GET /api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154181
HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "count": 1608389,
    "next": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154182",
    "previous": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154180",
    "results": [
        {
            "id": 1560002,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560002/?format=api",
            "text_counter": 993,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Likoni, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
            "speaker": null,
            "content": "hutia sahihi. Kwa hivyo, ni muhimu sana sheria hizo kutambulika kinaga ubaga haswa na Bunge la Kitaifa. Ili mikataba hii ikubalike, ni mujibu wa Bunge kutengeneza sheria nchini ambazo pia zinaambatana na Katiba yetu. Hivyo, nchi yetu inatambulika ulimwengu mzima kukubaliana. Mhe. Murugara amezungumzia kwa uwazi vifungu ambavyo vinahusiana na Mswada huu. Vifungu hivi vimeguzia maswala muhimu sana. Kwa sababu, ni lazima tujue faida na madhara ya mikataba hii katika taifa letu. Mfano ni sheria za mikataba ya kibiashara kama zile zinazohusiana na maswala ya ushuru. Je, tukikubaliana na mikataba hii, tutaboresha au kudidimiza uchumi wetu? Vile vile, mikataba hii huwa na mambo ya kisiasa yanayopinzana na tamaduni zetu. Mikataba mingi huzungumzia haki za kibinadamu. Hivi majuzi, tumeona nchi kadhaa zimekubaliana na ndoa za kijinsia. Je, iwapo mkataba kama huu hautaletwa Bungeni na sisi kufanya mashauriano, basi unaweza kutuleta madhara katika mila na tamaduni zetu za kidini za Kiisilamu na Kikristo. Kwa hivyo, suala kama hili ni suala muhimu sana. Pili, wakati wa kuadhimisha siku ya kina mama, huwa tunaenda mkutano mkubwa kule Amerika ili kuzungumzia haki za kimsingi, haswa haki ambazo zinaangalia masuala ya akina mama, watoto na walemavu. Siyo Wabunge wote wanaenda pale. Ni wachache ambao wanachaguliwa kuhudhuria mkutano ule. Wakati mwingi, unapata nchi yetu inaweka sahihi bila kuangalia mkataba vizuri. Halafu, baadaye tunaona unakiuka mila na desturi zetu ama Katiba ya taifa letu la Kenya. Mswada huu pia umezungumzia kwamba utatengeneza wakala ama gazeti ambalo litatangaza mkataba wa sheria ya kiulimwengu kuhusu jambo fulani. Kwa hivyo, Wakenya wataweza kuelewa na kufahamu. Kama Katiba inavyosema, Wakenya wapate uhuru na nafasi ya ufahamu ama kuelezwa mambo yanajiri na kupata mawasiliano ya mambo ambayo yanayotukabili katika taifa letu la Kenya. Kwa hivyo, gazeti hilo likitolewa wakati unaofaa, Wakenya watalipitia na kuwafahamisha Wabunge wao kuwa mkataba huo una madhara ama faida gani, na iwapo wanaukubali au la. Hili ni jambo la maana sana. Vile vile, Wabunge wataweza kushauriana na Waziri mhusika kama mkataba wa kimataifa unalingana na sheria na sera zetu, kabla haujaidhinishwa kikamilifu na kuchapishwa. Hivi sasa, nafikiri suala hili haliko. Tukipitisha Mswada huu na kutiwa sahihi na Rais wetu, ambaye tunamheshimu sana, utapatia nafasi Waziri na Wabunge kushirikiana na kufanya mazungumzo ili kupata mwongozo kuhusu iwapo tufuate sheria hiyo na kuithibitisha au tukatae kuithibitisha. Vile vile, tutaweza kupata nafasi muafaka ya kupiga msasa. Hii mikataba huwa kama sheria ambazo tunatengeneza katika hili Bunge la Kitaifa. Mikataba hiyo ina vifungu na maneno mengi sana kama sheria nyingine. Tutaangalia iwapo, baada ya kuikubali mikataba hiyo, tuna uwezo wa kuunda sheria katika Bunge letu ili uthibitisho uwe sawia. Hii itahakikisha kuwa tupo pamoja na yale mataifa yaliyokubaliana na mikataba hiyo. Mara nyingi, sheria hizi huwa zinakuja kisiasa sana. Unapata nchi ambazo zimejiweka pamoja, zina ushirikiano fulani wa kisiasa ama wa kibiashara na wanakubali mkataba huo. Unapata kuna nchi zingine ambazo hazishirikiani na baadhi ya mataifa katika masuala ya kisiasa ama wana mizozo au tofauti za kibiashara na, kwa hivyo, hawaungi mkono. Wakati mwingine mnajipata mumeingizwa katika mkataba na kumbe wale ambao wamekubaliana na mkataba ule ni mahasimu wa marafiki wenu katika nchi kadhaa."
        },
        {
            "id": 1560003,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560003/?format=api",
            "text_counter": 994,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Likoni, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
            "speaker": null,
            "content": "Kwa hivyo, hili ni suala nyeti sana. Sio jambo rahisi. Ni suala nyeti ambalo linahitaji mazungumzo ya kina na ushirikiano wa karibu kati ya Wakenya na Wabunge wanaowawakilisha ili kusudi wakati tunathibitisha ile tunaita kwa lugha ya Kiingereza"
        },
        {
            "id": 1560004,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560004/?format=api",
            "text_counter": 995,
            "type": "scene",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "ratification"
        },
        {
            "id": 1560005,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560005/?format=api",
            "text_counter": 996,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Likoni, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
            "speaker": null,
            "content": "ama treaty-making, tuwe tumefuata mazungumzo. Mara nyingi sisi hatutengenezi, lakini ni vizuri kuwe na uwakilishi wa watu ambao watatoa mapendekezo. Wakati huo ni muafaka wa kuyajua yale mapendekezo kabla ya ule mkataba kutengenezwa na kuletwa kwetu na kuambiwa tuweke sahihi kama taifa. Kwa sababu mkataba unazungumzia haki za The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
        },
        {
            "id": 1560006,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560006/?format=api",
            "text_counter": 997,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Likoni, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
            "speaker": null,
            "content": "kibanadamu na haki za kimsingi. Kwa kweli, haki za kibanadamu ni muhimu sana. Lakini, katika hizo haki za kibanadamu, kuna haki nyingine ambazo zinakiuka mila na tamaduni zetu, dini zetu na Afrika ama Uafrika. Kwa hivyo, lazima kila jambo lifanywe kwa utaratibu ufaao ndiposa tuwe tukiweka sahihi katika mikataba inaofaa. Namaanisha mikataba ambayo inasaidia Wakenya ambao hawana nafasi ya kuwa katika Bunge hili, ili waweze kusema kama wamekubali au kukataa mikataba hiyo."
        },
        {
            "id": 1560007,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560007/?format=api",
            "text_counter": 998,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Likoni, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
            "speaker": null,
            "content": "Kuna muda wa siku saba uliowekwa kama lazima kwa Bunge kujulishwa na watu. Ni vizuri kuwepo muda, bali sio kuletewa tu na kuambiwa tuweke sahihi ama tupatiwe vikwazo. Mara nyingi, hii mikataba ya kiulimwengu na kimataifa huja na vikwazo. Huenda wakasema hawatatupa msaada ambao wamekuwa wakitupatia."
        },
        {
            "id": 1560008,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560008/?format=api",
            "text_counter": 999,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Likoni, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
            "speaker": null,
            "content": "Kwa hivyo, Mswada huu ni wa muhimu sana na naunga mkono. Mhe. Murugara, ahsante sana kwa ufasaha wako ulivyouelezea kinaga-ubaga. Ahsante sana, Mheshimiwa Spika wa Muda."
        },
        {
            "id": 1560009,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560009/?format=api",
            "text_counter": 1000,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Hon. Omboko Milemba",
            "speaker_title": "The Temporary Speaker",
            "speaker": {
                "id": 13328,
                "legal_name": "Jeremiah Omboko Milemba",
                "slug": "jeremiah-omboko-milemba"
            },
            "content": " Very well. Ahsante sana. Mover."
        },
        {
            "id": 1560010,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560010/?format=api",
            "text_counter": 1001,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Tharaka, UDA",
            "speaker_title": "Hon. George Murugara",
            "speaker": null,
            "content": " Thank you very much, Hon. Temporary Speaker. Allow me to thank everyone who has contributed to this Bill, which is a very important Bill. Openly and candidly, Members have stated how important it is for this House to be involved in treaty-making, instead of just doing ratification alone. We should also be making treaties. I was keen to what Hon. Oundo has said, that we must be very clear on what we are doing and when the accompanying will be done. Let it be clear whether it will be at the time of signing or ratification. This will be amended further at the Committee of the whole House. Some words may have been interchanged. We will be looking at this as we move to the Committee of the whole House so that we get it right. Thank you. I beg to reply."
        },
        {
            "id": 1560011,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560011/?format=api",
            "text_counter": 1002,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Hon. Omboko Milemba",
            "speaker_title": "The Temporary Speaker",
            "speaker": {
                "id": 13328,
                "legal_name": "Jeremiah Omboko Milemba",
                "slug": "jeremiah-omboko-milemba"
            },
            "content": " Very well. It is a very progressive law. Next Order."
        }
    ]
}