All parliamentary appearances
Entries 141 to 150 of 186.
-
18 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, ninaomba kujibu. (a) Sina habari kwamba kuna jamii ambazo zilitengwa na hazisajiliwa na kupatiwa vitambulisho. Ni haki ya kila Mkenya kusajiliwa na Serikali anapotoa ombi la kufanya hivyo. (b) Serikali imechukua hatua zifuatazo kuhakikisha ya kwamba jamii za kutoka maeneo kame zimesajiliwa:- (i) Kupatiana fomu na vifaa vya kusajili katika maeneo haya. (ii) Kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kujisajili mara tu wanapofikisha umri wa miaka 18. (iii) Kusambaza huduma ya usajili hadi mashinani, yaani tarafa, ili kufikia watu wote wanaohitaji kusajiliwa.
view
-
18 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika maelezo yamekuwa mengi mpaka maswali yamepotea. Hata hivyo, ningependa kumwunga mkono mhe. Leshomo kwamba sehemu kame, kwa sababu ya ukubwa wake, wananchi kwa kweli wana shida kupata vitambulisho. Lakini kama nilivyosema hapo awali ni kwamba tumetoa fomu hadi tarafa. Siku hizi tarafa ziko karibu sana na wananchi. Kutoka Januari, 2010 hadi Juni, 2010, tumeandikisha watu 2,975 huko Samburu. Kati ya watu hawa, tuna vitambulisho 616 ambavyo havijachukuliwa. Kwa hivyo, tunamwomba mhe. Leshomo atusaidie kwa kuwauliza wale ambao hawajachukuwa vitambulisho vyao kufanya hivyo.
view
-
18 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, tumejaribu kuomba pesa zaidi siyo tu kwa ajili ya kununua mafuta lakini pia kwa magari. Tungekuwa na magari ya kutosha, sehemu hizi zingepata huduma ya kutosha kwa njia rahisi zaidi kwa sababu tungefanya mobile registration. Hii inamaanisha kwamba tungewatembelea wananchi kule vijijini. Ni matarajio yetu kwamba huduma zitasambazwa lakini kwa sasa, kila wilaya na tarafa zinatoa huduma hizi.
view
-
18 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, ijapokuwa walimu wakuu hawajaandikishwa kirasmi kama maofisa wa kusajili watu, bado tunawatumia. Sisi tunawatumia walimu wakuu wa shule za msingi na upili katika shughuli ya kutoa vyeti vya kuzaliwa. Lakini bado hawajaandikishwa kama maofisa. Tunawatumia wao pamoja na machifu.
view
-
18 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, kwa sasa hivi sijui kama mwalimu mkuu wa shule ya upili anashirikiana na wale maafisa wa kusajili watu kama ilivyo katika sehemu nyingine. Hii inategemea idadi ya watoto. Kama wako na hiyo shida, basi wawe wanawasiliana. Tumesisitiza hii na kazi hiyo inafanywa. Lakini kuhusu Lodwar, sijui vile inavyoendelea kwa sasa.
view
-
18 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, kama nilivyosema hapo awali, mipango ipo isipokuwa tu upungufu wa vitu kama mafuta na magari. Kama nilivyosema, tumeomba Wizara ya Fedha itupatie rasilmali ya kutosha ili tutoe huduma hii. Lakini ningetaka kuwaomba wenzangu pia kwamba ikiwezekana watenge pesa za hazina ya Constituencies Development Fund (CDF) ambazo zitatuwezesha kununua mafuta.
view
-
18 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, huo ni mfano ambao nilikuwa nimetoa lakini kama Mbunge anaweza kutoa pesa kutoka kwa mfuko wake pia ingesaidia.
view
-
18 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, sijui sehemu ambayo inachukua miezi sita kupata kitambulisho kwa sababu hapa Nairobi inachukua siku 18. Maeneo ambayo yako nje ya Nairobi isipokuwa zile sehemu kavu huchukua siku 28. Zile sehemu za mipakana kwa sababu ya ukaguzi wa hapa na pale, huchukua siku 38 kupata kitambulisho. Lakini ikiwa mhe. Mbunge anajua pahali ambapo pana shida hiyo anaweza kuja ofisini na tutarekebisha.
view
-
18 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, Swali lililoulizwa na mhe. Mbunge kama Wizara tumejaribu kulijibu. Lakini kuna sehemu ambazo pengine ziko na shida maalum. Nimesema ya kwamba tumeomba pesa ili tuongeze magari na mafuta. Pia, tunatumia maafisa wa utawala na hata walimu wakuu kuhakikisha kwamba tunawasajili wale ambao hawajapata vitambulisho kwa haraka iwezekanavyo. Kwa hivyo, kama Turkana ambayo naifahamu sana iko na shida hiyo, nafikiri itabidi kuongeza maofisa. Nikirudi ofisini, nitafanya mpango maalum ili tupeleke maofisa zaidi ili hao mamia ya watu ambao wako huko wasajiliwe.
view
-
18 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, tulipata dawa yake. Machifu wakishirikiana na manaibu wao wanaweza kuwafikia wananchi kwa njia iliyo bora na rahisi zaidi.
view