Rehema Hassan

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 71.

  • 19 Nov 2020 in National Assembly: Kenya ni yetu na ni kubwa kushinda watu wote. Pia, katika hilo suala la BBI, sioni kama mwanamke anatendewa haki. Ile nafasi ya wanawake 47 ambao ni wawakilishi wa kaunti ibaki katika Bunge la Kitaifa na watupatie wawakilishi wengine kutoka Bunge la Seneti. Wale wengine The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 19 Nov 2020 in National Assembly: ambao wanapanga twende tukapambane na wanaume nguvu, tunajua idadi tunayo na tutapambana. Hatusemi ile nafasi ambayo tuko nayo tunyang’anywe. Tuachie na tuongezwe zingine. view
  • 19 Nov 2020 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view
  • 5 Dec 2019 in National Assembly: Ahsante Naibu Spika wa Muda. Nataka kumpa kongole Mheshimwa K’oyoo kwa kuleta Hoja hii ya muhimu kwa Wakenya wote. Mafuriko hapa Kenya yamekuwa ni janga kuu haswa kwa wale tunaotoka sehemu tambarare. Nasema kwa Serikali kuwa shida zingine zinaweza tatuliwa. Kwa mfano, sehemu ninaotoka ni tambarare kweli lakini kule Tana River tuna barabara za maji. Barabara hizo zinaezajengwa ili maji yasipite huko kwa wengi. Kwa mfano, katika eneo la Madogo sehemu ya Ziwani iko ng’ambo ya mto sehemu ya Garissa, barabara ya maji ni ndogo sana sehemu hiyo. Serikali ikichukua hatua inaweza kuzuia maji yasiingie kwa miji. view
  • 5 Dec 2019 in National Assembly: Kiswahili chasema kuwa ni heri kuziba ufa kuliko kujenga ukuta. Yatakikana tuwe tunayapangilia mambo kama hayo kama mitigation. Ni muhimu sana. Tunajua mapema kuwa hadhari hizi ziko miaka nenda miaka rudi. Lazima tujipange. Saa hii sehemu kubwa ya Tana River iko ndani ya maji. Mimea iko ndani ya maji na nyumba zimebomoka. Pia naomba wasamaria wema waende kwa sehemu zimehadhirika kama Tana River, Pokot na zingine wapeane misaada kwa watu wanaoumia. Kuna watu wanalala kwenye nyumba ambazo wamezifunika na nguo zao. Hawana hema. Ni vizuri wafikishiwe hema, chakula na hata madawa. view
  • 5 Dec 2019 in National Assembly: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 5 Dec 2019 in National Assembly: Kwa hayo machache, naunga mkono. Ahsante. view
  • 26 Nov 2019 in National Assembly: Asante sana, Mheshimiwa Naibu wa Spika wa Muda. Hata mimi ninaunga mkono mjadala na kutuma risala za rambi rambi kwa wakaazi wa West Pokot. view
  • 26 Nov 2019 in National Assembly: Pia, ningependa kuongeza sauti wakati jambo kama hili la huzuni limetokezea na kuwaomba Waheshimiwa wenzangu tusiwakejeli wenzetu. Wakati wenzetu wamepoteza watu wao na wanahuzunika, sisi huku tunakuja kulifanya jambo la siasa hapa. Wengine bado hawajapata watu wao, wala kuwazika na sisi hapa tunafanya siasa nyingi badala ya kutafuta suluhu ya kudumu ya hiyo shida. Mimi pia watu wangu wa Tana River tunavyozungumza, kuanzia hapa Ziwani karibu na Garissa na Garseni sehemu ya Tana Delta, watu wamepoteza makaazi, mimea na hata mifugo yao. Hawana mahali pa kulala. Mimi pia ningeomba Serikali iwasaidie. Ile idara ambayo iko kwa kaunti hata kwa Serikali ... view
  • 26 Nov 2019 in National Assembly: Kwa hivyo, ninaomba Serikali iwasaidie wale walioadhirika na mafuriko na malazi, chakula na hata madawa. Wakati wa mafuriko, magonjwa mengi yanatokea. Mimi pia, ningeomba suluhu ya kuduma ipatikane hasa kwa hili janga la mafuriko la Tana Delta. Wakati view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus