All parliamentary appearances

Entries 121 to 130 of 232.

  • 9 Apr 2015 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Eneo la Tana River lilikuwa limesahulika kwa miaka nyingi. Lakini leo wakati kuna pendekezo la Tana River kusaidiwa, je, kwa nini sasa Wakenya wasiwe na huruma kwetu? Naomba Maseneta wenzangu waangalie masilahi ya wengine. Sala wa Bwana inasema: “Mtakie mwenzako lile unalojitakia nafsi yako.” Wengine wamebarikiwa na maendeleo. Je, ukiamua leo kwamba sisi pia tujengewe nyumba kisha tujenge yako kesho, kuna shida? Nawaomba wenzangu kwamba mimi ni mmoja wenu. Naomba tupewe pesa hizo leo ili mpate kura yangu. Asante. view
  • 2 Apr 2015 in Senate: Asante Bi. Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii ya mapunzi ya kikao cha Seneti. Leo hii tuna huzuni na tunaomboleza katika nchi yetu. Wakenya wenzetu wameadhirika. Naomboleza na ndugu zangu walio huko Garissa. Kabla sijaendelea, naomba Mungu azirehemu roho za wale waliohadhirika. Tunaomba kwamba Mungu atawafariji wazazi wa Garissa ambao watoto wao walipata shida. Huu ni wakati wa Seneti kusimama wima na kukabiliana na matatizo yanayoikumba Kenya yetu. Seneti inategemewa sana na Wakenya kwa sababu huwa inasimama wima na kutetea ukweli. Tangu Seneti ianze kukaa, sijasikia Wabunge wakizungumza mambo ya mishahara. Jambo la muhimu katika maisha ya binadamu ... view
  • 31 Mar 2015 in Senate: Madam Spika wa Muda, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Ningependa kutoa pongezi kwa Rais wetu wa Kenya kwa kutambua kwamba Wakenya wamedhulumika. Pia, nampongeza Rais wetu kwa kutambua kwamba mambo mengi yamefanyika katika nchi yetu na Wakenya wametatizika na kuumia kwa mikono ya viongozi na wakora waliopora rasilmali zetu. view
  • 31 Mar 2015 in Senate: Madam Spika wa Muda, sisi kama viongozi, ni lazima tuige mfano uliotolewa na Rais wetu, Uhuru Kenyatta. Hatua hii ya Rais ni ya kusisimua na kupendeza; yafaa kuigwa na watu wote. Sisi, kama viongozi, ni lazima tuzungumze ukweli na tufuate mwenendo mzuri kama huu. Madam Spika wa Muda, kuambatana na habari iliyotolewa hapa na Rais kuhusu ripoti ya Tume ya Kupambana na Ufisadi ( Ethics and Anti-Corruption Commission ) iliyowasilishwa hapa, inasema kwamba ripoti hiyo sio ya ukweli; inasema kwamba ripoti hii imetayarishwa kwa njia ya mapendeleo. Tuko na uhakika kwamba kuna ufisadi unaofanyika katika kila pembe ya Kenya hii. ... view
  • 31 Mar 2015 in Senate: Madam Spika wa Muda, kuna baadhi ya watu waliotajwa hapa kwa tuhuma za ufisadi lakini hatuoni ni ufisadi gani uliotajwa dhidi yao. Kwa mfano, katika Kaunti yangu ya Tana River, kumetajwa watu kadhaa hapa kama Ismail Jillo, Salim M. Dame, Hassan Bare Kuno na Swaleh Salad Abashora. Mmoja wao ni County ExecutiveCommittee (CEC) Member, Finance; mwingine ni CEC, Water; mwingine ni CEC, Sanitation na mwingine ni CEC wa Education . Huyu Bare ni CEC wa Education na ametajwa pamoja na Swaleh, na yale ambayo yanatajwa juu yao yote ni tofauti. Kwa hivyo, hii inaonesha wazi ya kwamba kuna ukora ndani ... view
  • 31 Mar 2015 in Senate: Thank you, Madam Temporary Speaker. view
  • 4 Mar 2015 in Senate: Bw. Spika ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii nikiwa na masikitiko makubwa sana, kwa sababu huu ni wakati Wakenya wengi wanaomboleza ufisadi uliokithiri nchini. Wakenya wengi wameathirika kwa mikono ya viongozi ambao hawajali hali ya wanyonge. Wakenya walituchagua kuambatana na sheria na kutupatia uwezo wa kuwakilisha kaunti zetu. Kufuatana na Kipengee 96(1) na (2) tumepewa uwezo wa kuwawakilisha, kuwalinda, kuwatumikia, kuwatatea na kuunda sheria zinazoweza kuleta maendeleo nchini Kenya. Hatukuchaguliwa kukaa hapa Bungeni na kusindikiza wafisadi na wakora. Bw. Spika inafaa hii Seneti ipeana mwongozo kwa Wakenya. Inafaa tume maalum ibuniwe ili ichunguze kiwango ambacho ufisadi umeathiri nchi ya Kenya. Asilimia ... view
  • 4 Mar 2015 in Senate: Bw. Spika, hiyo asilimia 99 ni kulingana na hekima, fikira na uchunguzi wangu. view
  • 4 Mar 2015 in Senate: Bw. Spika, hata Sen. (Dr.) Khalwale hawakilishi Kaunti ya Kakamega peke yake, bali anawawakilisha Wakenya wote ili wapate hudumu kule mashinani. Watu wanapigana ngumi na kuteta huku wakitaka pesa zipelekwe mashinani. Hiyo pesa inaishia makaburini ama inaenda kuwafanyia kazi wananchi wa Kenya? view
  • 4 Mar 2015 in Senate: Muda umepita wa kupiga gumzo ilhali Wakenya wanaendela kuumia. Pesa za Serikali zinavujwa na watu binafsi ilhali Serikali haiwachukulii hatua. Kama hatuwezi kuwahudumia Wakenya kama Maseneta, inafaa tujiuzulu ili pesa ambazo tunalipwa zigharamie miradi ambayo itawasaidia Wakenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus