaza porojo za kusema Malindi ni yao: “Ng’ooo!” Malindi ina wenyewe na watu wa Malindi waliongea. Tunawangoja. Hata mkaja leo, bado tutawanyoa. Wembe ni ule ule wa kutu. Msimamo ni ule ule. Nawashukuru Wakenya wote. Nachukua fursa hii kuwaambia wenzetu ambao kidogo wameanza kuteleza kwamba tunawakaribisha nyumbani. Tuweke siasa kando. Tulete maendeleo kwa watu wetu wa Malindi. Mwenyezi Mungu atulinde. Mwenyezi Mungu atubariki. Ahsante, Mhe. Spika. Mtengo aliwatenga kule Malindi. Ahsanteni. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus