6 Dec 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
6 Dec 2023 in Senate:
Kwa hivyo, tukienda mapumziko kesho, mimi sijui kama nitaenda Marsabit. Kama watu hao wangepata hizo pesa, wangenunulia familia zao chakula. Watu wetu hawana chakula na wanaendele kuteseka. Sisi tuna shida nyingi sana ingawa tuko katika Serikali moja. Hata ukiwa upande wa Upinzani au Serikali, sisi sote tunahudumia nchi moja, wananchi wetu na familia zetu. Jana Wabunge wa Bunge la Kitaifa walisusia kazi lakini leo wamerudi kwa sababu watalipwa marupurupu yao ya National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF). Mimi naona kama hili Bunge la Seneti tunaonyeshwa kwamba halina maana katika nchi hii. Ni mara ngapi Mawaziri wamekataa kuja hapa wakisema wanaugua, ...
view
6 Dec 2023 in Senate:
Jana niliona maajabu sana katika mtandao wa Twitter na nilishangaa sana. Kuna wageni kutoka Somaliland ambao walikuja kwa Ofisi ya Spika wa Seneti. Mhe. Spika aliwakaribisha na mimi pia nilikuwa hapo. Msimamizi wa Somaliland alisema kuna takriban Wakenya 30,000 wanafanya kazi Hargeisa huko Somaliland. Akaongezea kusema kuna wanakandarasi wa Kenya ambao wamejaa huko. Alieleza kwamba hawana mayai wala kuku huko Somaliland. Mayai na kuku ambao wanakula wanatoka Uropa.
view
6 Dec 2023 in Senate:
Akasema pia majani chai ambayo yangetoka Kenya yaende moja kwa moja hadi Somaliland, yanaenda Uropa na Uturuki ndio irudishwe Somaliland. Hayo majani chai ni ya wakulima wetu ambayo yanapelekwa huko Uropa na Uturuki kisha yanauzwa katika Somaliland. Huyo msimamizi aliiomba Serikali ya Kenya ianzishe huduma za usafiri wa ndege kutoka Nairobi hadi Hargeisa, Somaliland. Hiyo safari itarahisisha maisha ya watu wanaosafiri kikazi kutoka Kenya hadi Somaliland. Wale wanaoishi Somaliland, pia wakaomba huduma ya ndege kati ya Hargeisa na Nairobi.
view
6 Dec 2023 in Senate:
Alizidi kusema ya kwamba imechukua miezi 18 na mpaka sasa, hawajapata huduma za usafiri wa ndege kwenda mpaka Hargeisa. Nakumbuka alisema wanaenda Hargeisa kupitia Djibouti ama Ethiopia na gharama yake ni takriban Dola 1,800.
view
6 Dec 2023 in Senate:
Hiyo biashara ingekuwa ya manufaa kubwa kwa Kenya kuliko Somaliland. Nilishangaa sana kuona Katibu wa Kudumu wa Wizara ya Mambo ya Nje, akijibu kupitia kwa Twitter badala ya kuchukua simu na kusema wamepata hilo ombi na watashughulikia. Alijibu kwa Twitter huku akidhalalisha Bunge la Seneti, akauliza Seneti iko na kazi gani na Spika wa Seneti anaingiliaje haya mambo?
view
6 Dec 2023 in Senate:
Kwa hivyo, tutakaporejelea vikao vya Bunge, nitaleta swali nikitafuta kujua kwa nini hiyo safari ya ndege ya kwenda Hargeisa imechelewa kuanzishwa. Kama wamelalia kazi, waachane na hiyo kazi. Kama wanaweza kufanya hiyo kazi, waifanye na waache Seneti ifanye kazi yake.
view
6 Dec 2023 in Senate:
Kwa hayo machache, Bw. Spika, nashukuru.
view
5 Dec 2023 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. As I was watching YouTube last night, I came to know that Hon. Lawrence Sifuna was dead. What I did not know was that, the gentleman seated over there, the Senator of Nairobi City County, is related to Hon. Lawrence Sifuna. Now I know where his ability comes from. It is genetics. I also thank Sen. (Dr.) Khalwale for bringing this Statement. When I saw the video, I went through history to check what he did during his time in Parliament. I was surprised to know that he was among a very few Members of ...
view
5 Dec 2023 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. As I was watching YouTube last night, I came to know that Hon. Lawrence Sifuna was dead. What I did not know was that, the gentleman seated over there, the Senator of Nairobi City County, is related to Hon. Lawrence Sifuna. Now I know where his ability comes from. It is genetics. I also thank Sen. (Dr.) Khalwale for bringing this Statement. When I saw the video, I went through history to check what he did during his time in Parliament. I was surprised to know that he was among a very few Members of ...
view