10 Mar 2020 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika. Kusema kweli, kama wananchi wa Kwale na Pwani kwa jumla, tumesikitishwa sana na kifo cha mwendazake Mheshimiwa Suleiman Dori, ambaye alikuwa ni mpenda kazi, mpenda wenzake na mpenda nchi yake. Mheshimiwa Suleiman Dori, licha ya kuwa alikuwa Mbunge wa Msambweni, alikuwa rafiki wangu wa karibu. Tulizungumza mengi kuhusu maendeleo na kuhusu kazi yetu tunayoifanya na amesaidia sana Wabunge wengi wa kutoka Pwani kwa kuwaonyesha jinsi ambavyo watajifundisha maswala ya Bunge ili waweze kusaidia jamii kwa ujumla. Nataka niwashukuru sana viongozi wote walioweza kufika jana kwa mazishi, ijapokuwa muda ulikuwa mfupi. Familia imeshukuru sana kwa sababu, mwanzo, ...
view
19 Feb 2020 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. I rise to ask the Cabinet Secretary for Education, Science and Technology the following Question. (i) Could the Cabinet Secretary provide a list of all constituencies benefitting from the school feeding programme under the Ministry of Education, and indicate when Kinango Constituency will be considered? The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
19 Feb 2020 in National Assembly:
(ii) Could the Cabinet Secretary also explain the criteria used to allocate and distribute infrastructure funds and explain the amount of funds allocated to schools in Kinango Constituency, noting that these schools have the poorest infrastructure in the region?
view
6 Nov 2019 in National Assembly:
Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. I rise to ask Question No.471/2019 which is directed to the Cabinet Secretary for Transport, Infrastructure, Housing and Urban Development. (i) Could the Cabinet Secretary explain why quarries and other excavations dug during the construction of the Standard Gauge Railway have not been filled up or rehabilitated since the completion of the project, especially those along the railway in Kinango Constituency? (ii) Could the Cabinet Secretary further explain why schools built as compensation have not been furnished with necessary facilities since completion of the railway? (iii) Could the Cabinet Secretary provide details on when ...
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nafikiri utaniongezea dakika moja. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Mboko wa Likoni. Kwanza kabisa, wacha nichukue nafasi hii kupatiana rambirambi zangu kwa familia ya marehemu mwenda zake ambaye alituacha kwa sababu ya ajali iliyotokea pale Likoni.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Kusema ukweli, wafanyi kazi wengi wa feri hawana tajiriba ambayo inatakikana kuhakikisha kwamba wanafanya kazi ile vizuri. Wiki mbili zilizopita kabla ya ajali hii kutokea, feri moja ingegongwa na meli ambayo ilikuwa inapita. Watu wa feri walisema ya kwamba wanajua wanafanya nini na walikuwa tayari kwa lolote. Lakini kusema ukweli, ni Mwenyezi Mungu ambaye aliokoa ajali ile. Tungepoteza watu wengi sana pale Likoni wiki mbili zilizopita. Vile alivyosema mwenzangu, mwaka 1994 tulikuwa na ajali pale Mtongwe ambapo tulipoteza watu wengi sana. Ajali hiyo ilikuwa mita kadhaa na pale ambapo maafisa wa Kenya Navy wanaishi ama wanafanyia mazoezi yao lakini hakuna ...
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Tutalaumu Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Ferry Services lakini wale ambao wako na jukumu la kuhakikisha kwamba wanatetea ama wanaangalia maisha ya binadamu ambao wako katika vitengo vya maji ni maafisa wa Kenya Navy. Ningependa kuomba Waziri wa Usalama na Waziri wa Uchukuzi wachukue jukumu la kukiri makosa yale yaliyofanyika kama yao wala siyo ya wale ambao walikuwa pale. Hivyo ndivyo tutarekebisha mambo nchini mwetu. Hatutawalaumu watu wengine zaidi.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Pia, ningependa kujulisha Bunge hili la Kitaifa kwamba mambo kama haya yakitokea, Serikali haina mipangiliyo yoyote ya kuhakikisha familia ilioachwa inasaidiwa vizuri. Tangu juzi, tunaona kwa runinga familia ya Mariamu ikiwa imekaa pale chini. Wanalia lakini hata hakuna watu wa kuwasaidia kama vile Kenya Red Cross. Hii inaonyesha aibu kubwa kwa upande wa Serikali ya Kenya. Eti tunajivunia Coast Guards ilhali hatuwezi kusaidia wananchi wetu!
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Ningependa kuomba Serikali, kama feri bado zitazidi kutumiwa, iwaajiri life savers. Ni lazima wawe mule kwenye feri. Hakuna mahali duniani palipo na huduma za kuvuka maji ambapo hakuna watu ambao kazi yao ni kuangalia usalama wa wale ambao wanatumia maji yale. Hata kwenye ufuo wa bahari, lazima kuwepo na watu ambao watasaidia ikiwa jambo litatokea.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Kenya Ferry Services inapaswa kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba watu wanatumia feri vizuri. Ikifika jioni ambapo watu wanaenda nyumbani, utawaona watu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view