Franklin Bett

Parties & Coalitions

Full name

Franklin Kipng'etich Bett

Born

23rd March 1953

Post

P. O. Box 2181 Kericho

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

bureti@parliament.go.ke

Telephone

0721700797

Telephone

052 21200

All parliamentary appearances

Entries 241 to 250 of 1050.

  • 23 Nov 2011 in National Assembly: Mr. Speaker, Sir, I have already indicated that the design which was done did not anticipate the sort of earth work which was found out on the ground and the availability of the materials which were found not to be on site. There was also the availability of materials like fuel and I want to indicate that some of the changes were made because the design did not anticipate the amount of earth work which we underwent. view
  • 17 Nov 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Naibu Spika wa Muda, ni ukweli Rais alizindua ujenzi wa barabara katika eneo hilo. Hata hivyo, Bw. Kutuny ana haki ya kuuliza Swali lake hapa Bungeni. Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba kujibu. (a) Wizara yangu haijaweka lami barabara mpya katika eneo la Cherang’any mwaka huu. Hata hivyo, kupitia Kenya Rural Roads Authority (KeRRA), tumetoa kandarasi ya kujenga upya barabara ya Eldoret-Ziwa-Kachibora (D328) na Kachibora- Moi’s Bridge (D330/E334). Vile vile, kupitia Kenya National Highways Authority (KeNHA), Serikali imetenga Kshs160 million kugharamia ukarabati wa barabara ya Kitale-Sibanga (C48). (b) Kupitia Kamati ya Barabara ya Eneo Bunge la Cherang’any (CRC), ... view
  • 17 Nov 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ni kweli kwamba tumetoa kandarasi Sibanga, Kitale, na Chepkoilel mpaka Kachibora. Ni kweli kwamba kuna sehemu kutoka Kachibora hadi Sibanga ambayo imebaki. Ningetaka kuihakikishia Bunge hili kwamba, hatuwezi kuiwacha sehemu hiyo kwa sababu ni barabara moja hadi Kitale. Pesa ambazo tuko nazo zinatosha kutengeneza barabara kutoka Sibanga hadi Kitale. Tukipata pesa msimu ujao, tutamaliza kutengeneza barabara hiyo kutoka Sibanga hadi Kachibora. view
  • 17 Nov 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ninafahamu kwamba mvua imeleta taharuki katika sehemu ya Mombasa na kuharibu barabara. Ningetaka kulihakikishia Bunge hili kwamba jambo hilo limenifikia na nimeamuru maofisa wangu waziangalie barabara hizo. Muda si muda, nitakuwa na ripoti kuhusu Kaunti ya Mombasa. view
  • 17 Nov 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaamini kwamba mheshimiwa Mbunge anataka barabara hiyo irekebishwe. Kusema kweli, hilo ni Swali tofauti na Swali ambalo linajibu. Ningemwomba Mheshimiwa Mbunge alete Swali bungeni la kipekee ambalo linahusu barabara hiyo ili nitafute jibu ambalo litamfaa kwa sababu yeye ni mwanaume tosha! view
  • 17 Nov 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, mheshimiwa Mbunge ametumia maneno makubwa makubwa na mimi sielewi kama ni Kiarabu, Kiswahili au Sheng. view
  • 17 Nov 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, sijasikia mazungumzo kutoka kwa--- view
  • 17 Nov 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaamini kwamba vyombo hivi vinaogopa Kiswahili sanifu kutoka kwa jamaa hawa wakubwa wakubwa pale. view
  • 17 Nov 2011 in National Assembly: Tunatoa kandarasi kutokana na matangazo kuwa tuko na kazi fulani. Hii inafanyika kwa kutumia taratibu za kutosha ambazo zimewekwa. Hatuwezi kupeana kandarasi kwa njia ya ulegevu au kwa kuonea wengine. Jambo hilo haliwezekani kufuatana na sheria iliyoko katika Wizara yangu. Hatuwezi kuenda kinyume cha sheria tulizoziweka. view
  • 17 Nov 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa Bajeti hii ya Serikali, hatujatenga fedha za kugharamia barabara ambayo mheshimiwa amesema. Lakini tunaitengeneza barabara kutoka Kisumu, Kakamega, Webuye hadi Kitale. Tunaichora upya barabara kutoka Kitale kuelekea Makutano mpaka Lokichogio kama vile mhe. Ethuro alivyosema. Mambo hayo yanaendelea kupangwa lakini wakati huu, hatujatenga fedha za kugharamia barabara ambayo mhe. Wamalwa ameuliza. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus