Rehema Hassan

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 71.

  • 26 Nov 2019 in National Assembly: ) ilikuwa inaanza ule mradi wa kunyunyizia mchele maji, waliweka ukuta mkubwa ambao waliuita band. Ile ni kama imeteremka kidogo. Ninaomba watu wa TARDA wauinue ule ukuta ili wazuie maji yasiingie kwa mashamba na majumba ya watu. Sehemu ya Ziwani, maji yakifurika hata kidogo, yanapenya na kuingia kwa mji. Pia, ningeomba Serikali ijaribu kuziba hiyo barabara ya maji ambayo inapitisha maji saa zote kutoka kwa mto na yanaingia kwa eneo la Ziwani Bakuyu mpaka Garissa. view
  • 26 Nov 2019 in National Assembly: Ninaomba tunapozungumza hapa, tuwe tunachangia kutafuta suluhu lakini si malumbano. view
  • 26 Nov 2019 in National Assembly: Asante. view
  • 25 Jul 2019 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker. I rise to ask a question to the CS for Transport, Infrastructure, Housing and Urban Development: (i) What is the status of the proposed upgrade of the Malindi-Garsen-Hola-Madogo section of the Mombasa-Garissa Road that is funded by the Government with support from the World Bank? (ii) What plans does the Ministry have to construct the said section of the road and when is it expected to commence? Thank you, Hon. Speaker. view
  • 19 Jun 2019 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninaunga mkono watu wa IPOA wapatiwe pesa hizo lakini ninazungumza kwa masikitiko. Sioni kazi IPOA wanafanya kwa sababu mwaka jana, kuna vijana wa kwangu Madogo walidhulumiwa na sijaona wakichukua hatua yoyote. Watu watatu walikufa na kuna kijana wa miaka 20 ambaye amekatwa mkono kwa kupigwa risasi na askari wa polisi na mpaka saa hii, kijana huyo amezunguka akienda kwa IPOA Garissa. Mara anazungushwa akirudi, na mpaka saa hizi, hajapata haki yake. Kwa hivyo, kama watakuwa wanaongezwa pesa hizi ili wapate kula mishahara minono minono kwa nyumba zao na wananchi wanadhulumika, mimi hata sioni faida ... view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi nami niweze kuchangia Hoja ya leo ambayo ni ya maana sana. Pili, nataka kumpatia shukrani kubwa sana Mhe. Mohamed Ali wa Nyali, kwa kuleta hii Hoja. Kabla sijaendelea kuchangia chochote kwanza nataka kupeana shukrani zangu za dhati kwa Gavana Joho wa Mombasa. Kwa kuwa alinisaidia wakati fulani, mmoja wa wananchi kutoka kauti yangu alikuwa amelazwa na mtoto wake, kwenye hospitali ya Coast General. Baada ya wiki mbili ule mtoto aliaga dunia na akakuwa na ada kubwa sana ya kulipa. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Mtoto alizuiliwa mochari, lakini nilimpigia Gavana Joho na kumwelezea hiyo shida. Kwa sababu wazazi wa yule mtoto hawana kazi, kulipa ile ada ya shilingi 300,000 ilikuwa shida sana kwao. Lakini Gavana Joho aliweza kuwasamehea hiyo ada na maiti ikatolewa na kupelekwa Tana River kuzikwa. Mungu ambariki sana, Gavana Joho. Ni wengi sana wanaopitia haya. Kando na waliofariki na wale ambao wanapitishwa kwa huduma zaidi kwenye hospitali za rufaa, kuna jambo ambalo huwa linaniumiza roho yangu. Kuna wale wagonjwa ambao wanafanyiwa dialysis, ambapo utapata kila wiki mtu anatakikana asafishwe. Utapata pengine kama ni hospitali ya serikali, mtu analipa shilingi 15,000 kila ... view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: na sukari. Kwa hivyo, watu wanaishi wakiwa wagonjwa. Pia, nataka kumuunga mkono The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: alivyozungumza Mhe. Chelule kuwa hospitali za kibinafsi ziweze kuwa na njia ya kuangaliwa vile zinalipisha wananchi kwa sababu ile yao huwa si huduma wanapatiana lakini ni biashara. Mtu amekimbilia pale, si kwa kupenda bali kuwa apate huduma na aweze kupona na kuendelea na maisha. Wakati unaenda pale, jambo la kwanza kumwona daktari peke yake ile ada anaitisha ni kama shilingi elfu tano ama 10. Hujaenda hata kuangaliwa ni ugonjwa upi uko nao. Akishamaliza kabla mtu apatiwe matibabu, anambiwa ni lazima uweke kiwango fulani cha pesa ndiyo uweze kuhudumiwa. Huyo mtu maskini anaenda pale ni mgonjwa na hana pesa halafu unamwambia ... view
  • 17 Oct 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja ya ukosefu wa ajira kama janga la kitaifa. Ningependa kuzungumzia swala la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu. Jambo la kwanza, ukosefu wa ajira umefanya vijana wetu kupotea. Wengine wamejiunga na vikundi kama Al Shabaab, na wengine wamekuwa majambazi hapa nchini kwa sababu ya kukosa ajira. Hili si jambo nzuri kwa taifa hili. Ni aibu kubwa sana. Ningependa kuongezea kwa kusema kuwa ukosefu wa ajira hapa nchini unachangiwa na mambo mengi sana. Mambo mengine ni kama vile vikwazo wakati mtu anapotafuta ajira. Wakati kazi zinatangazwa, vijana hawa huwa wamewekewa vikwazo vingi. ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus