All parliamentary appearances
Entries 1521 to 1530 of 1711.
-
28 Nov 2013 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Chairman, Sir, I think that is very much in order. That was the intention I had.
view
-
27 Nov 2013 in National Assembly:
Hon. Speaker, Sir, I spoke on this Bill.
view
-
20 Nov 2013 in National Assembly:
Hon. Speaker, I beg to give notice of the following Motion:- THAT, aware that there are many talents amongst the youth of this country; having noted that these talents have been severally displayed through various inventions and innovations by the youth in platforms such as the Science Congress and the Annual Youth Innovation Week; concerned that most of these discoveries do not go beyond making sensational newspaper and electronic media stories; noting that most of these innovations are aimed at addressing the problems that afflict us as Kenyans on a daily basis; further concerned that there is inadequate enabling legislation ...
view
-
20 Nov 2013 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nimesimama kupinga Hoja hii kwa sababu Serikali ama chama kilio na wengi ama wachache kina nafasi ya kuleta miswada na ajenda zao Bungeni Jumanne, Jumatano saa nane na pia Alhamisi. Wabunge wengi wana miswada tofauti ambayo wangependa kupendekeza. Kutokana na Katiba mpya, Bunge hili halifai tu kupatiwa ajenda na upande wa Serikali. Tunafaa kuwa na nafasi ya kuweza kuwasilisha matakwa na jumbe kutoka kwa wale ambao tunawaakilisha, na Jumatano asubuhi tunakuwa na mwanya mwafaka. Ninapenda kupinga kwa sababu wakati huu ndio tunapata nafasi ya kuzungumza kwa sababu mara nyingi wakati ule mwingine hatupati nafasi. Utakuta ...
view
-
20 Nov 2013 in National Assembly:
Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Nimepatiwa nafasi na mwenzangu, Mhe. Bi. Regina Muia nichangie Mswada huu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
-
20 Nov 2013 in National Assembly:
Nasimama kuunga mkono Mswada huu kwa sababu watu wengi sana wameathirika kwa ajali za barabarani. Kuna watu wengi sana ambao wamelemaa na maisha yao yakabadilika kwa sababu ya ajali ya barabarani. Kwa hivyo, ni jukumu letu sisi Wabunge, sio tu kutambua ni ulemavu upi ama ni kiungo kipi kimeathirika bali tuangalie kwa undani zaidi vile ambavyo watu ambao wameathirika wanaweza kujumuishwa katika ujenzi wa nchi hii. Wengi wao hawawezi kutekeleza majukumu waliokuwa wakitekeleza kwa sababu ya ulemavu. Kwa kweli wahenga walisema kwamba ajali haina kinga lakini utakuta kwamba mara nyingi ajali hizi zinatendeka kwa sababu madereva wetu wamekosa kuzingatia zile ...
view
-
20 Nov 2013 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia mapendekezo ambayo yako katika Mswada huu, ningependa kuangazia kwamba ni muhimu yule mkurugenzi wa matibabu wa uma pia aweze kushirikiana na baraza la kitaifa kuhusu watu walemavu katika kutambua aina zingine za ulemavu ambazo hazijatajwa katika vipengele vya Mswada huu. Hilo ni jambo muhimu kwa sababu hili jopo limekuwa na uzoefu wa kazi wa kuhakikisha kwamba maswala ambao pengine hayaangaziwi, yanaangaziwa. Sio eti tuu kutoka kwa mtazamo wa afya bali pia katika mtazamo wa kijamii na mtazamo wa haki za kibinadamu. Pia tuangazie, kwa mfano vile ambavyo kumesemwa hapo awali, wale vijana ambao watapata ...
view
-
20 Nov 2013 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, pia nimeshangaa kwa sababu Mswada huu, hata kama ni mzuri kiasi kile, haujagusia kule kuathirika kwa ngozi; unajua kwamba ngozi ni kiungo kikubwa sana cha mwili. Ni asilimia ishirini ya miili yetu. Kwa hivyo, nafikiria pia kunafaa kuwa na vipengele ambavyo vinazungumzia vile ambavyo ngozi inaweza pia kuathirika.
view
-
20 Nov 2013 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, pia vile mwenzangu alivyosema nafikiri kiwango cha Kshs.3 million ni cha chini sana. Kama umepoteza viungo vya mwili wako, kama huwezi kufanya kazi, kama huwezi kuhudhuria shule, basi nafikiri lazima tuongeze hizi fedha pengine kuwa Kshs5 million ama Kshs.6 million ndiposa uweze kujimudu. Ni vizuri sana katika sheria hii tuweze kuwa na vipengele ambavyo vitawasaidia waathiriwa kufahamu jinsi ya kupata hizi fedha. Kwa kweli, watu wanaweza kupata uamuzi wa korti lakini tunaona kwamba kuna kule kuchelewa. Wakati mwingine utakuta kwamba kuna matapeli. Watu wanachukua hizi hela na wanaziweka katika mabenki ili wapate riba na ilhali ...
view
-
20 Nov 2013 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, nikimaliza nasema kwamba lazima tuangazie kwamba hizi hela ziongezwe na pia kuwe na mikakati ya kuhakikisha kwamba tunaangazia sio tu ulemavu wa viungo lakini vile ambavyo tunaweza kujizatiti katika jamii.
view