Davis Wafula Nakitare

Born

7th May 1943

Post

P. O. Box 126 Endebess

Email

nakitare@africaonline.co.ke

Telephone

0722489317

Telephone

0735669729

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 682.

  • 1 Aug 2023 in Senate: For my colleague teachers, I know we are suffering servants in this country but let us not give up. There is always a window of hope and we will strive to ensure that the rules of the game in the Teachers Service Commission (TSC) and the Government are favourable for teachers to be promoted and to equally enjoy terms of service like any other civil servant in this country. view
  • 1 Aug 2023 in Senate: For those few remarks, I thank you. view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Asante sana, Bw. Spika, kwa nafasi hii kwanza kuwapigia shangwe na kongole wanariadha wetu kwa matokeo ambayo yametufurahisha na kuwatia moyo wengi ambao wana azma ya kuleta taji au mataji katika nchi ya Kenya. Sen. Cherarkey ametaja kwamba ako talanta adimu ya kuchana mbuga usiku kama wanyama wa pori. Ni vyema kwamba nchi hii iweze kuwekeza kwa talanta aina hio, kwa sababu, inaweza epusha madhara yanayodhihirika katika barasi za nchi ya Kenya zinazoonekana kwa sababu ya maandamano ya kubeba ala za matumishi ya jikoni. Mheshimiwa Spika, zaidi ya hayo--- view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika. Anayotaja Kiongozi wa Wengi husema aisifuye mvua imemnyea. Kenya tunaye mwanabondia Wanyonyi ambaye siku kadhaa zilizopita, alikabiliana na mhasimu wake Madonga Nguvu Kazi, ngumi iliyozaliwa Ukraine. Alicharazwa makonde, masumbwi na nguvu za itikadi za Bungoma na maombezi ya Yesu wa Tongaren. view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Jambo la kushangaza, Wanyonyi hakupewa heko wala kushukuriwa. Lakini kwenye vyombo vya habari, tunaona wale ambao wana tabia mbovu na makosa ambayo hayastahili kuwekwa kwenye runinga, wanapewa mwezi mzima Kenya ikijadili vitu ambavyo havileti heshima katika nchi. Tunaomba kama Bunge la Seneti vilevile, tuhakikishe vyombo vya habari vinawapa kipao mbele wanariadha na viongozi ama wachapakazi nchini ambao matendo, matamshi, maisha na hulka zao zinaashiria uzito na kwamba wao wako katika jitihada za kuboresha nchi ya Kenya. view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Kwa niaba ya wanabondia nchini, ninampa heko Wanyonyi kwa kudhibiti shinikizo za nchi jirani kwamba hatuna nguvu wala uwezo, na kwamba tuekeze katika mchezo wa bondia hapa Kenya. view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika. view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Jambo tunayozungumzia sasa inaweka Mawaziri katikati ya jiwe na pahali pagumu. Yule ambaye aliwateua na anawaamini kwa uchapakazi na uadhilifu wao ameona kwa hekima yake kuwapa nafasi kusafiri naye katika nchi za ng’ambo kutetea nafasi na hadhi ya nchi ya Kenya na mustakabadhi wa Wizara zao na nchi wanayokwenda. view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Hapa sisi kama wawakilishi na watumwa wa wapigaji kura, vile vile tunadai wakuje hapa kutupa majibu yao. Ni kama shingo kuuliza kichwa: “Mbona hautumiki kumeza chakula unachotafuna?” view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Bw. Spika, naomba kwamba Bunge la Seneti na wachapakazi wake wawe na udiplomasia wa mapema, kujadili ratiba na mipangilio kwa mapema. Vile vile Mawaziri na wasaidizi wao wawe na mawasiliano ya karibu na Bunge la Seneti ili mipangilio yao isilete aibu mbele ya Wakenya. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus