GET /api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=157108
HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "count": 1608389,
    "next": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=157109",
    "previous": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=157107",
    "results": [
        {
            "id": 1589272,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589272/?format=api",
            "text_counter": 313,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Kinyua",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, swali ambalo tunapaswa kujiuliza pingamizi hii ya awali inaletwa kwa nini? Ni vizuri kwa sababu, katika Seneti hii na vile vile katika gatuzi zetu, tunapaswa kufuata sheria. Ni kinaya ikiwa tunatunga sheria, lakini hatuzifuati sheria zenyewe. Ukiangalia katika Taarifa Rasmi ya Bunge la Isiolo, hakuna kikao chochote kilichofanyika. Kwa hivyo, ikiwa hakukuwa na kikao chochote, sioni kwa nini tunapaswa kushughulikia jambo hili. Ikiwa hapakuwa na kikao chochote na hapo ndipo kungeshughulikiwa mambo haya, Seneti hii inapaswa kusema kwamba hilo pingamizi la awali tunalikubalia ndiposa sheria zifuatwe. Utaratibu wa sheria usipofuatwa, basi hakuna jambo ambalo tutalifanya hapa. Nilimsikia Sen. Faki akisema ya kwamba tuendelee kusikiliza ushahidi wa kutosha ndio tunaweza tukapata mambo mengi zaidi. Ikiwa sheria haikufuatwa kuanzia mwanzo, sioni haja yoyote ya sisi kusikiliza kesi hii kwa sababu, wahenga wanasema kwamba “Usikate kanzu kabla ya mtoto kuzaliwa.” Sisi hatuwezi kusikiliza. Tunajua ya kwamba katika gatuzi nyingi kuna shida nyingi. Laikipia, Nandi, Isiolo na kaunti nyingi kuna shida. Hata hivyo, hatutatua shida bila kufuata utaratibu wa sheria. Ni kinaya kwa sababu sisi ndio tunatunga sheria. Gatuzi hiyo ya Isiolo wanatunga sheria. Ikiwa hatutaweza kufuata Kanuni za Kudumu ambazo sisi tumeziweka, hakuna haja ya kuketi hapa; tunapaswa kuwa tumefunga virago na kuenda nyumbani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
        },
        {
            "id": 1589273,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589273/?format=api",
            "text_counter": 314,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Kinyua",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Ndiyo, ninajua ya kwamba Gavana wa Kaunti ya Isiolo anaweza kuwa na shida, lakini tunapaswa kufuata sheria. Sheria zikifuatwa sina hofu rohoni mwangu. Watu wa Isiolo wanataka haki itendwe lakini, sheria ni kama msumeno; inakata mbele na nyuma. Kwa hivyo, tufuate sheria na tukifuata sheria ukweli utapatikana lakini kwa leo ninaunga mkono pingamizi ya hapo awali kwamba hakukuwa na vikao katika Bunge la Isiolo."
        },
        {
            "id": 1589274,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589274/?format=api",
            "text_counter": 315,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Hon. Kingi",
            "speaker_title": "The Speaker",
            "speaker": null,
            "content": " Sen. Shakila Abdalla, you may proceed."
        },
        {
            "id": 1589275,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589275/?format=api",
            "text_counter": 316,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Asante, Bw. Spika. Hii ni Hoja muhimu sana leo. Ni muhimu kwa Bunge hili la Seneti kutoa uamuzi ambao utaridhisha kila mtu katika Kenya yetu kwa sababu utakuwa ni mfano mwema wa usoni. Hapa ninaona mambo ni mawili. Kuna mchakato na kuna ushahidi. Pengine watu wa Kaunti ya Isiolo wako na ushahidi na kesi ya kwamba wana haki ya kuimpeach gavana wao lakini mchakato ambao ni process haukufuatwa. Kwa hivyo, tunaomba ikiwezekana, huu mvutano uishe, kufuatwe mchakato ambao umewekwa kikamilifu. Mswada uletwe hapa tumalize hii kazi. Changamoto ambayo nimeona hapa ni kwamba mchakato ama process haikufuatwa. Kwa hivyo, kama kuna ushahidi na kama wako Hoja ya kutosheleza"
        },
        {
            "id": 1589276,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589276/?format=api",
            "text_counter": 317,
            "type": "scene",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "kumuimpeach"
        },
        {
            "id": 1589277,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589277/?format=api",
            "text_counter": 318,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "gavana wao wafuate mchakato, walete hiyo Hoja na kazi ifanyike. Asante, Bw. Spika."
        },
        {
            "id": 1589278,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589278/?format=api",
            "text_counter": 319,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Hon. Kingi",
            "speaker_title": "The Speaker",
            "speaker": null,
            "content": " Proceed, Sen. Cherarkey."
        },
        {
            "id": 1589279,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589279/?format=api",
            "text_counter": 320,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Cherarkey",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Mr. Speaker, Sir, you need to protect me from the Senate Majority Leader because he is telling me something in my local language. Under Article 126, the law is very clear on the sittings of Parliament. If some of us are saying that the process is not important, however, the process and the outcome is as important as the law. In the Raila Odinga case in the petition of 2017, Uhuru Kenyatta’s win as President was nullified because of only process. So, if the highest court, the Supreme Court of the Republic of Kenya has given direction and weight on the issue of process, who are we? The Senate cannot participate in settling clannism, regional or any politics. We only deal with the rule of law, which involves the Constitution and the process. The reading of Standing Order No.65 of the Isiolo County Assembly, Standing Orders and Standing Order No.36 is very clear on the sittings and the procedure of impeachment of the governor. We have had cases where there were two clerks and there were conflicting gazette notices. For a House to be functional, it should be in a gazetted place; we should have a speaker, a mace and a House Business Committee that organizes the business of the House. We should have necessary modification to ensure there is proper sittings. On this aspect, the County Assembly has struggled. I am the greatest champion of MCAs. I have always wished that their welfare be looked at. I have always wished that they have the Ward Development Fund, but they must follow the law. We cannot hang an innocent man as Lord Denning would say, “I better send 10,000 guilty men than to hang in gallows one innocent man.” Today evening we are invited to decide. We have set the precedent. With all due respect, I want to advise the Senate Majority Leader to have faith in his own committees. If there is a problem in Isiolo County Assembly, the Standing Committee on Devolution and Intergovernmental The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
        },
        {
            "id": 1589280,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589280/?format=api",
            "text_counter": 321,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Cherarkey",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Relation chaired by Sen. Mohamed Abass should pick it up immediately the way we did with Nyamira and sort out that issue, once and for all. That is why we have committees. By the time we agree, I even asked a question whether they have a YouTube channel. Senate proceedings are being televised live. You can realize there was no media, there was no live stream; they do not have a YouTube channel and there is a website, but it does not function. We just needed that evidence to know whether the sitting was done, including the recordings. In fact, my colleague, learned senior said that the HANSARD was vandalized. Then how did you cook the HANSARD reporting before the House? We know there are people who are experts in cooking chai and mandazi, but the Senate cannot be part of icing or putting any kachumbari into the process that have been--- Mr. Speaker, Sir, I support this Motion."
        },
        {
            "id": 1589281,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589281/?format=api",
            "text_counter": 322,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Kibwana",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Asante, Bw. Spika. Mchakato wa kung’oa kiongozi aliyechaguliwa na watu sio jambo rahisi; ni jambo nzito. Hapa Seneti, wanauliza kitu kidogo tu: Ushahidi uko wapi? Sitazungumza sana lakini ningependa kuuliza tu: Kama kuna ushahidi wowote ungeletwa na tuweze kuendelea. Tulikuwa hatuna haraka yoyote. Kama hamuna ushahidi wowote na kweli tumeona video, tukajaribu kuuliza maswali na tukajibiwa kwamba hapakuwa na kikao. Kwa hivyo, tunasikitika sana kuwa labda huu ushahidi uliletwa bila kujitayarisha vilivyo. Huyu kiongozi anafaa kung’olewa lakini pia ang’olewe kwa njia ya haki."
        }
    ]
}