David Musila

Born

24th February 1943

Post

P. O. Box 48 Migwani

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

davidmusila@yahoo.com

Email

mwingisouth@parliament.go.ke

Telephone

0733733521

All parliamentary appearances

Entries 1001 to 1010 of 1152.

  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, kama vile nilivyosema hapo awali, ni kweli kuwa kisa hicho cha kusikitisha kilitokea na ningependa kulijulisha Bunge kwamba Jeshi la Kenya lilikuwa likifanya mazoezi katika sehemu hiyo katika miaka ya 1980s na 1990s. Hivi sasa, tumeacha kutumia sehemu hiyo kwa mazoezi. Bw. Naibu Spika, vile ningependa kusema, haswa kwa Mheshimiwa aliyeuliza Swali hili na wengine ambao wanaishi katika sehemu ambazo mazoezi ya jeshi yanafanyika, tunafanya juhudi kubwa kila wakati baada ya mazoezi kutafuta vifaa vyovyote, vikiwemo mabomu, risasi na vyombo vingine; tunaviokota na kuvipeleka kwengine! Lakini, haiwezi kukosa kwamba moja ya mabomu yanaweza kukosa kuonekana. Kwa hivyo, ... view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Kwa hivyo, tunaomba wananchi wajue kwamba vifaa hivi ni hatari. Pia, tunawaomba wanapovipata watueleze ili tuvichukue. Kwa sasa, tumeacha kufanyia mazoezi pale. Tunaendelea kusaka sehemu hizo zote kwa minajili ya kutafuta hivyo vifaa. view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, hilo ni swali la kustaajabisha sana kwa sababu ni jeshi la Kenya ambalo linafanya mazoezi pale. Jeshi la Kenya lina manufaa mengi sana kwa wananchi wa Kenya. Kwa mfano, linatoa ulinzi kamilifu kwa nchi. Hata kama hakuna anachoweza kukubali, mhe. Chachu anapaswa kukubali kwamba Wakenya wanalindwa na majeshi ya Kenya. Hiyo pekee ni faida tosha. Kuna faida nyingi ambazo sitataja wakati huu. view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Jambo la maana ni kwamba jeshi lolote ni lazima lifanye mazoezi. Kwa kuzingatia sheria, Serikali ina uwezo wa kutenga sehemu fulani kuwa za mazoezi katika kifungu 199 cha Sheria zetu. La muhimu ni kwamba mazoezi yakiisha, vifaa vilivyotumika vitolewe na wananchi wajulishwe. Kifungu cha tatu cha sheria zetu, kinasema kwamba wananchi hawaruhusiwi kutangatanga ovyo ovyo katika sehemu zilizotengwa kwa minajili ya mazoezi ya wanajeshi. view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, ningependa kumsahihisha mhe. Abdirahman. Inaitwa “fidia” na si “ridhaa”. Hilo ni swali ambalo uchunguzi ukifanywa na ipatikana kwamba Serikali ilifanya makosa--- Bila shaka tutathibitisha jinsi mambo yalitukia. Pia, tutatekeleza yanayohitajika. Hilo litakuwa ni suala lingine. view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Hata hivyo, kwa wakati huu, jambo la muhimu si fidia bali ni kuhakikisha kwamba wananchi wanalindwa. Sharti waonywe wasikaribie maeneo ambayo yana vifaa hivyo. Wakiviona vifaa hivyo, basi wapige ripoti kwa polisi. Hii ni kwa sababu lazima vifaa hivyo vitapatikana huko. view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, Bw. Wamalwa ni wakili na bila shaka anaelewa mambo haya. Hapo awali nilisema kwamba kijana huyo alichukua bomu hilo na kulipigisha kwenye mwamba. Hicho kitendo kililifanya hilo bomu kulipuka. Hayo mambo yatafikiriwa wakati wake ukifika. Kwa sasa, tunasikitika kwamba mtoto wa miaka 12 aliaga dunia kwa sababu ya mlipuko wa bomu. view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, nimeeleza kwamba baada ya mazoezi yoyote kufanyika, juhudi kubwa hufanywa kuhakikisha kwamba vifaa vyote vilivyotumika vimeokotwa na kurudishwa mahali pake. Lakini kwa sababu sehemu inayofanyiwa mazoezi ni kubwa sana, kuna uwezekano kwamba kifaa kimoja ama viwili vinaweza kusahaulika. Ndiposa tunasema kwamba view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, utakubaliana nami kwamba hiyo si Hoja ya nidhamu bali ni swali. Nimesema kwamba Serikali inafanya mipango kutuma wanajeshi katika sehemu hizo zote kwa minajili ya kuzifagia na kutafuta njia za kuondoa vifaa hivyo vyote. Naomba wananchi washirikiane na wanajeshi wetu wakati huo ukifika ndiposa tuweze kumaliza shida hii kabisa. view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Ahsante, Bw. Naibu wa Spika. Nafikiri tunaelewa ni kwa nini mheshimiwa anafanya hivyo. Hili ni jambo la kusikitisha. Kama nilivyosema, tutachukua makaratasi yale. Sisi tuko tayari kupokea usaidizi na habari zozote ambazo zitatuwezesha kuzifanya sehemu hizo kuwa na usalama zaidi. Kwa hivyo, ninamwomba mheshimiwa kwamba kama ana habari nyingine zozote ambazo zinaweza kutusaidia, afike afisini mwangu ili tuweze kuyazungumzia mambo hayo zaidi. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus