9 May 2019 in National Assembly:
mfumo mpya wa Kenya inavyoendeshwa, Bunge hili hili likaamua kutoa kipengele kile kuwa, hakuna yeyote anayeweza kuinua sheria yoyote ya Bunge isipokuwa Bunge lenyewe. Lakini, huu Mswada kisawasawa – lau hawana nia mabaya na hakuna nia chafu katika masuala haya – ilikuwa iletwe kwa kupitia Mswada wa maana si Mswada kumba ambayo kuna uwezekano wa watu kutoweza kuona na kujua ni kitu gani kinachoendelea. Bunge hili lilikataa ilhali tunaletewa Mswada ili tukubali ya kuwa Waziri akiamua, licha ya mambo yaliyopitishwa Bungeni, anaweza kuinua sheria ambayo imewekwa na Bunge hili kwa kalamu yake. Kuna mambo mengine tutayahisi…
view
9 May 2019 in National Assembly:
Ndugu yangu, Mhe. Duale anasema kuwa hafahamu lugha yangu, lakini ningeomba zile dakika zilizobaki niweze kutoa duku duku langu, nisije nikazungumza kwa lugha ambayo pengine ni ya hasira nikaambiwa ni saumu. Ni zile hisia za hawa watu wanaojaribu kutuchukua sisi. Ukienda katika maeneo, anapotoka Mhe. Duale, ni mfano wa kuuziwa mifugo kwa kuonyeshwa wayo wa wale mifugo waliopita. Unaambiwa kwa kuangalia mfugo ule amepita hapa, amewanda na ukiangalia zile kato vile alivyoweza kupita pale… Kule kwetu mfano mwingine unaoweza kutumiwa ni kupelekwa katika bahari kisha uone yale mawimbi yanavyopigwa, mvuvi aanze kukuuzia samaki akuambie hapa kuna sulisuli, kolele, papa na ...
view
9 May 2019 in National Assembly:
Mhe. Spika, wakati mwingine kuna watu ambao hawafahamu zile sheria za Bunge wanaona kwa kuita jina lako wao hutukatiza maneno. Katika hali yaa kutukatiza maneno, hatufahamu nia yao ni ipi. Ningemuomba aache niendelee ama umkataze kuendelea kuzungumza…
view
9 May 2019 in National Assembly:
Ningependa tu kueleza kuwa lau wangekua na nia safi, Mswada huu ungeletwa kwa njia yaa kisawasawa sio kwa njia ya Mswada kumba. Huu Mswada Kumba ukiletwa, njia na madhumuni na nia ilikuwa ni Mswada kama huu ukiwekwa huwa ni Mkusanyiko wa sheria tofauti tofauti lau kuna mabadiliko ya herufi na mambo madogo madogo ambayo hayana uzito wa maana hivyo. Lakini leo kupeleka Mswada kama huu kwa kupitia njia hii, ni njia ya ulaghai ambayo inatumika. Watarejea hapa. Ningependa kulielezea Bunge kupitia kwako wewe Spika kuwa huu Mswada ukibadilishwa, njia na madhumuni ni nini? Serikali ya Japan ilitoa bilioni 27 kukajengwa ...
view
9 May 2019 in National Assembly:
KPA, asilimia12.5 ni ya Unimar na asilimia12.5 nyingine ni ya kampuni DEG. Lakini Serikali wamekubaliana na kabla ya sheria kupitishwa, lakini hizo hisa hazijatolewa. Hivi sasa, KPA ina asilimia 53, Kampuni ya AON ina asilimia 23, kampuni ya Unimar ina asilimia 7, na Kampuni ya DEG ina asilimia saba. Sasa wanajaribu…
view
9 May 2019 in National Assembly:
Ningeomba kiongozi anipatie ruhusa
view
9 May 2019 in National Assembly:
Mhe. Spika, asante sana. Hii ni barua iliyoandikwa kwa Karani Mkuu wa Bunge. Haya si maneno yangu mimi. Kwa ruhusa yako, Bwana Spika, ningeomba niiweke katika meza waweze kuikubali ama kuikataa karatasi hii.
view
9 May 2019 in National Assembly:
Unajua tatizo hapa ni kuwa kila mmoja hujifanya kuwa Spika katika Bunge hili. Ningeomba tu niweze kutaja jambo lingine hapa kwa sababu katika hisia ambazo wanajaribu kutumia, hawa mabwana; la kwanza na la pili wanasema kutakuwa na nafasi za kazi. Suala lile tunajiuliza sisi, hatukatai na hakuna anayepinga ya kuwa ni sawa tuwe na maendeleo na kuwe na usawa katika nchi. Kwa nini iwe ni kampuni moja pekee yake ambayo imepatiwa nafasi hii bila ya kuwa na mkataba wa maana ambao umefuata sheria? Kwa nini ikiwa tunataka kupeana port yetu kwa kampuni kwa sababu KPA imeshindwa kuiendesha, kwa nini kusiwe ...
view
9 May 2019 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika. Nashukuru kwanza kwa mwelekezo wako kuhusiana na karatasi hii. Pili, hii karatasi hawakutupatia sisi tulipokuwa katika kikao cha Bunge. Tulikuwa tumeitwa kama Wajumbe wa Pwani. Katika hali The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
9 May 2019 in National Assembly:
ya kuuliza, hii karatasi waliitoa pale. Sio kuwa tumeitoa katika kamati. Tatu, nasisitiza tena ya kuwa lao, nia na madhumuni yao ni kuhusiana na mambo ya wafanyikazi. Kwa nini yale maswali yote ambayo tumeyauliza, si mara mora si mara mbili, bali mara tatu, majibu ambayo yameletwa katika Bunge hili wakakubali ya kuwa kuna matatizo na wakasisitiza ya kuwa watabadilisha sheria? Mpaka leo hawajafanya jambo hilo. Licha ya hayo, wamejaribu kupenyeza mambo kwa njia ambayo sio mwafaka. Asante sana, Bw. Spika.
view