18 May 2021 in Senate:
Bi Spika wa Muda, wacha niseme mawili au matatu ambayo nilijifunza kutoka kwa Hotuba ya Rais Suluhu Hassan, majuma mawili yaliyopita. Bado ninakumbuka mambo hayo vizuri sana na pia ninafikiria wakati wowote ninapofikiria kuhusu uhusiano kati ya Kenya na Tanzania. Tanzania imebarikiwa na viongozi wa kike ambao wanaendesha uongozi wao kwa njia inayofurahisha. Iwapo wewe hufuatilia maswala ya Bunge la Tanzania na uongozi, utanielewa. Kuna viongozi watatu wa kike ambao mimi huwafuatilia sana uongozi wao na yale wanayofanya.
view
18 May 2021 in Senate:
Kiongozi wa kwanza ni Dr. Tulia Ackson, ambaye ni Naibu wa Spika katika Bunge la Tanzania. Kwa wale ambao hushiriki michezo ya mwisho wa mwaka miongoni mwa Mataifa ya Jumuia ya Afrika Mashariki, mnajua yeye hupenda riadha. Mbali na
view
18 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
18 May 2021 in Senate:
hayo, nimefuatilia uongozi wake pia. Mwingine ambaye pia tumepatana michezoni na nimefuatilia na kupenda uongozi na mawazo yake, ni Mama Salma Kikwete. Yeye ni Mbunge Mteule na pia kiongozi nchini Tanzania.
view
18 May 2021 in Senate:
Kiongozi wa tatu wa kike ambaye nilikuwa nikimfuatilia tangu akiwa Naibu wa Rais, ni huyu Mama, Samia Suluhu Hassan. Sijui kwa nini lakini ninaona mambo mengi aliyosema katika Hotuba yake hayakuwa mageni. Sio mambo ambayo hatujawahi kuzungumzia hapa Bungeni au kuyasikia kutoka kwa viongozi wengine. Hata hivyo, alizungumza kwa sauti yake ya upole na ustaarabu, alichukua nafasi yake na kutueleza huku akisita ili kuhakikisha tunamwelewa. Mambo hayo yamebaki akilini mwangu na kwa Wakenya wengi. Iwapo unafuata mazungumzo ya Wakenya katika maeneo ya burudani au hata mitandao ya kijamii, utaona Wakenya wengi wameelewa umuhimu wa kuwa na uhusiano mwema kati ya ...
view
18 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
18 May 2021 in Senate:
ubishi. Ni msomi. Mkiwa na tofauti za kimawazo, anaamini akupe nafasi useme yako kisha na wewe umsikize na hatimaye mkubaliane. Sijui nitakuwa nimekosea nikisema hili lakini jambo hilo lilifanya nikafikiria tungekuwa na viongozi wengi wa kike hapa barani Afrika, pengine tungekuwa mbele zaidi, kinyume na sisi wanaume tulio uongozini. Sisi wanaume tunaamini kama hukubaliani na mawazo yangu, basi tupigane, turushiane cheche za maneno ili nikuonyeshe jinsi niko na nguvu. Hayo hayakuwa mawazo ya Rais Suluhu.
view
18 May 2021 in Senate:
Nimeeleza kwamba hayo hata sikupata kwa mazungumzo yake peke yake bali nimekuwa nikimfuatilia hata akiwa kwao.
view
18 May 2021 in Senate:
Mimi nimepata nafasi kumfuatilia hata akiwa kule nyumbani kwao. Nakumbuka wakati mmoja alikuwa anazungumuza na wafanyikazi wa serikali wanaofanya kazi katika Tanzania Revenue Authority (TRA), kitengo chao cha kukusanya ushuru. Alikuwa anawazungumzia akiwaelezea kuhusu uhusiano kati yao na wafanyibiashara. Hapa nchini Kenya, Bi. Spika wa Muda, unajua kama kuna jambo ambalo wafanyibiashara wanaogopa na pahali wanateswa zaidi ni katika ofisi za Kenya Revenue Authority (KRA), wale ambao wanakusanya ushuru nchini. Mara nyingi, watu wengi hawapendi kuenda kule. Nakumbuka wakati mmoja nikiangalia Rais Suluhu Hassan akizungumza na wale akiwaeleza, “Tafadhalini, kama mna jambo ambalo mmetofautiana na mfanyibiashara yeyote, hakikisha kwamba mmekaa ...
view
18 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view