All parliamentary appearances
Entries 1581 to 1590 of 1711.
-
2 Oct 2013 in National Assembly:
On a point of order, hon. Deputy Speaker. I wish to raise a point of order with regard to the way the Motions before the House are drafted. I know that they are ending with the same statement that we have been against; urging the Government to do something. I thought there was a kind of a directive from the Speaker that Motions should be saying that “this House resolves”, so that it is a process of the House. I just wanted to raise that.
view
-
2 Oct 2013 in National Assembly:
Thank you, hon. Deputy Speaker. I rise to support the nominee, Mr. James Maina Muhoro because I have worked with this gentleman. Before I came to this House, I was an advisor to the Prime Minister on Special Interest Group and I worked with Mr. Muhoro in the office. I can attest that he is reliable, honest, and very competent as an administrator. It is somebody we depended on very much in the office. Let us not judge this issue based on ethnicity. The National Police Service Commission is chaired by one, Mr. John Kavuludi and through their decision they ...
view
-
26 Sep 2013 in National Assembly:
Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuunga mkono Hoja hii kwa sababu wakulima wetu wataweza kujimudu kwa sababu ya hela watakazopata kutokana na mauzo ya maziwa. Kule ambako nimezaliwa – eneo Bunge la Githunguri – wakulima wanaweza kuzalisha maziwa mengi zaidi ya wakulima katika eneo nzima la Bonde la Ufa. Hilo limekuwa jambo zuri sana kwa sababu ukiangalia mashamba ambayo wako nayo wakulima hao, ni madogo sana kuweza kufanya kilimo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
-
26 Sep 2013 in National Assembly:
kwa kiwango kikubwa. Kwa hivyo, litakuwa jambo la busara kuongeza bei ya maziwa yanayonunuliwa moja kwa moja kutoka kwa wakulima, ama maziwa yanayochukuliwa kutoka kwenye vyama vya maziwa ama kwenye barabara.
view
-
26 Sep 2013 in National Assembly:
Kwa sababu ya ufukara na ukosefu wa ajira, kilimo cha maziwa ni muhimu sana kwa wafugaji kule mashinani. Utaona kwamba kila mmoja wa wazee wetu ameachwa na ng’ombe mmoja ama wawili, na anaweza kupata riziki yake ya kila siku. Kwa hivyo, ni vizuri kuongeza bei ya maziwa ili wazee wetu na jamii zinazoishi kule mashinani, ambao ndizo nyingi; ziweze kupata fedha zitakazoziwezesha kukimu mahitaji yao ya kila siku.
view
-
26 Sep 2013 in National Assembly:
Mhe Spika wa Muda, hili ni jambo muhimu kwa sababu tunajua kwamba bei ya maisha imeenda juu mno, na pia kwamba kwa sababu ya ile sheria ya VAT ambayo tulipitisha hapa, watu sasa wanaona ni vigumu sana kujimudu. Hata tumeona wale wakulima wa kule Gatundu wakilalamika kwamba bei ya chakula cha mifugo imeongezeka sana, na baina ya mifugo hawa kuna ng’ombe. Bei ya chakula imeongezeka lakini bei ya maziwa ambayo wakulima huuza imebaki chini. Kwa hivyo, ningependa sana kuunga mkono ndiposa pia wao waweze kuhakikisha kwamba hiyo bei haiwaathiri.
view
-
26 Sep 2013 in National Assembly:
Pia, maziwa yakitoka shambani yanaweza kufanyiwa mambo mengi sana. Kuna siagi inayotolewa kwa maziwa. Ukiangalia ile gharama ya kupeleka maziwa hadi dukani inamfanya mkulima asiweze kupata pesa zake. Mwuuzaji wa maziwa anapata kama Kshs 100 kutokana na maziwa kwa sababu anauza bidhaa nyingine zinazotoka kwa maziwa. Ni jambo la kusikitisha kama wakulima wetu wataendelea kulipwa bei ile ile ya chini.
view
-
26 Sep 2013 in National Assembly:
Mhe Spika wa Muda, tunajua kwamba tukiongeza bei ya maziwa litakuwa ni jambo zuri kwa sababu itawafanya watu waweze kutoa maziwa kwa wingi. Watu watukunywa maziwa kwa wingi na kuwa na afya nzuri. Pia watu watapata madini na vitamini ambazo zitawasaidia kuwa Wakenya wa afya nzuri. Taifa ambalo linakula vyema pia linaweza kufanya kazi bora na uchumi wetu utaweza kuimarika.
view
-
26 Sep 2013 in National Assembly:
Mhe Spika wa Muda, nikimalizia nina kasheshe kidogo kwa sababu hivi karibuni tumeweza kuona kwamba makampuni madogo ya maziwa yameweza kununuliwa na makampuni makubwa, na hivyo basi inaonyesha kwamba soko la maziwa linamilikiwa na watu wachache. Ukiangalia sana utaona tuna New KCC na sasa Brookside kama makapuni ya maziwa yenye uwezo; hili ni jambo ambalo linanitia kiwewe. Katika ile kampuni ambayo inaitwa Githunguri Dairy kule ambako natoka kuna msukumano. Hii itafanya wakulima wasiwe na masoko mengi ya kuuza maziwa yao. Lakini nafikiri afueni itatoka kwa kampuni ya Serikali ambayo inaitwa New KCC, kama vile ambavyo tuna ile tume ya kawi, ...
view
-
26 Sep 2013 in National Assembly:
Tungependa kuona Serikali ikiingilia kati ndiposa New KCC iwe kama National Oil Corporation of Kenya. New KCC ikiwa hivi itaweza kuhakikisha kwamba makampuni ya maziwa kama Brookside yakiongeza bei yao nayo inawaongezea wakulima bei ya maziwa na kuhakikisha kwamba wakulima wanapata pesa zao vizuri, wanalipwa kwa njia ya haki na kwa wakati ufaao.
view