22 Mar 2023 in Senate:
Asante sana Bi. Spika wa Muda. Hii Nyumba imerudi kuwa kama ya watoto wadogo wanaopiga kilele. Pande zote mbili ni kama hawakuheshimu. Sen. Cherarkey, upande huu na upande ule mwingine, ni Seneta wa Nairobi. Tafadhali tupa hawa watu nje ili wajue hicho kiti umekikalia vizuri. Kama hautafanya hivyo, hawa watu watakusumbua mpaka kesho.
view
15 Mar 2023 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Wakati Agizo lilikuja kwako lilisimamisha hii Seneti kufanya kazi yake. Leo ningependa kujua, kesho mtu mwingine akileta agizo kama lile la kusema Seneti hii isifanye kazi wala kujadili mambo yoyote, tutafanya vile kweli?
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika nisaidie ili hawa watu wasi---
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika wakati tatizo hili lilitokea, kama Seneta na mzee aliyefanya biashara kwa muda mrefu, niliwatembelea Kiongozi wa Walio Wengi na Kiongozi wa Walio Wachache na kuongea nao. Niliwaeleza kuwa hii nchi inahitaji sisi kama viongozi tufanye kazi. Tulipewa hivi vyeo ili tufanye kazi. Niliwaeleza kuwa wanafaa waketi na waongee ili tuangalie kama tunaweza kutatua hili tatizo. Bw. Spika nilikuja hadi kwenye ofisi yako kuomba hili jambo litatuliwe. Nchi hii ina mambo mengi sana ya kutatuliwa hapa. Kama Mheshimiwa ametoka chama chake na kwenda upande mwingine---
view
15 Mar 2023 in Senate:
Ikiwa hujalazimishwa na umetoka ulipokuwa kwa upendo wako na kutangazia Kenya nzima kuwa umehama kile cheo ulichokuwa nacho, achia wengine wapewe pia wafanye mambo yao. Tumepoteza muda na siku nyingi juu ya mambo haya. Haya ni mambo ambayo hayangefaa kuwa katika Seneti. Seneti si nyumba ndogo ambamo watu huongea mambo ya watoto. Hii ni ‘ Upper House.’ Bw. Spika nakuomba kwa niaba ya wananchi wa Kenya, kwa sababu dunia nzima inatazama haya mambo yote yanayoendelea---
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, sisi ni watu wazima lakini tunabishana kuhusu mambo ambayo hayafai. Ningependa leo - si kesho - ikiwezekana hata saa hii jambo hili litatuliwe. Wengine wetu wamechoka. Niko na Hoja kuhusu bei ya nguvu za umeme. Wananchi wameshindwa kulipia nguvu za umeme. Baadhi ya Maseneta hawajakuwa wiki mbili sasa. Hatuwezi kuendelea hivi. Tafadhali Bw. Spika, nakusihi kwa niaba ya wananchi na kukuomba kwa kuwa leo uko na uwezo. Usipendelee upande mmoja kwa kuwa wewe ni mwamuzi na unaweza kuamua haki, na hakuna atakaye kulaumu. Usiyafuate mambo ya kesho; yamalize leo ili tuendelee na kazi yetu. Shukran.
view
9 Mar 2023 in Senate:
Shukran sana, Bw. Spika. Ninashukuru Kiongozi wa Walio Wengi kwa kuleta Petition hii leo. Hii Petition inazungumzia mambo ya zamani. Mimi nimetoka kaunti inayoitwa Marsabit. Zamani tulikuwa tunaita Northern Frontier District (NFD). Tulifungiwa huko kabisa na Wakoloni na tukaitwa marginalized community . Tukapewa jina ambalo ni kama watu disabled . Baada ya kuitwa marginalized community, Serikali ya Kenya ikapata Uhuru na Rais hayati Jomo Kenyatta akaingia mamlakani. Tuliendelea kufungiwa huko NFD na kuitwa marginalized. Serikali ya hayati Rais Moi ikaingia mamlakani bado tukaitwa marginalized . Serikali ya hayati Kibaki ikatuita bado marginalized . Serikali ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta bado ...
view
9 Mar 2023 in Senate:
. Wakoloni wametusumbua sisi. Saa hii tunapozungumza, ardhi inayoitwa Lake Turkana, watu fulani wazungu wameangalia atlas- map ya dunia, wakajua upepo mzuri uko mahali panaitwa Sarima
view
9 Mar 2023 in Senate:
. Wemekuja na kuchukua ardhi yote. Ardhi kutoka hapa mpaka Nakuru kupitia Nanyuki, Machakos hadi Kajiado, imechukuliwa. Bw. Spika, Warendile ndio wanaoishi Katika eneo Bunge la Laisamis. Malisho ya ngamia, mbuzi na ng’ombe ni kule. Sasa hivi tunavyozungumza, hawa watu wetu
view