All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 97.

  • 12 Apr 2016 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ambayo nilikuwa nimeingojea kwa hamu na gamu mchana wa leo. Nilikuwa likizoni lakini nilijua kwamba badala ya kupiga filimbi nitapata fursa ya kuongea na kusikika kwa njia inayokubalika. Nampa hongera Rais wa Jamhuri yetu ya Kenya kwa sababu alionyesha umahiri wake. Sio jambo rahisi wakati unataka kuongea na watu wengine wanataka kukufanya uonekane ni kama huna maana. Ule ulikuwa mtiani mkubwa na kwa hivyo nampa Rais hongera sana. Kulikuwa na wageni kutoka nchi mbalimbali na watoto wa shule katika Bunge letu. Wakenya wengi walikuwa wanaangalia kilichokuwa kinaendelea. Kilichotendeka halikuwa jambo rahisi; ... view
  • 12 Apr 2016 in Senate: Bw. Spika wa Muda, Waswahili husema: “Mpapia au mkamia maji hayanywi au hafaidiki nayo.” Pengine kama Sen. Muthama angenisikiliza kwa makini angeelewa nilichosema. Mimi ninataka watu hao wapewe haki ili waweze kujikimu kimaisha ili wasahau yale yaliyowapata. Naomba Serikali yetu iwasaidie ili waweze kununua mashamba na kuwa na makao mapya. view
  • 12 Apr 2016 in Senate: Bw. Spika wa Muda, nimerekebisha kwa kusema ni waathiriwa wa kindani. Nafikiri pia yeye hakunipata vyema. Ulimi ni kawaida kuteleza. view
  • 12 Apr 2016 in Senate: Bw. Spika wa Muda, Sen. Muthama amenirudisha nyuma. Hata hivyo, ni ombi langu kama Mkenya na mama kwamba waathiriwa wapewe haki. Shida tuliyonayo sasa ni moja si kama hapo awali wakati shida zilikuwa nyingi. Mhe. Naibu wa Rais sasa ametulia. Ninahakika kwamba mambo mazuri yanakuja kwa sababu tunataka sote tuishi pamoja kama Wakenya wa kabila na dini moja ndiposa kila mmoja wetu ajihisi huru katika nchi yetu. Ni ombi langu kuwa wote walioathiriwa katika ghasia za uchaguzi waridhiwe ili nao wajisikie ni Wakenya. Tumekuwa tukiomba na maombi tunayoandaa, ningependa tuwaombee kila mmoja wetu kwani shida tuliyonayo sasa ni ya uwiano ... view
  • 2 Dec 2015 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda kwa nafasi hii. Kama unavyojua, mwamba ngoma huvutia kwake. Naomba pia kukaribisha wageni wa Kaunti ya Kilifi ambao wamekuja hapa kujionea na kusoma zaidi ili wanaporudi nyumbani wawe wata tenda ipasavyo. view
  • 12 Nov 2015 in Senate: Bw. Spika wa Muda, natoa shukrani kwa Mwenyekiti wetu, Sen. Ongoro. Pia nawashukuru wale wageni ambao walikuwa wamekuja. Kama unavyojua, hadhari kidole na jicho(?). Sen. Ongoro anataka kilichotuuma jana, leo kisitutambae. Wimbo mbaya hauimbiwi mwana. Mwana ni nani? Mwana ni sisi akina mama. Kutoka tunapozaliwa, mama zetu tayari huwa wametutenga. Mtoto wa kike atatumwa jikoni na yule wa kiume atatumwa mambo ya nje ama aende acheze na wenzake. Kutoka tunapozaliwa ama hata kabla hatujazaliwa, kuna jamii ambazo mtoto The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained ... view
  • 12 Nov 2015 in Senate: Bw. Spika wa Muda, sijataja dini yoyote. Nimetaja mila, kwa hivyo huwezi kujua mimi niko kwa mila gani. Tukitoka hapa nitakueleza. Nilikuwa ninazungumzia itikadi zetu. Mimi kama mwenyeji siruhusiwi kuonekana wala kutoa sauti. Ni unyanyasaji ulioje? Itakuwaje mimi nitafanya kampeni bila kutoa sauti? Huo ndio uonevu ambao Seneta yuaona raha kwa sababu anasema hiyo ni mila yetu. Nasema katika mila yangu, siruhusiwi kuongea mbele ya wanaume au kukaa hadi usiku sana. Sijataja dini ya mtu. Bw. Spika wa Muda, usalama wetu kama akina mama pia ni changamoto. Sijui tukienda kampeni tutavaa nguo gani ili hata sisi tujisitiri. Ile nguo uliyovaa ... view
  • 10 Nov 2015 in Senate: Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kama vile umesema, umenipendelea, nashukuru sana. Nampa pongezi Sen. Musila kwa sababu Mswada huu umebobea kama yeye. Kuna sababu ambazo zinafanya stakabadhi hizi zizuiliwe shuleni. Kuna sababu mpya ambayo imejitokeza. Kuna haya masomo ya ziada ambayo ukienda shuleni kuchukua stakabadhi, utaambiwa hakulipa pesa za remedial . Pia, kuna stakabadhi zingine ambazo zinazuiliwa kwa sababu ya ukosefu wa nidhamu kwa mtoto. Kama mtoto hana nidhamu, na hata kama umelipa karo, utaambiwa zimezuiliwa kwa sababu ya nidhamu. Lazima tuangalie vile tutafanya ama tutawajibika vipi ile watoto wawe na nidhamu. Mwanafunzi ataogopa kwamba stakabadhi ... view
  • 5 Nov 2015 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Pia mimi najifunga kibwebwe niunge mkono mjadala huu. Shukrani zangu za dhati kwa Sen. (Prof.) Anyang'-Nyong'o kwa sababu hii ni Hoja ambayo ni ya maana sana. Nataka pia kumpongeza ndugu yangu, Sen. Harold Kipchumba, kwa kupasua mbarika hii. Bw. Spika wa Muda, aibu ya maiti aijuaye ni mwosha. Adhabu ya kaburi aijuaye ni maiti. Agunduaye ndwele ndiyo mganga. Sen. Harold amefanya jambo la maana sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 29 Oct 2015 in Senate: Asante sana, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii, ili nami niunge mkono Hoja hii ya Sen. Kittony. Hoja hii imebobea kama mamangu, Zippora kwa sababu ni Hoja ya maana sana ambayo imechukua muda mrefu, na tujuavyo wakati ni mali. Lakini sisi hatuoni kama wakati ni mali kwa sababu muda mwingi sana tunaharibu brarabarani, muda mwingi sana hatujui tutafika salama ama vipi kwa sababu ukiangalia ule msongamano, haujui nani atakuzaba kofi au atakupiga risasi. Tulitembelea Uchina, na tulishangazwa kuona kuwa sera zao zinahimiza kila familia kuwa na mtoto mmoja. Tulijiuliza mbona hii nchi haina watu, ilhali tunasikia kwamba wamezaana ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus