All parliamentary appearances
Entries 11 to 20 of 893.
-
13 Nov 2024 in Senate:
Bw. Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Wakenya wanatazama kwa makini sana yale yanayojiri katika Bunge hili. Jana katika vyombo vya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate.
view
-
13 Nov 2024 in Senate:
habari tuliona viongozi shupavu wa Seneti wakitetea kaunti ili fedha siziwe chini ya Kshs400 bilioni. Haiwezekani kuwalisha mamba na baadaye watule sisi. Haiwezekani tukeshe kila kuchao tukitetea wananchi wa kaunti zetu ili wapate pesa ilhali kuna viongozi ambao wana dhana kwamba sisi ni kama wanaosukuma rukwama kwa niaba ya watu wetu. Hatutakubali. Sen. Dullo amesema kwamba sekta ya afya imedorora. Wengine hapa wametuambia kwamba sekta za kilimo na elimu zimedorora, ilihali tukiita viongozi hao katika kamati zetu hawaji. Wanajipiga vifua na kubwata maneno yasiyoeleweka. Wakati umefika tuonane jicho kwa jicho. Kule mashinani, tunasema mundu khu mundu .
view
-
13 Nov 2024 in Senate:
Bw. Spika, haitawezeka kuwa Wakenya ambao wanadai kila siku ushuru unapanda lakini unaporudi katika mikono ya magavana, wao ni kufurahia na tunapowaita wanasema wako katika safari za ng’ambo. Mimi najua ng’ambo ni sayuni peke yake. Iwapo wanataka kwenda sayuni, tuonane baadaye. Kunao wanaohudumia Wakenya na ni lazima waje wabebe misalaba yao na kwa vinywa vyao wakiri dhambi zao. Iwapo wana makosa, lazima wabebwe hobela hobela na kuwekwa korokoroni.
view
-
13 Nov 2024 in Senate:
Naambia magavana popote walipo kwamba tunafungua ukurasa mpya wa ugatuzi Kenya hii. Kama hawanioni wataambiwa tuliyoyasema. Unapopewa pesa nyingi, uwajibikaji ni wa hali ya juu. Tutawaandama kushoto na kulia, kwenye handaki na mlimani, kote tutafika ili ugatuzi--- Sisi ni wasanii wa nyimbo za mavoka, halmashauri tunasema, “tutaanguka na wao”. Tukishaanguka nao, “ tutafinish kumalo ”. Hiyo ndiyo lugha vijana mashinani wanaelewa. Kwamba ni lazima ugatuzi ufanye kazi na magavana wawajibike. Ndugu yangu wa Migori, ni lazima tufanye kazi.
view
-
13 Nov 2024 in Senate:
Asante.
view
-
22 Oct 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I beg to lay the following Paper on the Table of the Senate today, 22nd October, 2024- Report of the Mediation Committee on The Sugar Bill (National Assembly Bills No.34 of 2022). Thank you.
view
-
22 Oct 2024 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
-
22 Oct 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I beg to give notice of the following Motion- THAT, the Senate adopts the Report of the Mediation Committee on the Sugar Bill (National Assembly Bills No.34 of 2022), laid on the Table of the Senate on Tuesday, 22nd October, 2024; and further that pursuant to Article 113(2) of the Constitution and Standing Order No.167(3) of the Senate, approves the mediated version of the Bill. Thank you.
view
-
22 Oct 2024 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Ripoti ya Seneti kuhusu makadirio ya fedha ambayo tumeisoma hivi sasa katika Seneti. Muda mchache uliopita, niliuliza maswali hususan kandarasi za madaktari mashinani, malipo ya madaktari mashinani na mazingira ambayo madaktari wanafanya kazi katika Kaunti ya Bungoma. Nilipouliza maswali haya, misururu ya maswali yalichipuka kutoka kaunti mbalimbali humu Kenya, ikiwemo kwamba madaktari mashinani Kenya nzima, kwa zaidi ya miezi kumi hawajapata marupurupu yao. Leo nimeona kiini cha shida za madaktari mashinani. Kuna viongozi katika jumba fulani hapa Kenya ambao wanadhani wana uwezo wa kuhujumu, kuwatesa na kuwagandamiza madaktari mashinani kwamba hawalipi ushuru na hakuna ...
view
-
22 Oct 2024 in Senate:
tulivyotoa juzi kwamba Gavana wa Isiolo akamatwe na kuletwa mzimamzima ili kujibu maswala ya uwajibikaji. Bi. Spika wa Muda, miundo mbinu kama barabara katika nchi ya Kenya zinahitaji fedha. Hatuwezi kusema magavana na viongozi wa kata, Members of County Assemblies(MCAs) wachukue jembe na vifaa mbalimbali waende kutengeneza barabara. Lazima Serikali ihakikishe mabilioni ya pesa wanayopunguza kutoka mapendekezo tuliyopeana ya zaidi ya Shilingi 400 bilioni zitolewe ili tujenge barabara na vivukio ili Wakenya waweze kufurahia matokeo ya jasho lao. Nikimalizia, Wakenya waliandamana na kuleta bugdha katika baraste na nchi nzima wakitaka uwajibikaji, utendakazi na uwazi. Kama Seneti kazi yetu ni kulinda ...
view