All parliamentary appearances
Entries 441 to 450 of 612.
-
21 Nov 2013 in National Assembly:
Ili sheria hii ambayo tunaitunga isigongane na Katiba, mamlaka ya kutangaza sehemu kuwa national park ipitishwe na Bunge. Isipopitishwa na Bunge hivi ilivyo, inafaa kubadilishwa na haifai kupita hapa ndani. Ukiangalia sehemu ya hatia na faini, inanichekeza. Naona mkono wa wakoloni ndani ya hii sheria. Nasema hivyo kwa sababu kuna wanyama katika kifungu cha (a) ambao ukiwaua, utatoa faini ya Kshs20 milioni au kufungwa milele gerezani. Lakini wale wanyama wakiuwa wewe, utalipwa Kshs1 milioni au Kshs3 milioni. Baina ya hao wanyama na wanadamu, nani anastahili kulipwa Kshs20 milioni? Nikiua ndovu, nitafainiwa Kshs20 milioni au nifungwe milele gerezani.Ndovu akiua mtu, familia ...
view
-
21 Nov 2013 in National Assembly:
Kifungu cha 89(f), kinasema kuwa ukipatwa ukilisha ndani ya uhifadhi ya wanyama, hata kama ni mbuzi kumi, utafainiwa Kshs200,000. Pengine dhamana ya wanyama wako haifiki Kshs200,000. Sheria hii itaumiza wafugaji. Ukisoma ukurasa wa mwisho, hifadhi za wanyama ambazo zinahesabiwa hapo ziko katika sehemu za wafugaji. Ni lazima tutambue kwamba kuna haki baina ya mifugo na wanyama hao. Nikimalizia, juzi, maafisa wangazi za juu katika KWS, ambao wote wanatoka katika sehemu ya wafugaji, walisimamishwa kazi. Lakini kabla ya muda wao wakufutwa kufika, ofisi yao ilibadilishiwa watu wengine. Hiyo ni dhuluma. Sisi ardhi yetu imechukuliwa na KWS na tunataka nafasi za kazi ...
view
-
5 Nov 2013 in National Assembly:
Thank you, hon. Speaker. If I heard the Leader of Majority Party well, he said that the recommendations of this report are very clear and that the name of Joseph Kinyua is not in the report, I will then invite you to read page 12, Recommendation “b”. Has that been deleted? I beg to be informed, hon. Speaker, Sir. Thank you.
view
-
5 Nov 2013 in National Assembly:
Hon. Speaker, Sir, is that the name of Joseph Kinyua?
view
-
5 Nov 2013 in National Assembly:
Asante Mhe. Spika. Ninachukuwa fursa hii kukushukuru. Wahenga walisema kwamba, “Mnyonge kupata haki ni mwenye nguvu kupenda,” Ninasema hivyo kwa sababu nimesimama katika Bunge hili kuchangia Hoja hii. Kulingana na kipengele 89(3)(d) cha Kanuni za Bunge, kwa heshima na taadhima kubwa, uliahidi na kusema kwamba: “Mhe. Wario, nimesikia nitakuja kuamua.” Siku ya kwanza, ya pili, na ya tatu nimekaa kungojea uamuzi kutoka kwa Mhe. Spika. Kwa sikitiko kubwa sikupata uamuzi huo. Leo nimeambiwa kwamba: “Mhe. Ali Wario, huna habari, uamuzi ulishatolewa.” Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo, nimechukua uamuzi wako na wacha niendelee mbele na msafara. Mhe. Spika, ninasema kwamba; tunaambiwa kwamba ...
view
-
5 Nov 2013 in National Assembly:
Wakati walipelekwa kortini, wakili yule hakuenda kupinga ile hukumu.
view
-
5 Nov 2013 in National Assembly:
Hapana, Bw. Spika. Nimesimama kuichangia Hoja hii.
view
-
5 Nov 2013 in National Assembly:
Ninasimama kuichangia Hoja hii. Sijaichangia Hoja hii. Nilisimama kwa jambo la nidhamu na nikachangia marekebisho. Ikiwa kusema kwangu kunawadhuru; kama hamfurahii, nataka--- Sikuichangia Hoja hii.
view
-
5 Nov 2013 in National Assembly:
Hon. Speaker, Sir, I did not contribute. I only contributed to the amendment. I only moved an amendment and I contributed to that amendment. I did not contribute to the main Motion. I only contributed to the amendment. Bw. Spika, nilileta hoja ya nidhamu na nikaleta marekebisho. Nilizungumza kuhusu hayo marekebisho lakini si juu ya Hoja hii.
view
-
5 Nov 2013 in National Assembly:
Bw. Spika, hon. Kamau ananitukana. Neno “uongo” siyo lugha ya Bunge.
view