5 Dec 2019 in National Assembly:
Mhe. Naibu wa Muda, ningependa tu kutoa shukrani na kuwajulisha wenzangu ya kuwa ifikapo 6.00 p.m. na hatujaweza kumaliza, nataka kufafanua ili wenzangu wafahamu kwa nini tunakata mazungumzo. Ni kwa sababu Mhe. K’oyoo alikuwa ameomba ikifika 6.00 p.m., Bunge lisimamishwe lizungumzie swala la maafa ya mafuriko.
view
5 Dec 2019 in National Assembly:
Kwa hiyvo, mimi natoa shukrani na sasa tunaacha jukumu hili kwa Kenya Ferry Services, Kenya Maritime Authority na Wizara. Kama Wajumbe tumefanya kazi yetu; tumeweza
view
5 Dec 2019 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
5 Dec 2019 in National Assembly:
kumaliza; na mimi natoa shukrani kwa kila aliyehusika: Wajumbe wenzangu, wafanyikazi wa Bunge wakiwemo makarani, afisi ya Spika na afisi ya Karani Mkuu. Ahsante sana, nawatakia likizo yenye heri na fanaka.
view
4 Dec 2019 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naomba kuwasilisha Hoja ifuatayo: THAT, this House adopts the Report of the Public Investments Committee on its Inquiry into the Safety of Ferries as observed in the Audited Accounts of Kenya Ferry Services for the Financial Year 2016/2017,laid on the Table of the House on Tuesday, December 3, 2019. Katika Ripoti yake ya mwaka wa 2016/2017, Mkaguzi Mkuu alitaja na kuweka wazi kuwa milango ya ferry haikuwa inafanya kazi na ferry zilikuwa zinafanya kazi bila marekebisho kwa mda. Tunapoongea sasa hivi, dakika chache zilizopita, kuna ferry ambayo imekwama katikati ya bahari na ferry ...
view
4 Dec 2019 in National Assembly:
Takriban siku tatu or nne zilizopita, kwa sababu ya milango kutofanya kazi, mtu mmoja kwa sababu ya mvua, aliteleza na kuingia ndani ya maji. Lau angelikuwa mjasiri na kama hakungekuwa na boti ya haraka, leo tungekuwa tunazungumza masuala mengine. Kenya haitasahau tarehe 29 September 2019. Wakenya wawili, mama na mwanawe, walipoteza maisha yao. Ninapongeza wanakamati wenzangu kwa kazi waliofanya. Naipongeza afisi ya Karani Mkuu wa Bunge na pia afisi ya Spika kwa usaidizi wa kuhakikisha kuwa tumeandaa Ripoti hii.
view
4 Dec 2019 in National Assembly:
Tunavyoongea, hizi ferry mpaka sasa milango haifanyi kazi. Feri inatumia Kshs102 milioni kila mwaka ili kulipia gharama ya mafuta ya kuendesha lakini asilimia 25 ya hiyo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
4 Dec 2019 in National Assembly:
imesababishwa na milango kutoafanya kazi. Waswahili wana msemo ya kuwa tunatupa shilingi ili tuokote penny. Hatutengenezi lakini tunazidi kudidimia. Katika ukaguzi wetu, tuliita Kenya Maritime Authority (KMA), Waziri mhusika, Kenya Ferry Services (KFS) na tukaenda hadi kwa feri zenyewe. Tunaomba Bunge likubaliane na nasi. Ninajua kuwa ni tembe chungu na sindano chungu ambao lazima tuikubali ili pawe na mwelekeo bora. Kwanza shirika la KFS, Ripoti hii ikikubaliwa na Bunge inafaa kuhakikisha kuwa feri ya MV Harambee imewekwa kando na ifanyiwe dry docking ama ukaguzi na utengezaji wa feri kwenye kitanda chake pale chini.
view
4 Dec 2019 in National Assembly:
Pili, ni jambo la kusikitisha. Katika ukaguzi, ilitokea wazi hakuna ukaguzi wowote unaoendelea kwa feri hizi. Tulipowauliza wakaguzi kama waliona kuwa milango haifanyi kazi, walisema walikuwa wameona. Hakuna aliyekipofu kujua kwamba milango ya feri haifanyi kazi. Tunaambia KMA kuwa feri zilizobaki zifanyiwe ukaguzi upya, zile cheti wamezitoa za bandia bila kufikiria zirekebishwe. Feri ikiwa haipo sawa, isimamishwe isiendelee kufanya kazi.
view
4 Dec 2019 in National Assembly:
Tatu, tunataka Serikali kupitia kwa Wizara ya Fedha, itoe pesa kwa KFS. Tulipokuwa tunafanya Ripoti hii, ilisemekana kuwa fedha zinatoka lakini baada ya ile siku tulikuwa tunaandika Ripoti, fedha hazikuwa zimefika kwa KFS. Kwa hivyo, tunashurutisha Serikali itoe fedha za kuhakikisha kuwa marekebisho yamefanyika. Pia, hizi fedha ziziregeshwe tena katika Serikali Kuu mwisho wa mwaka bali zibaki ili zitumike kutengeneza feri. Kwa lugha ya kitaaluma ya Bunge na sheria, zile fedha ziwe ring-fenced . Pili, afisi ya Mkaguzi Mkuu iangalie ule mkataba uliopo baina ya kampuni ya African Marine and General Engineering na KFS kwa sababu hiyo ndio kampuni pekee ...
view