Amin Deddy Mohamed Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 61 to 67 of 67.

  • 14 Sep 2017 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu Spika. Awali ya yote, naomba kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwenye wingi wa rehema kwa kutujalia afya njema na kutufikisha siku ya leo. Mwenyezi Mungu anaendelea kuitikia dua ya kuliombea Bunge hili kwa kutuongezea hekima na maono kwa ajili ya kuwatumikia Wakenya. Nachukua fursa hii pia kukushukuru wewe binafsi, Naibu Spika, wenye viti Bungeni pamoja na Wabunge wote kwa uteuzi wayo. Mighairi na hayo nachukua fursa hii pia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 14 Sep 2017 in National Assembly: kuwapongeza na kuwashukuru wana Nyali kwa kuamua kwenda kinyume na itikadi na siasa chafu za pesa, vyama na ukabila na badala yake kunichagua mimi kama mgombea huru katika eneo Bunge la Nyali. Nawapongeza pia Wakenya wote waliojitolea na kuchangia katika mkoba wangu wa Kampeni pamoja na ushauri walionipa. Sina la kuwapa ila nawaahidi kuwa nitazidi kuwapigania na kuwakilisha sauti zao katika Bunge la 12. Kwa ufupi, nasema Mungu awabariki wote kwa kuamini kuwa hakuna lisilowezekana mbele ya macho ya Mungu. Fauka na hayo, naomba hili Bunge la 12 liwe kielelezo na tofauti kabisa na Bunge za hapo awali kwa kujadili ... view
  • 14 Sep 2017 in National Assembly: Mhe. Naibu wa Spika, licha ya Hoja zote zilizotajwa majuzi na Rais – Hoja za Kenya na Ukenya ndani yetu – ningelipenda pia kuchukua fursa hii kuomba Bunge hili, chini ya uangalizi wako, katika siku za usoni kuwa makini na kutunga sheria kali dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya. view
  • 14 Sep 2017 in National Assembly: Hakika sisi Wapwani tumeathirika pakubwa na watu wachache wanaojipiga kifua na kujiona kama miungu midogo huku wakiangamiza kizazi chetu. Safari hii tunaujumbe kwa walanguzi wa dawa za kulevya Pwani. Tunasema kama noma, naiwe noma . Wakenya wote ni mashahidi kwamba vijana wetu wengi wameendelea kudhoofisha afya zao kutokana na matumiza ya dawa za kulevya. Dawa za kulevya ni hatari sana kwa usalama wa ustawi wa taifa letu. Vita hivi ni vita vikubwa dhidi ya uagizaji, uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya. Sote tunapaswa kuunga mkono jitihada hizi. Nikimalizia, nihitimishe hotuba yangu kwa kuombea waheshimiwa Wabunge-wenza, pamoja na Wakenya ... view
  • 14 Sep 2017 in National Assembly: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 14 Sep 2017 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika. Ninawakilisha Eneo Bunge la Laikipia Kusini. Nimesimama kwa heshima zote na unyenyekevu kumushukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia nafasi ya utumishi. Ningependa kuwahakikishia ya kwamba nitawawakilisha kikamilifu. Majukumu ambayo wametupatia tunaamini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, tutayatekeleza kikamilifu. Mambo ambayo yako mbele yetu si rahisi. Tunajua kuna shida kwetu kutoka mahali panaitwa Wiyumire, Solio mpaka Umande. Tunajua akina mama walituchagua bila ubaguzi wakijua ya kwamba mizigo ambayo wamekuwa wakibeba kwa miaka yote, na changamoto ambazo ziko pale, tutaweza kuwarahisishia. Ningependa kumpongeza sana Rais kwa sababu aliongea kuhusu mambo ya ugatuzi na kupiga siasa kama mtu mzima. ... view
  • 14 Sep 2017 in National Assembly: kwamba sisi sote ni wana wa Mungu. Tuko hapa kumtumikia na kuhakikisha tumewakilisha watu wetu kikamilifu. Ahsante sana, Mungu awabariki. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus