(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Order! We are not properly constituted to start business of the House and so I do order that the Quorum Bell be rung for 10 minutes.
Order Members! Order! Allow those who are walking in, hasten your steps. Hon. Members, I confirm that we have the numbers for us to start the business.
(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Very well, the Leader of Majority Party you have Papers to lay in Order No.5.
Hon. Temporary Deputy Speaker, I beg to lay the following Papers on the Table of the House: The Reports of the Auditor General and Financial Statements in respect of the following institutions for the year ended 30th June 2020 and the certificates therein: (a) Parliamentary Joint Services; (b) Railway Development Levy Fund (Holding Account), Ministry of Transport; (c) Kenya Local Loans Support Fund; (d) Judicial Service Commission; (e) The State Department for Culture and Heritage; (f) State Department for Immigration and Citizen Services; (g) The State Officers' House Mortgage Scheme Fund; (h) The Revenue Statements for the State Department for Interior; and The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
(i) National Humanitarian Fund. Summary of the Report of the Auditor General for the National Government for the year 2018/2019. Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker.
(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Very well. Next we have the Chairperson, Select Committee on Delegated Legislation.
Hon. Speaker, I beg to lay the following Papers on the Table of the House: Reports of the Select Committee on Delegated Legislation on its consideration of: (a) Legal Notice No. 15 of 2021 on the Exemption from Income Tax for Japanese Companies, Japanese Consultants and Japanese Employees. (b) Legal Notice No.27 of 2021 on the Exemption from Income Tax for Airlines with Government of Kenya Shareholding of at least 45% and its Subsidiaries; and (c) The Public Finance Management (National Drought Emergency Fund) Regulations, 2021, published as Legal Notice No.27 of 2021. Thank you.
(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Very well. You lay the Papers. Next Order!
(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): We have Notices of Motions from the Chairperson, Committee on Delegated Legislation.
Hon. Temporary Deputy Speaker, I beg to give notices of the following Motions: THAT, this House adopts the Report of the Committee on Delegated Legislation on its consideration of Legal Notice No.15 of 2021 on Exemption from Income Tax for Japanese Companies, Japanese Consultants and Japanese Employees, laid on the Table of the House on Thursday, 13th May 2021 and pursuant to the provisions of Section 13(2) of the Income Tax Act approves Legal Notice No.15 of 2021 on Exemption of Income Tax for Japanese Companies, Japanese Consultants and Japanese Employees.
(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Very well. Next Order!
(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Mtoa Hoja na Mdhamini ambaye ni Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi.
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba kuwakilisha Hoja ifuatayo: KWAMBA, kwa mujibu wa Kanuni ya 25 (Mgeni Mashuhuri), Shukrani za Bunge la Taifa zinakiliwe kwa ajili ya Hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyotolewa katika Kikao cha Pamoja cha Bunge la Jamhuri ya Kenya mnamo Jumatano, tarehe 5, Mei, 2021. Mnamo Jumatano, tarehe 5 mwezi huu wa Mei mwaka huu wa 2021, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyekuwa katika ziara rasmi ya hapa Kenya kwa mwaliko wa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta alihutubia Bunge hili katika kikao cha pamoja tukiwa Bunge la Taifa na Bunge la Seneti. Kikao hiki kilifanyika kwa mujibu wa Kanuni zetu za Bunge ikiwa Kanuni 25 ya Bunge la Taifa na Kanuni 26 ya Bunge la Seneti. Mhe. Rais Suluhu Hassan alitoa Hotuba ya ufasaha, ya kueleweka na yenye ujumbe mzito kwetu sisi tukiwa Wabunge wanaowakilisha wananchi wa Kenya na haswa kwa sababu ya uhusiano wa mataifa yetu mawili. Alitoa mifano mingi na kuchora taswira iliyofanya ujumbe wake ueleweke kwa wepesi. Pia alitufunza mengi haswa katika lugha ya Kiswahili. Alitupatia misamiati ya kutosha, sasa tunajua “ushoroba wa pwani” unamaanisha “ coastal corridor” . Kabla ya siku hiyo, ni Mhe. Naomi Shaban aliyekuwa anaulewa msamiati wa ushoroba wa pwani. Pia majina kama “adhimu” na “rea” yalitumika. Heshima adhimu aliyopewa na Rais and rea ni respect . “Mikakati hasi” ina maana ya negative measures or strategies ambazo hazisaidii. Kuna mafundo ambayo sijui kama Kiongozi wa Chama cha Walio Wachache anaweza kutuelimisha kwa sababu kama unavyoona, ameingia mitini. Rais Suluhu pia alituonyesha vile amejitahidi kueneza na kutetea lugha ya Kiswahili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hotuba ya Rais Hassan ilisheheni mambo mengi lakini kwa sababu ya uchache wa muda naomba nitaje maswala mawili. Swala la kwanza ni umoja wa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
mataifa yetu mawili au utangamano tukielewa kwamba tuko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki tukiwa nchi sita; Kenya, Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda na pia Sudan Kusini. Kuhusu Kenya na Tanzania Rais alisisitiza kuhusu umoja wetu, tumeshikana kidamu. Sisi ni ndugu wa damu, tumeshikana kupitia historia na jiografia yetu kwa sababu tuna mipaka ambayo huwezi ukaelewa kama uko kusini mwa Kenya ama Kaskazi mwa Tanzania. Ukiwa Arusha na usafiri hadi Taveta unaona hawa watu wote wanashirikiana vizuri. Wao ni jamii na wameshirikiana kwa damu. Hakuna haja ya sisi kutengana kisiasa. Alitushauri tudumishe huu undugu wetu na akasema, kwake yeye na katika awamu yake ya uongozi, atahakikisha kuwa Kenya inabaki kuwa ndugu, jirani na mshirika wa kimikakati na mbia.
Suala la pili ni himizo lake Rais kwamba Bunge liwezeshe biashara kati ya nchi zetu mbili na kuendeleza ushirika kwa jumla tukikumbuka kwamba tuko katika soko huru ambalo ni la nchi hizi sita. Katika mkataba uliowekwa wa kuunganisha nchi hizi na kufungua soko huru, kuna uhuru wa watu kutembea na kufanya biashara. Unaweza kwenda Tanzania kuanzisha biashara na Mtanzania akatoka Tanzania akaja hapa Kenya akaanzisha biashara. Uganda vile vile. Unaweza kununua ardhi na kufanya kazi popote lakini kumekuwa na tatizo. Nilivyomusikia, alisema wakati umefika wa sisi kusema, "Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyo sasa na yajayo". Huu ni ukurasa mpya ambao tunaona unafunguka. Ni sura mpya inafunguka katika ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Kuhusu biashara kati ya nchi hizi zetu mbili, Rais Saluhu Samia Hassan alisema kwamba anaona wafanyabiashara wako mbele. Wametembea hatua kadha mbele ya sisi Wabunge na serikali. Wao wenyewe wametutangulia na ni lazima sisi tukiwa serikali au Wabunge, tuanze kuangalia ni vipi sera na sheria zetu zitawafikia. Hivyo, tutaweza kufanya biashara bila matatizo. Anatuhimiza sisi viongozi katika Bunge na mahakama kuwaonyesha wananchi wetu njia. Tusiwafungie njia za maendeleo na ustawi wao. Mhe. Naibu Spika wa Muda, mimi nafurahia kwamba kupitia uongozi wa Spika wa Bunge letu, Bunge la Taifa na lile la Seneti limepitisha sheria za biashara zinazojulikana kwa kimombo kama Business Laws (Amendment) Bills. Wazo la Mheshimiwa Rais wa taifa letu limekuwa kurekebisha sheria ambazo zinalemaza biashara. Tumewasilisha Mswada mmoja hapa leo wa kueleza vile wawekezaji wa kibinafsi wanaweza kuhusika kwenye miradi ya maendeleo ya umma. Hizo zote tunafanya ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao katika hali na mazingira ambayo yatawastawisha bila wao kupata matatizo. Hivyo basi ni lazima tufuatilie suala la Mheshimiwa Rais ama kwa utunzi wa sheria au maswali kwa Serikali. Mimi ningependa kumshukuru Rais Suluhu Hassan kwa uamuzi wake. Inaonekana wazi amejitolea. Anataka kutatua yale matatizo ya watu kuchukiana hasa kati ya sisi Wakenya na Watanzania. Anataka kuondoa hiyo chuki. Ni njia moja ya kupalilia magugu ambayo yanakua na kuzuia mbegu ambayo ilipandwa ya uhusiano bora. Sharti tuweze kufanya biashara na kuketi kama ndugu. Haya magugu yaliingia na yakaanza kuharibu mahusiano baina yetu. Inaonekana yeye, akishirikiana na Rais wetu Mhe. Kenyatta, wataweza kupalilia hayo magugu ndio uhusiano wetu usiwe mashakani siku za usoni. Labda nitaje kwamba nilifurahia kumsikia Rais Suluhu akitupatia hongera kwa kutafsiri Kanuni zetu za Kudumu katika lugha ya Kiswahili. Juhudi hizi na nyinginezo za kuleta Kiswahili Bungeni zitakuwako. Zitakuza matumizi ya Kiswahili Bungeni. Leo nafurahia kuwaona Wajumbe wengi wakiwa hapa. Kuna wataalamu wa lugha na kuna wengine ni lugha yao ya kwanza. Kwa hivyo, sote kwa pamoja tunaweza kukitumia Kiswahili sio tu katika siasa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
huko mitaani bali pia katika utunzi wa sheria. Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa Rais Suluhu kwa hotuba yake ya kipekee yenye wingi wa hoja na ujumbe wa aina yake. Naomba pia nitoe pongezi zangu kwa Rais wetu Uhuru Muigai Kenyatta, wewe Mhe. Spika, mwenzako Spika wa Seneti, Mhe. Kenneth Lusaka na Wabunge wa Bunge la Taifa na Wabunge wa Seneti kwa heshima waliomwonyesha Rais wa nchi jirani, Rais Suluhu Samia Hassan. Hilo lilifanya kikao hicho kikawa cha kihistoria. Ni kikao cha kupigiwa mfano kwa viongozi watakaokuja siku za usoni. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kuhitimisha kwa heshima, naomba kutoa Hoja na kumwalika Mhe. Naomi Shaban, akiwa mtaalamu wa lugha hii, aweze kuafiki Hoja hii.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Tumpate mwafiki, Mhe. Shaban.
Asante sana, Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi hapa Bungeni. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni heshima kubwa sana kuwa Bunge hili liliweza kumpokea mgeni ambaye alitoka nchi jirani.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Unaomba kuafiki.
Ndio naendelea. Nitaeleza. Katika hali yangu ya kuafiki, natoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wetu Uhuru Kenyatta kwa kumwalika Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Namshukuru haswa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutembele Bunge letu la Kenya. Ningependa kusema kuwa ndugu si kufanana tu bali ni kufaana. Ndugu wa Kenya na Tanzania ni ndugu ambao wamezaliwa... Kama vile Mheshiwa Rais Suluhu Hassan mwenyewe alivyosema, kutengana kwetu hakuwezekani kwa sababu sisi ni ndugu wamoja. Mimi natoka maeneo ya mpakani. Haswa tunapakana pale Taveta na Holili upande wa Tanzania. Sisi ni ndugu kwa sababu ndugu zetu wengine wamevuka mpaka wako upande ule mwengine. Wengine kutoka Tanzania wako upande wetu. Vile vile ndugu wa Kenya wameolewa na wameoa... Vile vile, ndugu wa Kenya wameolewa na wameoa Tanzania. Hivyo basi, kama vile Mhe. Raisi Samia Suluhu alivyosema, mimba yaweza tungiwa Kenya ikazaliwa Tanzania. Ukweli wa mambo ni kuwa, hospitali ya karibu pahali ambapo huwa tunatuma wagonjwa kukiwa kunahitajika matibabu zaidi ni upande wa Tanzania, Kilimanjaro Christian Medical Center ambayo iko upande ule, kwa sababu ndiyo iko karibu kushinda kuenda Voi ambako hutuchukua safari ndefu. Katika hali ya kukaa pale mipakani, hatuwezi kugawa hali ya uchumi wetu kwa sababu hakuna uchumi wa mpaka huu ama mpaka ule. Wakulima wetu wanauza bidhaa zao, haswa vyakula wanavyovuna mashambani, upande ule mwingine na wale pia wanauza bidhaa zao upande huu. Hivyo basi, Mhe. Rais katika hotuba yake akitaja mpaka wa Taveta na Holili ambako kuna ile inatwa kwa Kingereza one-stop-boarder, pahali pamoja pakufanyia shughuli za mipakani, kazi zinazoendelea pale zinaleta faida kwa watu wetu kutoka pande zote mbili. Ningependa kutaja kuwa, sisi tunaotoka mpakani kama Taveta, Mwaka wa 2015 nataka kuwakumbusha kuwa Mhe. Raisi Uhuru Kenyatta alimualika Mhe. Rais Jakaya Kikwete kule Taveta kabla hajamaliza awamu yake. Wakati huo, wakaanzisha ile barabara inayoelekea upande wa Voi. Haya yote yalitendeka kwa sababu ya uhusiano mzuri ulioyoko kati ya Kenya na Tanzania. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
Vile vile, namshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa sababu mwanzo wa ziara zake, ameona kuwa aweke Kenya mbele aipatie nafasi ya awali ili aweze kututembelea. Haya yote hayangewezekana kama siyo uhusiano wetu mzuri ambao una mizizi mirefu sana. Hata Kanuni za Kudumu za hapa Bungeni zilizinduliwa na Bunge la Muungano wa Tanzania. Hatuyachukulii maswala haya kama mchezo. Haya ni maswala ya undugu ambayo tutazidi kudumisha. Ningependa vile vile, kushukuru kuwa Mhe. Rais Mwendazake, John Pombe Magufuli aliamua kumpatia nafasi mama Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa naibu wake. Sasa hivi ndio amepata nafasi hiyo ya kuwa Rais. Alionyesha heshima kubwa kwa akina mama. Vile vile, ningependa kuwashukuru Watanzania kwa hali ya utulivu waliyokuwa nayo kumpokea Rais Suluhu Hassan. Heko kwao. Ningependa kuchukua nafasi hii kama Mbunge wa Taveta kutoa pole kwa kumpoteza Rais jirani wetu, lakini vile vile, kwa sababu nilikua Waziri aliyehusika na mambo ya jinsia, kufurahia kuwa Mama Suluhu amepata nafasi hiyo.
Bila kusema mengi naunga mkono hotuba yake Mhe. Rais Samia Suluhu na kumtakia kila la heri katika kazi nzito ambayo Mwenyezi Mungu amemjalia na ametunukiwa na Watanzania.
Mhe. Spika, naomba kumalizia hapo kwa hayo machache na kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa Bunge hili, limekuja kusalimiwa na mama mmoja ambaye amepata nafasi ya kuwa Rais barani Africa, na si Africa tu, bali Afrika Mashariki. Naafikiana na Kiongozi wa Walio Wengi hapa Bungeni.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Asante sana. Basi Waheshimiwa ni wakati wa kujadili hotuba hii ya Mhe. Rais Suluhu Hassan.
Tuanze na Mhe. ole Sankok David.
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninaunga mkono hotuba hii. Nataka kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mtukufu Rais wa Muungano wa Tanzania. Ningependa kumualika tena na tena ili arudi nchini kwetu kwa sababu kulikuwa na mazuri.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Ukiendelea ningependa kuwakumbusha kuwa kila Mbunge ana dakika tano za kujadili hotuba hii.
Naomba uniongezee dakika zangu. Ningependa kumshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kutuletea Suluhu hapa nchini Kenya. Tulipata suluhu ya ng’ombe zetu kutopigwa mnada hata kama zitavuka mpaka bila pasipoti. Tulipata suluhu za vifaranga kutoteketezwa hata kama watapatikana nchini Tanzania bila pasipoti. Tulipata suluhu ya miundo mbinu za kidiplomasia, ushirikiano, maendeleo na amani. Mhe. Suluhu karibu tena nchini kwa sababu nchi hii ina uhuru; uhuru wa kujieleza, wa kuabudu, kutembea, kuishi na kufanya biashara popote nchini na uwezekano wa vipaji. Mhe. Suhulu, vile nyumbu wa Serengeti wanavyovuka mipaka kutungwa mimba Maasai Mara, ndivyo Wakenya na Watanzania watavuka mipaka kuekeza na kufanya biashara katika nchi zote mbili. Vile nyumbu wa Tanganyika wanavuka mipaka kutafuta mapenzi Maasai Mara bila pasipoti ndivyo Wamaasai wa Kenya watavuka mipaka kutavuta wamaasai wenzao Tanzania bila masharti. Vile wanyama wa Serengeti wanatembeleana na wenzao wa Mara bila pasipoti, ndivyo waendeshaji wa utalii watatembea kuenda Tanzania bila vikwazo vyovyote ili The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
tuimarishe biashara ya utalii. Vile Nyumbu wa Serengeti wanatungwa mimba Maasai Mara na kuzalia Tanzania, ndivyo ng'ombe wa wamaasai watatungwa mimba huku Kenya na kuzalia Tanzania bila masharti yoyote. Mtukufu Rais Suluhu Hassan, ni heshima kubwa sana nikiwa mwakilishi wa wakenya walemavu kuwa mmoja wa Wabunge ambao walisikiza hotuba yako kwa vikao vya pamoja vya Bunge la Seneti na Bunge la Taifa. Ilikuwa heshima kubwa sana na nashukuru sana. Kuwa mama wa kwanza kuwa Rais Afrika Mashariki ni ishara tosha kuwa watu wetu wanadhamini vikundi maalum vya riba, special interest groups kwa kimombo. Kwa mapenzi ya Maulana, mkenya mlemavu atakuwa rais hivi karibuni. Rais Suluhu Hassan, nakubaliana nawe kwamba Kiswahili chetu sio murua kama chenu. Kiswahili chetu kina vioja na vitimbi. Tulipoanzisha rasmi Kiswahili Bungeni, mimi, Mhe. David ole Sankok, nilifikiri Standing Orders zinatafsiriwa kama “Amri ya Kusimama”. Naomba msamaha. Nimejikakamua tangu tuanzishe Kiswahili Bungeni mpaka sasa at least, nimeweza kuongea Kiswahili na nafikiri nitapata alama ya “A”. Asante, naunga mkono.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Asante. Standing Orders zinaitwa ‘Kanuni za Kudumu’. Waheshimiwa, tungependa kupea kipaumbele wenyeviti wa Kamati ya Maswala ya Haki na Sheria, Kamati ya Ulinzi na Uhusiano wa Kigeni, Mhe. Katoo ole Metito, na Kamati ya Utawala na Usalama wa Taifa, Mhe. Peter Mwathi. Hio ni kulingana na Kanuni za Kudumu zetu. Hizo ndio Kamati zinakubaliwa kupewa kipaumbele kupitia Kanuni za Kudumu zetu. Sasa tuende kwa Mhe. wa Suba North, Mhe. (Bi) Odhiambo-Mabona. Mhe. Opiyo Wandayi, wewe sio Mwenyekiti wa Kamati ya Maswala ya Haki na Sheria.
Mhe. Spika wa Muda, mimi ndio Mhe. wa Suba North, sio Mhe. Opiyo Wandayi.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Mhe. Suba North, endelea.
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kiswahili sio mdomo wangu lakini nitaongea leo ili nipongeze mama mwenzangu. Ninajiona mwenye bahati kubwa kupewa nafasi hii adimu na ya kipekee kuongea kuhusu hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan. Hapo nimeongea sawa au sio? Inanikumbusha wakati nilikuwa shule ya msingi ya Homa Bay ambapo Jumatano ilikuwa siku ya kuongea kwa Kiswahili. Watu wengi walikuwa wananyamaza. Wale waliopenda kuongea sana kama mimi walikuwa wananyamaza na kwa wale waliokuwa wanapenda kunyamaza, walikuwa wanaongea. Kwa hivyo, leo tutaona ni akina nani huwa wananyamaza. Leo watajiinua kwa sababu wanajua hatujui Kiswahili, sasa watataka kutushtua. Hio ni sawa au sio sawa? Mhe. Naibu Spika wa Muda, nataka kukubaliana na Rais Suluhu Hassan aliposema kuwa sio kila rais anayefanya ziara rasmi hupewa heshima ya kuhutubia Bunge, tena kikao cha pamoja cha Bunge zote mbili. Tumefurahi, sana sana mimi kama mama Mbunge. Ninamrudishia shukrani kwa kututembelea na namrudishia shukrani Rais wetu Uhuru Kenyatta kwa kumwalika kuja Kenya. Kama mama kiongozi, nilifurahi zaidi kwa sababu yeye ndiye mama wa kwanza Afrika Mashariki kuwa rais. Watu wa Suba North na Tanzania wanashirikiana mpakani mwa Ziwa Victoria. Mara nyingi wavuvi wetu wanashikwa Tanzania. Naomba Rais wetu Mhe. Uhuru Kenyatta aendelee kujadiliana na Rais wa Tanzania ili tusiwe na shida tukifanya uvuvi. Mimi kama mama kiongozi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
ninajiamini kwa vile nimeona kweli urais unaweza kufika kwangu kama mama. Kitu ambacho sikuelewa siku hiyo alipoongea, aliongea ju ya wanyama ambao wanatungwa mimba hapa Kenya na wanazaa Tanzania. Alimaanisha nini, ni wanyama wa Bungeni hapa ama ni wanyamapori? Nafikiri alimaanisha wanyama wa pori. Naona wakati wangu umeisha. Ninarudisha shukrani. Ninafurahia kwa sababu kumbe ninakifahamu Kiswahili. Najidharau tu lakini naelewa na naweza kuongea Kiswahili. Asante na Mungu awabariki na anibariki pia.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Asante, Mhe. Odhiambo-Mabona. Tumeona ukipata usaidizi kwa wenye Kiswahili kutoka upande wa Mombasa. Mhe. kutoka Kaunti ya Isiolo, Mhe. Rehema Jaldesa.
Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii kuchangia mjadala ambao ni muhimu sana, hasa kwa mtu kama mimi ambaye nimetoka kwa jamii ndogo. Nimeweza kupata nafasi ya kuona dada yangu ambaye ni Rais wa pekee katika jumuiya ya Afrika. Hiyo imenifurahisha sana. Nataka nichukue nafasi hii kumshukuru Rais wetu Mhe. Uhuru Kenyatta kwa kumualika Rais Samia Suluhu Hassan. Mhe. Naibu Spika wa Muda, Rais Suluhu Hassan aliongea mengi ambayo ni muhimu kwa sisi Kenya na pia nchi ya Tanzania. Kwanza, aliongea kwa ukarimu sana na utulivu pia. Aliweza kuonyesha ujuzi mwingi kwa yale mambo alikuwa anayasema. Aliongea mengi kuhusu nchi zetu mbili. Kwanza, aliweza kuongea mambo ya uboreshaji wa biashara kati ya nchi zetu mbili. Pili, Rais aliweza kuleta uhusiano bora katika Kenya na Tanzania. Alisisitiza kuwa sisi tumehusiana kwa damu na kijirani pia. Hayo ni mambo ambayo ni muhimu. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kuna wale ambao wametoka kwa jamii ndogo. Mimi ni kiongozi wa Kiislamu ambayo ni jamii haijawahi kukubali uongozi wa akina mama. Rais Suluhu Hassan alikuja Kenya na kuhutubia Bunge letu. Hii ilipeleka graph yetu juu kama viongozi akina mama. Hilo ni jambo siwezi kuchukua rahisi. Imeonyesha ya kwamba sisi, wamama, tunaweza. Aliongea na ujuzi mwingi. Lakini, hapo alikuwa pia anawaonyesha upole. Kwa hivyo, ni jambo ambalo limefurahisha Kenya na dunia nzima. Kama kiongozi mama, nimefurahi sana. Namuombea Mwenyezi Mungu aendelee kuwasha nyota yake.
Mambo yale alituambia ni muhimu. Kwa mfano, alikubali ya kwamba ugonjwa wa Korona upo na akateua jopo ambalo litaangalia mambo kati ya Kenya na Tanzania. Hiyo itaboresha biashara na kufungua mipaka yetu. Kwa hivyo, ni kiongozi ambaye ako na maono. Sisi kama wamama, tunamwangalia. Ametupatia moyo wa kulenga viti vingine kubwa.
Kwa hivyo, nashukuru sana.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Asante sana. Nafasi hii ni ya Mwenyekiti wa Kamati ya Hasibu za Umma, Mhe. Opiyo.
Mhe. Naibu Spika wa muda, naomba uniruhusu nitoe barakoa, ili niweze kuongea vizuri.
Nataka nichukue fursa ili niunge mkono Hoja hii ya maana kwa Bunge hili na taifa kwa jumla. Ni wazi ya kwamba, kuchaguliwa kwa Mhe. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu, ni jambo la kihistoria. Yeye ndiye Rais wa kwanza mama kuchagulia katika eneo hili la Afrika Mashariki. Pongezi kubwa kwake na wananchi wa Tanzania. Kenya na Tanzania wana uhusiano wa muda mrefu sana, uliyoanza hata kabla ya nchi hizi mbili kujinyakulia uhuru. Huo uhusiano umekuwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
ukiendelea, ingawa hapo awali ulikuwa na tashwishi kidogo. Kwa hivyo, kuchukua usukani kwa Rais Suluhu ni jambo la kufurahia. Tumepata nafasi ya kufufua na kuimarisha huo uhusiano.
Nikimpongeza Rais Suluhu, ni lazima nipongeze pia Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta. Hakupoteza wakati hata kidogo. Alichukua hatua haraka kuhakikisha ya kwamba tumetengeneza urafiki na Rais mpya wa Tanzania, Samia Suluhu. Hakuna nchi yoyote katika dunia nzima ambayo inaweza kuendesha shughuli zake kivyake. Nchi zinahitaji ushirikiano katika mambo ya uchumi, jamii na kadhalika. Hakuna nchi hata moja inaweza kuwa kama Island.
Kisiwa.
Asante sana, Mhe. Zuleikha Hassan ambaye ni rafiki yangu na Mbunge wa Kwale kwa kunikumbusha hilo neno muhimu.
Tanzania na Kenya lazima ziendelee kushirikiana kwa manufaa ya watu wa nchi hizi mbili. Kuna watu wetu kutoka jamii mbalimbali katika nchi ya Kenya ambao wako Tanzania. Tutaanza na Wajaluo ambao wako kule Nyanza. Vilevile, kuna Wajaluo wengi sana katika nchi ya Tanzania. Wamaasai wengi wako kule Tanzania. Hiyo ni kumaanisha ya kwamba hatuwezi kujitenga. Vilevile, Watanzania hawawezi kujitenga.
Nikimalizia, nataka nimpongeze Rais Suluhu Hassan kwa kuchukua fursa yake ya kwanza kututembelea na kumwombea heri na baraka katika urais wake nchini humo. Vilevile, nawasihi Wananchi wa Tanzania washirikiane naye. Kama inawezekana, wamchague tena ili amalize mihula yake miwili ya urais. Sisi kama Wakenya, tutabaki na baraka.
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia hii nafasi ili…
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Uunge mkono Hoja hii ama ujadili. Hii nafasi tutampatia Mhe. Maoka Maore.
Mhe. Naibu Spika wa Muda, niwie radhi nitoe barakoa kidogo ndio niweze kupumua vizuri.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Waheshimiwa, hatutavunja sheria zetu za Bunge, hasa kuvaa barakoa. Tunajua wakati huu tu….
Naona niko mbali na Waheshimiwa wengi.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Nimeona ya kwamba Mhe. Opiyo akivaa miwani, barakoa inaleta shida.
Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Suluhu Hassan. Ni baraka kutoka kwa Mungu kuwa na jirani ambaye mnaheshimiana. Ni baraka kutoka kwa mungu kuwa na jirani mwema ambaye ako na manufaa mengi sana. Jirani mwema akiona unanawiri, anafurahia. Tulipokuwa shuleni, tulikuwa na watu kutoka Tanzania ambao walikuwa mashuhuri. Walikuwa wameandika vitabu ambavyo tulikuwa tunavisoma shuleni kama vile Shaaban Robert. Kuna wale wanajua kutunga mashairi kwa mfano, “Titi la Mama Litamu hata Likiwa la Mbwa’’ . Pia, kuna mwingine mashuhuri anaitwa Ibrahim Hussein ambaye ameandika mchezo wa kuigiza ambao unaitwa Mashetani . Kuna msemo ambao naupenda sana na ningependa kuutumia leo: “Mpanda ngazi na mshuka ngazi hawawezi kushikana mikono.” Kwa sababu hiyo, Rais Suluhu Hassan alipowasili hapa, alikuja ili tushikane mikono ndio tuweze kusonga mbele pamoja kiuchumi, kimaendeleo na kidiplomasia. Vile vile, alipotutembelea hapa katika ziara yake, nilipata simu nyingi nikiambiwa kwamba Tanzania haina sheria ambazo zinaweza kuharibu biashara nyingi. Kuna mumea The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
tunaopanda kule kwetu unaoitwa ‘ miraa ’ ama ‘ maurungi ’ kama unavyojulikana huko. Ni vizuri kusema kuwa hapa Kenya, mumea huu ni biashara halali. Lakini ukivuka mpaka upande wa Tanzania, biashara ya miraa ni haramu. Mara nyingi nimejaribu kuwatoa vijana jela kule wakiwa wamefungwa maisha kwa sababu ya kujihusisha na biashara ya miraa . Tunasema kuwa huu ndio wakati wa kupeleka ujumbe kule pole pole ili tujitetee kidogo tusiwe tunaumia. Bi. Naibu Spika wa Muda, kabla ya kuaga dunia kwa Hayati Rais John Pombe Magufuli, hatukuwa tunamfahamu Makamu wa Rais wa Tanzania. Alivyochipuka na kuchukua usukani, wengi walipomskia, waliona ni kiongozi ambaye amejaa taadhima, hekima na ni mwerevu wa akili kuliko viongozi wengi tuliowahi kuwasikia. Rais Suluhu aliweza kuwasisimua Wakenya kwa njia nyingi. Afrika Masharika imepunga hewa tofauti na tunamsifu Mungu kwa kutuletea kiongozi kama huyu kututembelea hapa nchini Kenya. Ahsante, Bi. Naibu Spika wa Muda.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Shukrani. Tuweze kumsikia Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Narok, Mhe. Soipan Tuya.
Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia Hoja hii. Kwanza kabisa ni kutoa shukrani zangu kwa Spika wa Bunge hili kwa kumwalika Rais wa nchi jirani, Mhe. Suluhu Hassan, kuja kuhutubia Bunge la Taifa na Bunge la Seneti kwenye kikao cha pamoja. Bi. Naibu Spika wa Muda, nina furaha isiyo na kifani ninapozungumzia Rais Suluhu Hassan. Mhe. Suluhu ameangaza mwanga mkubwa sana katika…
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Mbunge wa Narok, tuko na Hoja ya nidhamu kutoka kwa Mhe. Mohamed Abdikhaim. Na iwe ni hoja inayozingatia Kanuni za Kudumu za Bunge.
Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii. Kuna ndugu yangu hapa nyuma ambaye ananyeshewa. Jumba hili linavuja kutoka juu. Asante.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Ninapoketi kama Naibu Spika wa Muda, siwezi nikathibitisha hilo lakini tutaweza kuthibitishiwa na ofisi ifaayo.
Endelea, Mhe. Soipan.
Mhe. Bi. Naibu Spika wa Muda, utaniongezea muda wangu kwa sababu amenikatiza kwa njia isiyo halali. Tunahitaji kuthibitisha kama kweli ni maji ama ni kitu kingine. Nilikuwa nasema kwamba niko na furaha sana kama mama kiongozi; mama ambaye ako na watoto wa kike, ambao ndio viongozi wa kesho. Hatua ambayo wamechukua Watanzania, ingawaje uongozi wa Rais Suluhu ulikuja kwa njia ya kipekee ambayo ni ya kusikitisha, akiwa mama kiongozi ambaye anaona mwanga mpya ambao unaangazia uongozi wa kina mama, nina furaha sana. Unaposoma vichwa vya habari kuhusu uhusiano mwema Afrika Mashariki kwenye mambo ya uwekezaji, maendeleo na biashara, tangu Rais Suluhu kushika usukani, umekuwa ni muda mfupi sana lakini tayari tumeshaanza kuona anga mpya na mwamko mpya katika uhusiano mwema kati ya Kenya na Tanzania. Uhusiano huu pengine utafungua nafasi nyingi za kuweza kuendeleza uwekezaji na ujirani mwema. Haya ni maneno ambayo yataleta mambo mazuri na yanapitia katika uongozi wa mama. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
Uongozi wa Rais Suluhu Hassan unatuonyesha kwamba wakati wa akina mama umefika. Kwa lugha ya Kimombo, tunasema “ We should rise to the occasion. We should wake up andsmell the coffee ” kwa sababu wakati wa kina mama umefika. Nikiangazia nyanja mbali mbali, leo asubuhi tuliweza kumkagua aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Kenya. Hili ni jambo ambalo halijasikika kihistoria katika nchi hii yetu. Hata katika nyadhifa nyingine nyingi, tunaona nafasi ya kina mama inazidi kupanuka na kuongezeka. Rais Suluhu alizuru nchini Kenya ikiwa ziara yake rasmi ya kwanza tangu achukue hatamu za uongozi nchini Tanzania. Hiyo ni heshima kubwa sana kwa Kenya, na shukrani kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta kwa kumpa fursa hiyo. Hii ni njia moja ya kuonyesha kwamba Kenya tunatambua uongozi wa kina mama na tunajua wanaweza. Na wale ambao wanaendeleza mijadala na fikira za kusema kwamba kina mama hawawezi, nafikiri wanaendelea kuota ndoto ya mchana. Nawasihi Wakenya wote, Wanaafrika Mashariki, Wanaafrika na dunia nzima; tuwape kina mama uhuru wa kuweza kuingia katika nyanja zote za uongozi kwa sababu wanaweza, na tutakuwa na matumaini. Hata watoto tunaolea watajua kwamba ndoto zao ni halali bila kujali kama yeye ni msichana au mvulana. Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda.
(Mhe. (Ms.) Jessica Mbalu): Asante. Nilisubiri useme kuwa hata Spika wa Kikao cha Jioni ni mama.
Mbunge wa Nyando, Mhe. Okelo Odoyo.
Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwanza kabisa, wacha nikushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuongeza sauti yangu katika Hoja hii ya mjadala huhusu hotuba ya Mhe. Suluhu ambaye ni Rais wa Tanzania aliyoitoa hapa Bungeni kwetu. Kuja kwa Mhe. Suluhu katika Jengo hili, ni kuonyesha heshima kubwa sana kwa Wabunge wa Taifa la Kenya. Tunamshukuru kwa kupata nafasi ya kuja kwetu kututembelea na kuzungumza maneno ambayo yana uzito katika uboreshaji wa maswala ya uchumi, elimu, mambo ya barabara na mengineyo. Sisi kama Wakenya ambao Mwenyezi Mungu ametupa nafasi kuwa hapa Bungeni, tunasema asante sana. Tuligundua kwamba Mhe. Suluhu ndiye Rais wa pili kuzungumza katika Jengo hili baada ya Rais wao wa awali, Mhe. Jakaya Kikwete, pia kupata nafasi mwafaka kama hiyo na kuzungumza nasi hapa nchini Kenya. Nchi zetu zimepakana na ni dhihirisho ya kufanana kwa utamaduni wetu kama ndugu na dada. Alizungumza maneno mengi sana juu ya undugu wetu. Tusionyeshe undugu huo tu kwa mambo ya Kenya na Tanzania lakini kwa bara la Afrika nzima na hata ikiwezekana, tuionyeshe katika dunia nzima. Akina mama wamekuwa na vita vikali sana dhidi ya kutopanda ngazi. Katika Karne hii ya 21, bado tunatatizwa na akina mama kutopanda nyadhifa za uongozi. Sasa tunasema kwamba Mhe. Suluhu kule Tanzania ametuonyesha kwamba akina mama wanaweza na kama Mungu atatujalia kwa huu wakati bado tunapumua hapa duniani, hata Kenya wakati fulani tupate mama atuongoze huku. Hii ni kwa sababu wameonyesha kwamba wanawake wanaweza. Juzi kule Ujerumani, tuliona wakati aliyekuwa Chancellor wao, Angela Merkel, alipomaliza kutoa hotuba yake ya kustaafu, kila mmoja alisimama na kumpigia makofi kwa dakika sita kwa kazi nzuri ambayo aliwafanyia. Hapa Kenya pia tuwape wanawake nafasi kutuongoza na tuwapigie makofi vile tuliona kule Ujerumani. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
Tukiwa hapa Bungeni na Mhe. Suluhu, tulichekeshwa. Kulikuwa na mbwembwe na nderemo alipotaja kwamba wanyama wa pori kule Tanzania huwa wanakuja Kenya kutiwa mimba na kurudi kule Tanzania kuzaa. Sasa kazi ya wanyama wetu hapa nyumbani ni rahisi aje? Kazi yao ni kutia tu mimba wanyama wa kike kutoka kule Tanzania na kurudi kuzaa. Sasa hiyo mzigo tunapeleka Tanzania. Tulikuwa na vichekesho sana hapa wakati Mhe. Suluhu alitutembelea. Tumekuwa na changamoto kadhaa katika uwekezaji wa mali na jinsi ya kufanya biashara hapa na kule Tanzania. Kila mtu anatambua kuwa cheti au kibali cha kufanya kazi kule Tanzania kimekuwa kizungumkuti na alisema kwamba atafanya chochote anachoweza kuondoa kizingiti chochote ili tukae kama ndugu. Pia kama kibali kinatakikana na Mkenya kufanya kazi Tanzania, anafaa kupewa na vilevile Watanzania pia wakitaka kibali kufanya kazi Kenya, wapewe kwa sababu sisi ni majirani, ndugu na jamii moja. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi. Naona light yangu is
Hon
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo imefana sana. Ninaanza kwa kumpa pongezi zangu mimi binafsi na ya akina mama wa Kenya kwa Mama Suluhu Samia kwa kupata nafasi ya kuongoza kama Rais wa kwanza mwanamke katika Afrika Mashariki na pia kuwakumbuka wahusika ambao walikubali kumpa nafasi ili kuwaongoza na kumwamini. Si rahisi kwamba Mhe. Suluhu angepewa nafasi na ninashuku kwamba wale wote waliohusika walikuwa wanaume. Kwa hivyo, hongera sana kwa Serikali ya Tanzania kwa kukubali Mhe. Suluhu awaongoze. Pia tunapongeza Serikali yetu ya Kenya kwa kukubali kumkaribisha Mhe. Suluhu hapa nchini alipozuru. Alipewa heshima na nafasi ya kutosha ndiposa akaja hapa Bungeni kuhutubia Bunge zote mbili na tukamsikiliza kwa hekima aliyonayo, umri ambao anao na kwa kazi ambazo amefanya. Siku nyingi anaonekana kwamba anaweza na anaelewa kazi yake. Mimi binafsi, nilimwona yule Rais kama mama ambaye anataka kuleta uhusiano ulio bora kati ya nchi hizi mbili na hata Afrika Mashariki kwa jumla. Najua kwamba imekuwa si rahisi sisi kama Afrika Mashariki kuongea pamoja na kufanya biashara pamoja. Mara nyingi nimesikia wafanyabiashara humu nchini wakilalamika kwamba wakifanya biashara humo Tanzania, wale wanafaidika kuliko sisi Wakenya. Sasa natumai kwamba wakati huu wa Mhe. Suluhu ambaye ataleta suluhu, ataweza kufanya Wakenya kufurahia biashara humo nchini Tanzania. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
Kuna mambo mengi ambayo tumeona Mhe. Suluhu akiyafikiria, akiyapanga na tunaona kwamba tukimshika mkono, kuna mabadiliko yataonekana. Tunajua kwamba mimea ambayo inapandwa hapa nchini mara nyingi tunabadilishana katika biashara ya Kenya na Tanzania. Hata hivyo, wafanyabiashara wetu huwa wanalalamika kidogo kwa sababu wakati wanapanda mimea yao, wataona wale wameleta nyingi lakini wao hawawezi kupeleka yao kule. Hii inaleta kukosana kidogo. Lakini naona Mhe. Suluhu anafanya bidii na tunashukuru sana. Tunaomba pia katika hiyo hali, sisi akina mama kwa sababu tumepata bahati kupata Rais mwanamke kwa Afrika Mashariki, tusitumie hiyo nafasi vibaya, kujigamba wala kuonyesha dharau lakini tunapaswa kupeana heshima na kushika mkono Mhe. Suluhu atekeleze kazi yake ili kuonyesha kwamba akina mama pia wanaweza. Tunamwambia kwamba anapokaa pale, anawakilisha akina mama wengi sana hapa Afrika Mashariki na hata dunia nzima. Kwa hivyo, anapofanya kazi yake, anapaswa kujua kwamba sisi sote na dunia nzima tunamtazama ili tuweze kukubali uongozi wa akina mama. Katika ile hali, hata hapa Kenya Rais wetu ameona ni vyema kumpa nafasi mama mmoja kuwa Jaji Mkuu humu nchini. Ninaona amezungumuziwa na ni kana kwamba amekubalika. Naomba tu uapishaji wake ufanywe kwa upesi kidogo ili katika ule moyo wa kupata akina mama uongozini, pia tupate Jaji Mkuu hapa nchini ili pia yeye aweze kuwakilisha akina mama katika mahakama zetu kama vile Mama Suluhu anafanya kule Tanzania. Mhe. Suluhu alipoongea kuna msemo ambao alisema, sijui kama sisi sote tulisikiliza. Alisema kuwa deni ya wema ni wema. Kwa hivyo, wakitutenda mema sisi pia tutende mema kwao. Kwa hivyo, ninaunga mkono Hoja hii. Bi. Suluhu, Mungu akusaidie uweze kutekeleza kazi na kuonesha kuwa akina mama wanaweza. Asante sana Bi. Spika.
(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Shukrani. Mbunge wa Fafi, Mhe. Mohamed Osman.
Asante Naibu Spika wa Muda. Nimefurahi umenipa hii nafasi nichangie mjadala huu kuhusu hotuba ya Rais jirani, Suluhu, alipofanya ziara yake ya kwanza hapa Kenya. Katika dini yetu ya Kiislamu, Mtume, ṣallā -llāhu ʿalayhī wa-sallam, ametuambia kitambo sana kuwa mtu akitaka kwenda peponi, basi iko katikati ya miguu ya mama. Alisema hilo mara tatu. Kwa hivyo, sisi kama Waislamu tumekubali akina mama kuwa viongozi kama alivyo Mama Suluhu. Pia kuna suala la jinsia. Sisi Wabunge wa Taifa la Kenya, hayo masuala ya jinsia yalipofika humu Bungeni hatukufanikiwa kuyapitisha. Ningeomba akina mama wakubali kujipigia kura. Vile najua, tuko na akina mama shujaa kama vile Martha Karua ambaye alikuwa katika hili Bunge kwa muda wa miaka ishirini. Alijaribu kugombea kiti cha urais wa hii nchi. Tulikuwa na mama mwingine kutoka Kitui, anaitwa Ngilu. Alikuwa waziri. Kwa hivyo, kama Wakenya tunataka kukubali akina mama kuongoza, lazima tupate huo uongozi kutoka kwa akina mama wenyewe—wakubali kupigia wenzao kura. Kwa nini nimesema hivi? Sitini kwa mia ya wapigajikura hapa Kenya ni akina mama. Kama akina mama watakubali kupigia mama mwenzao kura tutapata Rais wa kike humu nchini. Suala la pili ningependa kuchangia ni kuhusu ufisadi. Mimi nimefanikiwa na Mungu kuwa na wasichana wanne. Niko na watoto saba. Nasema alhamdulillah . Wanne ni wasichana. Bado ninatafuta mke wa pili, wa tatu na wa nne. Dini yangu inakubali hilo. Kuhusu mambo ya ufisadi niliyotaka kuchangia, kama tunataka kupigana na ufisadi hapa Kenya ama tunataka The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
kumaliza ufisadi hapa Kenya, ningeomba Rais wetu, Uhuru Muigai Kenyatta, apatie akina mama kazi kwa kiwango cha sitini kwa mia. Ni kwa sababu akina mama ni watu ambao wako na utu, wanajali masilahi, hawataki vita, na si watu wa kuiba ama kupora nchi. Kama tunataka kupigana na ufisadi, lazima tutambue akina mama katika kuongoza kazi humu nchini. Kuhusu biashara, sisi kama Wakenya lazima tuwe na amani kwanza, vile Rais Uhuru Muigai Kenyatta alitafuta ndugu yake aitwaye Baba na wakafanya Handshake . Walikumbatiana kuleta amani nchini. Lazima pia tuchunge jirani wetu. Tuko na jirani wengi sana. Wa kwanza ni Tanzania. Juzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuja hapa, Watanzania walilalamika sana. Walisema kila wanapojaribu kufanya kazi ama kuanzisha biashara hapa Kenya inakuwa vigumu kwao kupata cheti ama leseni ya kuanzisha kazi. Sisi Wakenya, katika
yaani Afrika Mashariki kwa Kiswahili, ndio tunaongoza katika economy ama uchumi. Lazima tuwe mfano bora. Sharti tuwaoneshe mfano bora jirani wetu kama Uganda na Tanzania. Saa hii tuko na Rais Suluhu.
(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Asante sana. Nafasi sasa ni ya Mbunge wa Eneo-Bunge la Shinyalu, Mhe. Justus Kizito.
Asante. Naomba nitoe hii kwa sababu nitakuwa nikidurusu kidogo. Tafadhali.
(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Sasa, Waheshimiwa, tuchunge wenzetu. Tunakusikia hata ukiwa na mask.
Niko mbali, halafu nabanwa. Nashukuru Bi. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niseme machache tu kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Serikali hiyo, Bi. Suluhu Hassan. Kwanza kabisa ningependa kumshukuru Rais wetu wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa sababu ilitokana na ule uhusiano wake mzuri na watu wa Jumuiya hii. Nafikiri ndilo lilimfanya Bi. Suluhu kuona kwamba ni muhimu aje hapa ili atengeneze uhusiano. Kwa hilo ningependa kusema shukrani. Kwanza kabisa ningependa kumshukuru huyo Mhe. Rais wa Tanzania kwa kubadilisha mwenendo. Kama mnavyojua, mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kutoka mwanzo yalikuwa na mporomoko na mushkili—mipaparuzano, mikinzano mingi, ikitokana na mambo ya kutoelewana, taharuki, kuogopana namna hiyo na kusema kwamba Wakenya ndio wajuaji. Kwa hiyo ilikuwa ni mambo ambayo hayana msingi. Lakini Dkt. Bi. Suluhu ambaye ndiye Rais wa nchi hiyo amebadilisha na kuleta mwenendo ambao sasa ni sawa kuleta ukuruba, kuleta mahusiano mazuri kati yetu na wao ili tuweze kuweka msingi wa undugu ambao utatufaa zaidi katika siku nenda siku rudi, daima dawamu. Utadumu milele ili kusaidia watu wetu wafanye kazi pamoja kwa sababu ya soko kuu. Wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati wakifanya biashara pamoja, tutakuwa na soko kubwa la kazi, kuuza mazao yetu na kufanya mambo yetu mengi ambayo yatakuwa yanatufaa sisi haswa katika kuleta vitega- uchumi vitakavyofaa kwa watu wetu. Muhimu ni kwamba, ulipomuona Mama Suluhu akizungumza hapa, alizungumza Kiswahili kizuri sana. Kiswahili chenye uletelezi, sahili, burudani nyingi, bashasha, vijembe vimejaa mumo kwa ndani. Tuliona kwamba Kiswahili hicho kilikuwa kizuri sana kikatuchangamsha. Nimeona Kiswahili kimewatia Wabunge wa hapa motisha. Naona Wabunge wanazungumza Kiswahili kizuri. Nimemuona yule anayetoka kule Nyanza, nimemuona dada hapa wa kutoka kule akisema Kiswahili kizuri sana. Nawaambia kwamba lugha ya Kiswahili ni nzuri na itatufanya tuwe na mahusiano mazuri sana Tanzania. Ningependa, kwa vile mama yule The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
ametutia motisha na mshawasha wa kuwa na uchu na tamaa ya kuendeleza lugha hii katika Bunge hili, itatufaa sisi pia tupate siku moja au mbili katika zile kaida ama Kanuni zetu ili tuweze kuzungumza Kiswahili kwa lazima. Tunapofanya mazoezi pale-hapa, tutakuwa tunazungumza sawasawa. Nilipomuona Mama Mhe. Rais akisema kwamba Kiswahili chetu kinakuwa na vituko na vijembe vinavyowafanya wacheke na kufurahia kinapozunguzwa, nafikiri ni sawa. Nataka niwaambie Wakenya wajue kwamba taifa letu la Kenya, katika ustandadi wa Kiswahili, tunaposema waandishi ambao wamekomaa, wale gwiji wanaojua lugha ya Kiswahili undani, wale wakiritimba, ni walewale wanaotoka hapa. Ningependa kuwashangaza kuwa yule anayezungumza Kiswahili kizuri zaidi, yule gwiji au bingwa mkubwa anatoka Nyanza. Anaitwa James Ndeda, ama muite Wallah bin Wallah. Ndiye muandishi wa mno katika lugha ya Kiswahili. Namshukuru Bibiye Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano, na Rais wa Kenya. Nasema asante, shukrani, naunga mjadala huu mkono wa dhati. Asante.
(Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Kiswahili sanifu hata wewe. Sasa tumpate Mhe. wa Kabondo Kasipul, Mhe. Obara Akinyi.
Asante sana, Bi Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi niunge mkono hoja ya Mama Rais Suluhu wa taifa la Tanzania. Ni mama wa kwanza kuwa Rais kwa Afrika Mashariki. Nafurahi kwamba marais wengi sana wametembelea Kenya, lakini hatujaona yeyote akifika hapa Bungeni. Tunampatia pongezi kwa kuwa Rais wa kwanza kutembelea Bunge la 12 la Kenya. Mama alisema maneno mengi mazito. Wenzetu wameongea maneno ya utaalii. Alitambua kwamba Kenya ni jirani mwema. Na alitutambua kama wale ambao atafanya nao biashara na kuendesha maendeleo kama majirani. Sisi wote we will benefit from both sides . Tutafaidika from both sides .
Hon
Hon. Temporary Deputy Speaker, can we speak in English?
Hon
Asante. Nitaendelea na Kiswahili. Rais Mama Suluhu alituonyesha ya kwamba yeye ni mama anaye unyenyekevu.
Hon
Mama Rais Suluhu ni mama aliye na unyenyekevu na ni mwakishi kwa wamama wote ambao ni viongozi katika Afrika Mashariki na dunia nzima. Tunampa pongezi. Nimefurahia sana. Na tunaomba arudi tena. Mwisho, tunampatia Rais wetu mpendwa Uhuru Kenyatta hongera kwa kumpokea jirani Rais Bi Suluhu. Asante sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Asante sana, Mhe. Obara Akinyi. Umeweka bidii na kufanya vyema kwa kujadili Hoja hiyo. Mwakilishi wa Gatanga.
Asante sana, Bi Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia hii nafasi niseme machache. Mimi naona unafanana na Rais wa Tanzania aliyetutembelea hivi majuzi. Nakuombea mazuri hata wewe ukuwe Rais wa Kenya siku moja. Lingine ni kushukuru sana Rais wa Tanzania kwa kututembelea na kusema yale aliyosema katika Bunge letu. Kutembea kwake hapa Kenya kutawezesha kuimarisha biashara kati ya watu wa Kenya na watu wa Tanzania. Tunawajua Watanzania kama wafanyabiashara kama Wakenya wenzetu. Na wanajulikana sana. Vyakula vingi hapa Nairobi hutoka pale Tanzania, kama mahindi na kitungu. Kwa hivyo, hiyo italeta bei ya chakula chini. Nawaambia wakulima wetu wafanye bidii pia waweze kuuza vitu vingine pale Tanzania. Lingine, ningependa kushukuru Rais kwa sababu ameuimarisha uhusiano wetu. Hapo mbeleni tulikuwa na shida sana maana wale viongozi tulikuwa nao Watanzania waliona ni kama tuko na vita. Sisi Wakenya ni watu wa amani. Chenye tunataka ni kufanya biashara pamoja maana Watanzania ni ndugu zetu na tunawapenda sana. Uhusiano usiwe tu na Watanzania peke yake. Tushikane pia na majirani wengine kama Uganda. Nashukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya kwani jana nilimuona Uganda katika sherehe ya kutawaza Rais Yoweri Museveni. Naomba Rais azidi kutembea ndio tuweze kufanya biashara pamoja. Inajulikana wazi kuwa ile biashara Wakenya wanafanya zaidi ni hapa sehemu zetu za Afrika Mashariki. Kama tungeruhusiwa tufanye biashara pamoja, haingekuwa haja ya kuenda mbali. Wananchi wa hili jimbo wako na uwezo wa kusaidiana na kuendeleza nchi zetu mbele. Si lazima wakati wote tunategemea watu wa ng’ambo. Nauliza Waafrika wajiheshimu na tuwe na mashirika yanayoweza kutusaidia. Kwa vile naona kuna wenzangu wanataka kuongea, niseme Kiswahili changu kimefika hapo. Nafikiri hata mimi nimepita Kiswahili. Asante.
Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Asante. Umejaribu. Mwakilishi wa Kilome, Mhe. Nzambia Kithua.
Asante sana, Bi Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa hii fursa kuchangia huu mjadala muhimu. Kwanza nataka kushukuru Wabunge wote waliompokea Mhe. Rais Suluhu kwa shangwe na vigelegele. Hiyo ilimpa motisha sana ya kutupatia habari kamili kuhusu nchi zetu mbili. Nataka kushukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kuchukua nafasi ya haraka sana kumkaribisha mwenzaki jirani Rais Suluhu. Kwa muda tumekuwa na shida nyingi sana. Na hicho ni kitu cha kusema bila uwoga wala kuficha. Wanabiashara wa Kenya wamekuwa na shida ya kufanya biashara Tanzania. Kuwemo kwa Rais wa Tanzania hapa kwetu kulitupatia nafasi safi ili biashara iendelee na amani. Ushirikiano na umoja unaimarisha maendeleo katika nchi yoyote. Ule undugu Suluhu mwenyewe alituonyesha ilibainika wazi kwamba tukiendelea hivyo katika nchi hizi mbili, itakuwa ni kwa manufaa yetu sisi wote. Kuna kitu muhimu katika nchi jirani. Wakati kuna umoja, biashara na maendeleo huimirika haraka sana. Pia ningependa kushukuru Rais wetu Uhuru Kenyatta kwa kuchukua nafasi kumualika Rais Suluhu, kwa sababu moja: zile shida zimekuwa katika mipaka ya nchi zetu mbili, ilibainika wazi kwamba kumekuwa na uhuru wa kufanya biashara na kuimarisha maisha ya Wakenya na Watanzania. Pia, nachukua nafasi hii kushukuru ukarimu wa Rais Suluhu kwa kuitikia wito wa kututembelea. Kama walivyosema wenzangu, ilikuwa nafasi nzuri kwa viongozi wetu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
wawakilishi wa wanawake. Imeweza kuwapa nguvu na motisha kujua kwamba kuna uwezekano wa wao pia kuwa marais ama viongozi wakuu kwenye taifa hili siku moja. Ninachojua ni kwamba uongozi wowote unaoshikiliwa na wanawake huimarisha hali ya nchi zaidi ukilinganisha na uongozi wa wanaume. Ninawashukuru Waheshimiwa wote kutoka Bunge la Taifa la Kenya na Bunge la Seneti kwa kumkaribisha Mhe. Suluhu na kwa kumwalika aje tena ili aendeleze mipango ya kung’arisha nchi zote mbili. Shukrani, Naibu Spika wa Muda.
Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Shukrani Mhe. wa Kilome. Nafasi iliyopo sasa ni ya Mbunge wa Isiolo Kaskazini, Mhe. Hulufo Oda. Ninaomba uchukue usukani. Waheshimiwa, sio lazima tena kufuata Kanuni za Kudumu. Pia, sio lazima mtumie wakati wenu wote maana tuko na Waheshimiwa wengine kwenye foleni.
Ahsante sana Naibu Spika wa Muda kwa hii nafasi. Ninaunga mkono hii Hoja ya Hotuba iliyotolewa katika Bunge hili na Rais Samia Suluhu wa Muungano wa Tanzania. Ujio wa Mhe. Rais Suluhu Hassan, kwa hakika, ulikuwa safari yake rasmi ya kwanza tangu alipochukua usukani wa wa nchi hiyo, na hiyo ni heshima kubwa kwa nchi yetu. Namshukuru Rais wetu pia. Rais Suluhu alituambia kwamba Mhe. Uhuru Kenyatta alikuwa kiongozi wa kwanza kuwafariji Watanzania alipopata habari ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli. Rais Suluhu pia alitueleza jinsi Rais Uhuru Kenyatta alivyokatiza hotuba yake kwa muda kwa heshima ya adhana ya kuwaita Waislamu kwenda msikitini kusuali alipokuwa akiwafariji Watanzania kule Dodoma. Hilo ni jambo lililowafanya Watanzania kumuona Rais wetu kama kiongozi anayethamini na kuiheshimu dini ya Kiislamu. Rais Suluhu ametuonyesha kuwa viongozi kina mama wako na hekima. Alikaa kwa kikao na Rais wetu na wengine wanaoendeleza Serikali yetu. Hiyo, ilimuwezesha kuelewa dhana tulizonazo kuhusu Tanzania; kama ile dhana ya kwamba Watanzia wanachukia Wakenya, na kadhalika. Rais Suluhu pia aligusia masuala yanayounganisha hizi nchi mbili jirani, na ni mengi kuliko yale ambayo hatukubaliani nayo. Kuhusu yale mambo machache ambayo hatukubaliani nayo, Rais Suluhu alisema kwamba hayaambatani na msingi wowote isipokuwa kile alichokiita
, yaani fikira potovu. Kwa sababu ya muda, ningependa tu kumshukuru Rais Suluhu. Tunaomba tuwe na uhusiano mwema kama mataifa jirani.
Hon
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninakushukuru kwa kunipatia hii fursa ili nichangie Hoja hii kuhusu Hotuba ya Rais wa Muungano Tanzania. Ninatangulia kwa kumshukuru Rais wetu kwa kumpa mwaliko Mama Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani. Pia, nampongeza Mama Suluhu kwa kukubali mwaliko huo na kuifanya Kenya nchi yake ya kwanza kuzuru rasmi akiwa kama Rais. Leo hii, tunamshukuru. Hotuba ya Mama Rais Suluhu ilikuwa ya kufana sana. Nilivutiwa na hekima yake. Pia nilipendezwa na umakini wake kila alipokuwa akijieleza. Nilifurahishwa na jinsi alivyotilia mkazo jambo la umoja na undugu wetu, haswa aliposema kuwa hili ni jambo ambalo limekuwa tangu mwanzo akieleza kwamba tangu jadi, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
Watanzania na Wakenya waliishi kama ndugu. Nilifurahi kuona kwamba anataka kufufua uhusiano wetu wa tangu mwanzoni. Ndugu ni kufaana sio kufanana. Nchi za Kenya na Tanzania, na haswa Gatuzi la Taita Taveta, Eneo Bunge la Taveta, ni jirani wa Tanzania na tumekuwa tukifaana na ndugu zetu wa Tanzania kwa mambo mengi sana...
Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Mhe. Wa Ruiru, Kingara. Tafadhali, chukua usukani.
Asante Sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie mema na mazuri ambayo yanatuleta sote katika eneo la Afrika Mashariki. Mwaliko wa Rais wa Tanzania Bi. Samia Suluhu ulifanywa na kiongozi mwenye hekima, Rais Uhuru Muigai Kenyatta. Ninawapongeza wote wawili kwa kutumia njia hiyo kama nafasi ya kuleta uwiano katika maendeleo ya Afrika Mashariki. Kuna Nchi sita zinazoshirikiana katika Afrika Mashariki. Tukianza na Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuliko nyingine kwa ukubwa wa ardhi, ninaona maisha yakiwa mazuri. Alinivutia pia wakati marais wote wawili walipoangazia vile tutafungua mipaka yetu. Mipaka kati ya Kenya na Tanzani ni mingi. Mifano ni Namanga, Lunga Lunga, Isebania na Sirare. Wafanyabiashara wetu wamekuwa na shida sana katika shughuli zao za biashara pale katia mipaka. Viongozi hao walipokutana walijaribu kulainisha vile biashara inaweza kunoga kati ya nchi hizi mbili, na kuonyesha maendeleo yatapatikana. Pia, waliongea kuhusu usalama. Hapa kwetu, tumekuwa na shida ya usalama hapa na pale. Nchi zote mbili zikiungana, na haswa zikileta nchi nyingine kwenye muungano huu, hali ya usalama itakuwa nzuri. Akigusia masuala ya utalii katika nchi zote mbili, Rais Suluhu alisema kwamba kulikuwa na changamoto kwa vile Wakenya na Watanzania hawakuwa wakifanya biashara bila ya matatizo katika maeneo ya hifadhi za wanyamapori za Serengeti upande wa Tanzania na Maasai Mara upande wa Kenya…
Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia hotuba ya Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu. Kwanza kabisa ni kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya na Rais wa Tanzania kwa kushikana na kuonelea ni vizuri wakutane na wafanye kazi pamoja. Mwaka uliopita nilitamka matamshi ambayo yalileta shida sana katika nchi hii na nchi jirani. Na mimi kama Mbunge wa Starehe nilikuwa natetea wale wakaaji wa Starehe ambao wengi ni wafanyabiashara. Kumekuwa na changamoto nyingi sana na mimi nilifurahia sana wakati Mhe. Suluhu, Rais wa Tanzania, alipozuru nchi yetu kwa sababu ilionyesha kwa kweli kulikuwa na matatizo ambayo nilikuwa nimeyaongea. Na mimi nataka niseme ni kitu cha maana sana sisi kufanya kazi pamoja na Tanzania. Tumekuwa na tulikuwa na shida nyingi sana kama vile Waheshimiwa wengine wamesema, kwa maneno ya kilimo na maneno ya wafanyabiashara. Ulikuwa unapata mfanyabiashara akitoka hapa akienda nchi Jirani, kuna mahali hangeweza kufanyia biashara; kuna mahali angewezaenda na asiingie. Wengine wananunua mizigo wakiwa juu ya miti lakini wale Watanzania wakija Kenya unapata wanafanya biashara bila kusumbuliwa. Kwa hivyo, nikimalizia kwa sababu sitaki kupoteza muda sana, nataka niwaeleze wale waliopatiwa majukumu na marais hao wawili kulainisha biashara za hizi nchi mbili, wakae chini, sio na matajiri pekee, wakae chini na hata wakulima wadogo wanaoteseka wakati nchi hizo mbili zinazozana. Asante sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Asante. Kabla sijamwita mtu wa kuhitimisha hoja, wacha nimpe dakika moja Mbunge wa Kirinyaga Central nikitumia Kanuni za Kudumu Namba 1.
Asante sana, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii pia nami nichangie huu mjadala. Kwanza kabisa, nigependa kumpongeza Rais wetu mpendwa kwa kumwalika Rais Suluhu Hassan na yeye pia kukubali kuja hapa na kuhudhuria kikao cha Bunge zote mbili. Pia ningetaka kuwashukuru maspika wetu wote wawili kwa hiyo hatua walichukua kutuita sisi sote tuje kuhudhuria hotuba ya Rais wa Tanzania. Katika hotuba yake sana sana alilenga uhusiano mzuri ama mwema kati ya Tanzania na Kenya. Vile vile, alisema kuwa unaeza kuchagua marafiki lakini huwezi kuchagua jirani...
Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Asante. Tumesema dakika moja. Mheshimiwa Moi.
Asante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii nichangie hotuba ya Rais wa Tanzania. Wakati niliposikia hotuba yake ilikuwa ya kuwawezesha Watanzania waingie Kenya kwa wingi jinsi Wakenya wameingia Tanzania na kupeleka biashara huko. Aliseme kwamba ile pesa wanabiashara wamepeleka Tanzania ni nyingi sana kushinda ile Watanzania wameleta Kenya. Kwa hivyo, alikuja kuongea na Rais wetu wa Kenya kusaidia Watazania pia hao waweze kuweka pesa zao hapa Kenya. Pia, aliongea kuhusu barabara na umeme ambayo ni miradi Tanzania na Kenya wanafanya pamoja. Alifurahia kwamba...
Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Mheshimiwa Hassan, Kwale County, Hassan Juma.
Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alisema kwamba uongozi ni kuoyesha njia na sio kufunga njia. Nafikiri ni somo kubwa sote viongozi. Pili, sasa nimekuwa na moyo kuwa shida za biashara kubwa na ndogo ndogo kama za boda boda katika mpaka wetu wa Horo Horo ulioko Kaunti ya Kwale zitaisha. Alisema tushikane na tuungane naye ili tuweze kupitisha yale maswala aliyotuambia ya kusaidia nchi zetu mbili katika biashara na utalii. Asante sana.
Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Mhe. wa Kinangop.
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii. Kwanza ningetaka kumshukuru Rais wetu kwa kumwalika Rais Suluhu Hassan kuwa pamoja nasi. Tanzania wamebarikiwa sana kwa sababu wana Suluhu, Mpango na Majaliwa. Hawa wote ni viongozi katika serikali yao. Jambo la pili na la mwisho ni kwamba Rais Suluhu amejionyesha kuwa mwanadiplomasia ambaye Jumuiya ya Afrika Mashariki inahitaji sana. Nasema pongezi na aendelee zaidi.
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Mhe. wa Runyenjes
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mhe. Rais wa Tanzania Bi Suluhu aliongea na nikamsikia kama kiongozi anayeongea kwa upole, ukarimu na si wa kuamrisha. Niliona nchi ya Kenya na Tanzania zitafaidika pakubwa kupitia uongozi wake na wa Rais Uhuru Kenyatta. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Hon. (Ms.) Jessica Mbalu): Wa mwisho, Mhe. wa Nyeri County.
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii niweze kuchangia Hotuba hii ya Rais Suluhu. Kwanza ni kumshukuru Mungu kwa Rais Suluhu kututembelea hapa Kenya kama nchi jirani. Ni Rais aliyenyenyekea sana, anapenda amani na alitutembelea ndiyo tuwe na uhusiano mzuri kati yetu na Tanzania. Pia aliweza kutuambia biashara inaendelea vizuri sana na miradi ya ujenzi wa barabara kutoka Lamu, Mombasa na Tanga yenye urefu wa kilomita 454 unaendelea vizuri. Tutaendelea kumuombea na pongezi sana kwa Rais Suluhu, Mungu amulinde na amuongoze...
Hon
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Pia mimi nataka kuchangia Hoja hii. Namshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kujenga uhusiano mwema na Rais Suluhu Hassan wa Tanzania. Yale mambo nimeona Rais wetu akifanya yanatutia nguvu kila wakati kwa sababu analeta uhusiano ambao utasaidia Wakenya.
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Hon
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hotuba ya Rais Suluhu Hassan. Yangu ni maswala ambayo yalijitokeza sana kama mambo ya biashara na utalii. Tukiangalia uhusiano wetu wa kibiashara na utalii haujaweza kuwa mzuri sana. Watalii kutoka Tanzania wanaweza kuja Kenya na Wakenya hawawezi kwenda kule Tanzania.
Hon
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka kusema kwanza tunashukuru kwa sababu mwanamke amechukua urais katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Napongeza Serikali yetu kwa kumkaribisha Rais Samia Suluhu Hassan hapa Kenya. Tunatarajia kwamba Rais wetu akipanga mambo ya 2022 atajaribu sana kuweka wanawake huko juu kwa sababu ameona kama Afrika Mashariki inaweza kuwa na Rais mama basi Kenya pia inaweza kuwa na mama...
Hon
Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba kuwashukuru Wabunge wenzangu wote waliochangia Hoja hii na kwa maneno yote mazuri wamezungumza kuhusu Rais Samia Suluhu Hassan, safari yake na hotuba aliyotoa katika Bunge hili. Ninashukuru kwa vile alivyojitolea kuboresha uhusiano baina ya nchi zetu mbili na kama nilivyosema ni kupapalia magugu yote ambayo yamekua na kuanza ukurasa mpya katika uwiano wa nchi zetu mbili na hasa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa jumla. Pia, ikiwa hiki ni kikao cha mwisho kabla ya kwenda kwenye likizo fupi, ningetaka kuwatakia Wabunge wote likizo yenye mafanikio na Mungu awalinde wote. Tuonane tena panapo majaliwa na kila mtu akumbuke kujikinga kutokana na janga la corona ambalo liko hapa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
na liko na sisi. Tukiweza kurudi hapa tutamshukuru Mungu kwamba tumeenda kutenda yale tunayotenda kwa wananchi tunaowahudumia na tumerudi hapa kuendelea na huduma tunazotoa katika Bunge tukiwa Wabunge ambao wameteuliwa kuwahudumia wananchi.
Kwa hayo machache, naomba kuhitimisha.
Hon
Hon