Rehema Hassan

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 71.

  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu wa Spika. Nimesimama kuunga mkono Mswada wa leo. Natoka Tana River, ambako tuna miradi mitatu ya kunyunyizia mimea maji. Kuna miradi ya Hola, Bura na TARDA. Ukweli ni kwamba hiyo miradi mitatu inaweza kulisha taifa letu la Kenya lakini, uzembe kazini na uporaji wa mali ya umma umefanya tunalia njaa. Hivi juzi, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: nilikuwa Brazil. Niliona aibu sana kusikia mkulima mmoja akisema kuwa anaweza kulisha Kenya nzima. Tuko na miradi ya unyunyizaji maji mashamba mengi sana ambayo inaweza kutufanya tujisimamie bila kuomba misaada. view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika, kwa hivyo, kama mabadiliko haya yataleta usalama kwa wakulima, nayaunga mkono. view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Pia tukibadilisha wafanyikazi wa bodi hizo, naomba pia suala la sheria kwa kimombo view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: lizingatiwe. Ukiweka mtu afanye kazi kwa afisi moja kwa muda mrefu, anajua siri nyingi sana za hiyo afisi na huanza kupora. Tafadhali tuwe tunageuza. view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Tusikize wakulima wanapolia. Mkulima analalamika kuwa meneja wa mradi wa unyunyizaji maji mashamba ni mporaji, lakini hatusikii. Mkulima ndiye anayeumia. Wakati anatuambia mtu fulani hamfai, tafadhali, tumsikize tubadilishe yule afisa ili afanikiwe. view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Kama mwakilishi wa kina mama wa Kaunti ya Tana River, ninasema tuanze kwa kubadilisha wasimamizi wa Hola Irrigation Scheme. Siku hizi tuko na nafuu sana. Mradi huo hauko vibaya sana kwa sababu watu angalau wanapata chakula kidogo. Hawapati mazao ya kuuza lakini hawalali njaa. Lakini kuna shida ndogo ndogo. Kwa hivyo wanakamati pia watembelee mradi huu kusikiza wanayoyapitia wakulima. view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Zamani tulikuwa na miradi ya unyunyizaji maji mashamba midogo midogo inayoitwa view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Kamati pia itilie maanani hilo suala. Linasaidia sana kwa sababu watu wanapata mboga na vitunguu ambavyo wanaweza kutumia nyumbani na wakiuza wanapata pesa. Hawatalala njaa. view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Zamani waatalaam wa ukulima walikuwa wengi. Naona siku hizi Serikali imeacha kuwaajiri. Hakuna waalimu wa kutosha wa kufundisha wakulima miundo misingi bora ya kisasa ili wapate mavuno bora. Hayo yote yamechangia kuanguka kwa miradi yetu ya unyunyizaji maji mashamba. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus