16 Jun 2021 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. Once he starts interrogating the matter, it is very clear and straightforward. It is just that some people insist on doing other things. I am confident, knowing the Committee’s capability that they can give us a response in earlier than three weeks. The earlier the better.
view
15 Jun 2021 in National Assembly:
Hon. Speaker, I beg to speak in English so that my leader can know that I am educated enough. Pursuant to the provisions of Standing Order 44 (2) (c), I seek to request a statement from the Chairperson of the Departmental Committee on Education regarding renewal of teachers’ Collective Bargaining Agreement (CBA). The current Collective Bargaining Agreement (CBA) between the Teachers Service Commission and teachers across the country is set to expire in a matter of weeks, thereby creating unwarranted anxiety amongst teachers. Already, the Kenya National Union of Teachers (KNUT) as well as the Salaries and Remuneration Commission (SRC) ...
view
15 Jun 2021 in National Assembly:
(i) Within which specific timelines is the TSC planning to submit its CBA proposals for teachers in order to renew the current CBA that is about to expire? (ii) How many KNUT members have either not been promoted or have not received salary increments as per the existing Collective Bargaining Agreement? I thank you, Hon. Speaker.
view
9 Jun 2021 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. Accept my apologies. Mine was actually about a Statement that I meant to present. Thank you.
view
9 Jun 2021 in National Assembly:
Asante sana Mhe. Spika. Kupitia Kanuni za Kudumu 44(2)(c), naomba kupata jawabu kutoka kwa kamati husika ya Elimu kuhusu mambo ya Serikali kulipia wanafunzi wa shule za upili karo. Serikali iliweka mikakati kulipia wanafunzi wa shule za upili mwaka wa 2008 ili kuhakikisha kila mtoto anaweza kupata elimu licha ya kipato cha jamii yake. Hali hii ilisababisha wanafunzi kuwa wengi na kuongezeka katika shule zetu. La kusikitisha, Waziri wa Elimu, juzi ametoa amri kwa walimu wakuu wa shule hizi kufukuza wanafunzi ambao wana deni la karo. Hakuachia hapo. Alidai kuwa wazazi hawalipi karo kusudi licha ya kuwa wana uwezo. Matamshi ...
view
9 Jun 2021 in National Assembly:
(i) Serikali yafanya nini kuhakikisha kila mtoto amesoma licha ya anapotoka wala uwezo wake? (ii) Hizi kauli za Waziri ni msimamo wa serikali au ni kauli yake mwenyewe ya kibinafsi? (iii) Lini Waziri atarekebisha kauli yake na kuwaomba Wakenya msamaha? Asante sana, Mhe. Spika.
view
9 Jun 2021 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika. Tatizo si wiki mbili. Tatizo ni ombi letu. Nina imani kuwa wale wenye kufikisha habari hizi kwa Serikali wanajua kwamba watoto wetu kila wakikaa nje ya shule inawawia rahisi kuingia katika uhalifu. Watoto hawa hawa ndio wataingia katika mambo yasiyofaa kijamii. Kwa hivyo, tukumbuke kuwa wiki mbili hizi ni mamilioni ya watoto ambao watapoteza maisha yao na ni lazima mtu aweze kuchukua jukumu. Kwa hivyo itakuwa ni bora apunguze ili tujue msimamo ni wa Serikali au mtu binafsi.
view
8 Jun 2021 in National Assembly:
Yes, Sir. Mhe. Spika, ningeomba nikariri kilio hiki kwa Kiswahili ili tuweze kufahamikiana. Niko na Ardhilhali ya umma, ambayo kwa lugha maarufu ni Public Petition, Nambari 22 ya 2021. Tukitukuze Kiswahili kiongozi wangu ili tufahamikiane hapa na nje ya Bunge pia. Ardhilhali Nambari 22 ya mwaka 2021 inayohusu pingamizi za biashara mjini Mombasa. Mhe. Spika, mimi, Mhe. Abdullswamad Nassir, Mbunge wa eneo la Mvita, kwa niaba ya wafanyibiashara katika Kaunti ya Mombasa na hususan wafanyibiashara wadogo katika Mama Ngina Water Front, kwa jina jingine Light House, na Jomo Kenyatta Public Beach ama kama inavyojulikana Bamburi Beach, nataka kufahamisha Jumba hili ...
view
8 Jun 2021 in National Assembly:
Kwa hivyo, Mhe. Spika kwa unyenyekevu, ombi langu ni kuwa Bunge hili, kupitia Kamati ya Biashara, Viwanda na Vyama vya Ushirika, liingilie kati na liangalie jambo hili haraka iwezekanavyo. Watu warejee na wafanye biashara zao katika Mama Ngina Recreation Centre, Light House, Jomo Kenyatta Public Beach na katika sehemu zingine Mombasa. Vilevile, ikiwa kutakuwa na maoni yoyote Kamati itazingatia, tuko radhi na sawa kuweza kuyafuata.
view
8 Jun 2021 in National Assembly:
Asante sana.
view