GET /api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154731
HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "count": 1608389,
    "next": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154732",
    "previous": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154730",
    "results": [
        {
            "id": 1565502,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565502/?format=api",
            "text_counter": 187,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Watu wamesahau ya kwamba sisi Maseneta tuko hapa kutetea devolution. Serikali za kaunti zilipatiwa department kumi. Mara nyingi kumekuwa na shida kwa sababu pesa ambazo tumepewa ni kidogo sana na hata department zingine hazipati pesa. Pesa nyingi zimekuwa zikienda upande wa hospitali, kilimo na barabara. Hata hivyo, unapata kwamba hizo pesa hazitoshi kushughulikia mambo mengine kama mifugo. Tumeshuhudia magavana wengi wakipata shida kwa sababu wakati walipoingia ofisi walipata kuna pending bills na wage bills kubwa. Mfano ni Kaunti ya Embu. Hapo awali hapakuwa na usawa katika ugavi wa pesa kwenye makaunti. Tuliona kwamba kaunti zile ambazo zilikuwa hazijiwezi zilikuwa zinapatiwa pesa nyingi na zile kaunti ambazo zilikuwa na uwezo mkubwa zilikuwa zinapatiwa pesa kidogo. Ikafika wakati wakufanya audit ili kuona kama hizo pesa zimesaidia hizo kaunti kujimudu na zilitumika kwa njia inayofaa. Mimi ninaunga mkono counties ziweze kupewa Ksh465 bilioni ili ziweze kufanya kazi vile inatakikana. Kila wakati sisi tumeona CHPs wakija hapa kwa gate ya Bunge, wakiandamana. Hii ni aibu sana. Tungependa MPs wa Bunge la Taifa, Serikali Kuu na Treasury wajuwe kwamba Seneti inataka CHPs, madaktari na watu wengine wapatiwe pesa. Tumeona wafanyi kazi wa county government wakichelewa kupata mishahara yao na pia tunaona vile hali ya uchumi inaendelea kuwa . Pay slips nyingi zimekuwa na shida kwa sababu mambo ya ushuru wa nyumba na hata SHA zimeenda juu. Kama county governments watapata pesa, wataweza kuongezea wale wafanyikazi ili wawache kulia. Magavana wengi wako na shida kwa sababu tunaona wakati mvua inanyesha hawapati pesa za kutengeneza barabara. Kwa sasa, SHA inafanya kazi lakini magavana wanalia kwamba hakuna pesa za kununua dawa katika mahospitali. Kwa hivyo, mambo mengi yanafaa kuangaliwa. Pia mambo ya kilimo inafaa kuangaliwa. Wakati tulikuja hapa Seneti, tulipitisha tuwe CHPs na pia kuwe na agricultural extension officers. Lakini kutoka wakati huo, wengine wajawahi kupata pesa. Kama counties zitaweza kupata pesa kwa njia ambayo inafaa, hawa watu wote wataweza kulipwa mishahara yao. Mimi nikiwa Seneta wa Kaunti ya Embu, ninasema counties ziweze kupatiwa pesa. Tumesikia MPs wakisema ya kwamba counties hazitumii pesa vile inavyotakikana. Mimi ninakataa kwa sababu, kazi yao ni kupitisha pesa ikuje Seneti, ili Seneti iweze kufanya ugavi kulingana vile inafaa kuwa ndio kaunti zote ziweze kupata pesa sawa. Kazi ya Seneti ni oversight na kuangalia vile pesa inafanya kazi; hiyo sio kazi ya MPs. Tutapitisha budget ili counties zipate pesa. Pia mambo ya the National Treasury, ninakumbuka wiki jana, Waziri wa Fedha alitakikana kuja Seneti ili kujibu maswali lakini hakuja. Kwa hivyo, mambo ya Treasury inafaa kuangaliwa ili tuone kama kuna shida ndio Waziri aweze kupatia counties zetu pesa na wananchi waweze kufaidika. Wakati huu tumeona counties nyingi zimeweza kufanya kazi na pia magavana wanafanya kazi. Kusema ukweli magavana katika kaunti nyingi wanateseka sana. Wafanyikazi wanachelewa kupata mishahara na watu wengi hawapati pesa vile inafaa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
        },
        {
            "id": 1565503,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565503/?format=api",
            "text_counter": 188,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Ninakumbuka katika Kaunti ya Embu kulikuwa na shida wakati pesa iliyotolewa kwa ajili ya kununua chakula ilichelewa. Na wakati pesa ilikuja, gavana aliweza kununua mahindi akiwa amechelewa na utapata mpaka sasa huenda pesa za fertilizer hazijapeanwa ili gavana apelekee wakulima. Wakati mwingine magavana wako na ujuzi wa kufanyia wananchi kazi lakini unapata pesa zinachelewa kutoka. Kwa hivyo, wakati mwingine sio magavana ndio wako na shida; shida inatokana na Bunge ama National Treasury ambapo pesa zinatoka. Mwaka jana pesa hazikutosha. Tungependa wale Maseneta professionals ambao watachaguliwa kuenda kufanya mediation na Bunge la Kitaifa, waweze kuangalia kwamba ile pesa isipunguzwe na hata kama itapunguzwa, iende chini kidogo ndio tuweze kusaidia ugatuzi na economy za kaunti zetu ziweze kuendelea vizuri. Tumeona kwamba walipopata pesa kidogo, wameweza kuendeleza mambo ya kilimo. Wameendeleza ukulima wa majani chai, kahawa macadamia, maembe na mimea mingine. Magavana wanataka kuwe na value addition na Serikali ya Kenya Kwanza inaunga mkono. Tunataka miraa na muguka ifanyiwe value addition ndio watu waweze kuisimamisha ili katika miaka ijayo serikali kuu na serikali za ugatuzi ziweze kuendelea vizuri na economy ya kaunti zote iweze kuendelea."
        },
        {
            "id": 1565504,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565504/?format=api",
            "text_counter": 189,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Kathuri",
            "speaker_title": "The Deputy Speaker",
            "speaker": {
                "id": 13590,
                "legal_name": "Murungi Kathuri",
                "slug": "murungi-kathuri"
            },
            "content": " Sen. Mundigi---"
        },
        {
            "id": 1565505,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565505/?format=api",
            "text_counter": 190,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Bw. Naibu Spika, mimi ninaunga mkono."
        },
        {
            "id": 1565506,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565506/?format=api",
            "text_counter": 191,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Kathuri",
            "speaker_title": "The Deputy Speaker",
            "speaker": {
                "id": 13590,
                "legal_name": "Murungi Kathuri",
                "slug": "murungi-kathuri"
            },
            "content": " Sen. Mundigi, kwa sababu nilianza kuongea kabla umalize mchango wako, nitampatia Sen. Omogeni nafasi aulize swali lake. Kwa vile nilianza kuongea kabla umalize, ungesimamisha hotuba yako, ili uniskize mimi ni Spika."
        },
        {
            "id": 1565507,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565507/?format=api",
            "text_counter": 192,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Omogeni",
            "speaker_title": "",
            "speaker": {
                "id": 13219,
                "legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
                "slug": "erick-okongo-mogeni"
            },
            "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Hii Seneti ni Bunge la rekodi na Wakenya wanashuhudia Mswada huu na jinsi tunavyozungumza hapa kwenye runinga zao. Tunapaswa yale mambo ambayo tunazungumza hapa, yawe ni ya ukweli na tukiulizwa swali tunaweza kutetea. Ninataka kuuliza hoja ya nidhamu kwa rafiki yangu Seneta wa Embu. Amesema kwamba yeye anangoja siku ambayo Serikali itafanya Muguka kuwa na value addition. Ningependa Sen. Mundigi atueleze, kutokana na sayansi yetu, kuna utafiti ambao umefanywa ambapo anaweza kusema kwamba kweli Muguka inaweza kufanyiwa value addition? Ningependa kuelewa kutoka kwa Seneta wa Embu."
        },
        {
            "id": 1565508,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565508/?format=api",
            "text_counter": 193,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Kathuri",
            "speaker_title": "The Deputy Speaker",
            "speaker": {
                "id": 13590,
                "legal_name": "Murungi Kathuri",
                "slug": "murungi-kathuri"
            },
            "content": " Proceed, Sen. Mundigi."
        },
        {
            "id": 1565509,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565509/?format=api",
            "text_counter": 194,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Bw. Naibu Spika, nilisema pesa iweze kupatikana ili mkulima aweze kufaidika. Sen. Omogeni alipokuwa anazungumza hapa alisema kwamba Mount Kenya wamekuwa favoured katika mambo ya kilimo. Lakini mambo mengi yanafaa kuangaliwa ndio wakulima wote Kenya wafaidike. Ukulima wa mimea kama muguka na miraa, majani chai na hata sukari inafaa iangaliwe ndio mkulima apate value addition na awache kutaabika. Hata kama haijakubaliwa, kuna mambo inafaa kufanywa ndio wakulima wote katika Kenya waweze kufaidika."
        },
        {
            "id": 1565510,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565510/?format=api",
            "text_counter": 195,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Kathuri",
            "speaker_title": "The Deputy Speaker",
            "speaker": {
                "id": 13590,
                "legal_name": "Murungi Kathuri",
                "slug": "murungi-kathuri"
            },
            "content": " Sen. Omogeni, aliuliza kama muguka unaweza kufanyiwa value addition? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
        },
        {
            "id": 1565511,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1565511/?format=api",
            "text_counter": 196,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Mundigi",
            "speaker_title": "",
            "speaker": {
                "id": 13586,
                "legal_name": "Alexander Mundigi Munyi",
                "slug": "alexander-mundigi-munyi"
            },
            "content": "Bw. Naibu Spika, muguka unaweza kutengeneza juice, wine hata dawa ya kufufua mwili iwapo mtu amedungwa sindano akawa hali mahututi. Kinachofaa ni pesa za kufanya utafiti zitolewe. Ninaunga mkono pesa nyingi zitolewe na Serikali iangalie utafiti wa mimea mingi sio muguka pekee."
        }
    ]
}