Ali Wario

Parties & Coalitions

Born

5th May 1970

Post

P. O. Box 10 Bura, Tana

Email

warioali@yahoo.com

Telephone

0721398361

Telephone

0725206089

All parliamentary appearances

Entries 451 to 460 of 612.

  • 5 Nov 2013 in National Assembly: Thank you, hon. Speaker, Sir. You have heard hon. Kamau using unparliamentary language on me, telling me that, that is a lie. Could he withdraw and apologise? The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 5 Nov 2013 in National Assembly: Bw. Spika, nilikuwa mbele ya mheshimiwa kuingia katika Bunge hili. Kwa hivyo, si mara yangu ya kwanza na hawezi kunifundisha Standing Orders . Nimesimama kupinga Hoja hii. Sipingi kwa sababu ninaunga mkono ufisadi au ninataka NCPB ikufe. Ninapinga kwa sababu shida ambayo imepatikana imetokana na NCPB ambayo imesimamia zabuni. Wao ndio wametoa kadarasi. Wakati wamezozana na Erad, Erad wemeenda kortini, NCPB hawajakata rufani hata mara moja mpaka leo. view
  • 5 Nov 2013 in National Assembly: Bw. Spika, nilipoleta hoja ya nidhamu, niliitwa majina mengi ikiwemo kusemekana kuwa nimeleta hoja kupinga, moja, kwa sababu ya ufisadi na pili, kwa sababu ya ukabila. Mimi nimetoka Mkoa wa Pwani, kisha Pwani barani, si baharini kule. Katika hiyo bara, cheo kubwa kabisa tulichonacho katika Serikali ni DC. Ukabila hautanipeleka mahali. Mimi ni kiongozi na ninatoka Bura ambapo kumetoka makabila 42 ya nchi ya Kenya. Siwezi kuleta hoja kwa ajili ya ukabila. Pendekezo la 13 katika ripoti iliyo mbele yetu linasema uchunguzi ufanywe kwa sababu ukame ambao umetangazwa haufai kutangazwa saa hii. Wajibu wa kutangaza ukame kama janga la kitaifa ... view
  • 5 Nov 2013 in National Assembly: Bwana Spika, pendekezo la 13 linasema kwamba uchunguzi ufanywe katika Wizara ya Miradi Spesheli na Wizara ya Kilimo kwa kutangaza ukame. Miaka tisa imepita sasa. Kwa nini ukame ulitangazwa kuwa janga la kitaifa? Wajibu wa kufanya hivyo ni wajibu wa Baraza la Mawaziri na Rais. Kwa nini ripoti haijaletwa hapa? Ripoti hi inatupatia ukweli nusu na uongo nusu. Hatujaambiwa fedha ni za nani. Tumechukua kampuni moja na kujaribu kuihalalisha kwa sababu tunataka kuwaambia Wakenya kwamba hawa ndio wabaya zaidi. Je, wale waliochukuwa zabuni ya kuleta tani zaidi ya 110 wako wapi? Wamefanya nini? Wamelipwa pesa ngapi? Ripoti hii haituelezi hayo. ... view
  • 5 Nov 2013 in National Assembly: Iwapo tutapitisha hii Hoja, kuna pendekezo--- view
  • 5 Nov 2013 in National Assembly: Bwana Spika, hii ni nyumba ambayo inaangaliwa na Wakenya wote, wakubwa kwa wadogo na watoto kwa wazee. Tegemeo lao ni sheria tunazotunga hapa. Bila usawa na haki hadhi ya nyumba hii itateremka. Kuna pendekezo moja kwamba Serikali itoe ruzuku kwa NCPB ili iweze kusimama. Mimi nitaunga hilo mkono ikiwa viongozi wa NCPB watabadilishwa. Baada ya hukumu kutolewa wale waliokuwepo hawakwenda kukata rufaa. Hawakumjulisha Mkuu wa Sheria kwamba kuna tatizo kama hili. Kwa sababu gani? Ni kwa sababu wao pia wana mikono yao ndani ya suala hili. Ikiwa Erad imepoteza robo ya mali ya umma, NCPB itapoteza theluthi tatu ya mali ... view
  • 31 Oct 2013 in National Assembly: Hon. Speaker, I am lost. I thought, through Standing Order 89(3) (d), I tabled a court decree proving that this matter is before a court of law. I am asking for your indulgence, through Standing Order No.1. Is this amendment not a clever way of going round the ruling that I am waiting from you? This is because the purpose of this amendment is to pre-empt the ruling by the court. Do we, first, get a ruling on the concern I raised yesterday and then proceed with the amendment or do we proceed with the amendment and then wait for ... view
  • 31 Oct 2013 in National Assembly: Ahsante sana mhe. Spika. Nasimama kuchangia marekebisho ya Hoja yaliyoko mbele yetu. Tumetoa miezi sita kwa PIC. Kamati hii imeenda na ikatuletea Ripoti. Kwa masikitiko makubwa, imeamua kwamba kampuni fulani isipewe kazi na nyingine ipewe kazi. Baada ya sisi kusema kwamba hii ni kazi ya mahakama, tunaletewa marekebisho ili korti ikiamua kwa manufaa ya National Cereals and Produce Board (NCPB), jambo hili lifanyike. Swala nyeti ni moja. Je, korti itakapoamua kwamba Erad imeshinda, marekebisho haya yatakuwa na maana gani? Kwa nini tunapoteza muda wa Wakenya? Hii ni kwa sababu haya ni masuala ya mahakama. view
  • 31 Oct 2013 in National Assembly: Tunaambiwa kwamba ikiwa korti itatoa hukumu kwa manufaa ya NCPB--- Je, maana ya marekebisho ni gani kama korti haitatoa hukumu? view
  • 31 Oct 2013 in National Assembly: Nguzo tatu za Serikali ni Bunge, Mahakama na Utawala. Bunge linatunga sheria, Utawala unatekeleza sheria na kama kuna ugomvi, Mahakama inatatua huo ugomvi. Leo Bunge litachukua jukumu la utunzi wa sheria, litatoa hukumu kati ya Erad na NCPB--- Naona tunavuka mpaka na tunazungushwa hapa. Wanaopiga hesabu hii wanajua wanafanya nini. Miezi sita, sisi tumetarajia Ripoti ambayo itatupatia mwongozo na walioandika Ripoti hii ndio wanakuja kuikosoa. Ikiwa wenyewe wanaikosoa, sisi tuna wajibu wa kuikataa kwa sababu wenyewe hawana imani nayo. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus