Isaac Maigua Mwaura

Parties & Coalitions

Born

1982

Email

mwaura.isa@gmail.com

Web

www.isaacmwaura.com/

Telephone

0721864949

Telephone

0733864949

Link

@MwauraIsaac1 on Twitter

All parliamentary appearances

Entries 1591 to 1600 of 1711.

  • 26 Sep 2013 in National Assembly: Mhe Spika wa Muda, naomba kuunga mkono. view
  • 25 Sep 2013 in National Assembly: Hon. Deputy Speaker there are very many good provisions in this Bill. For example, there was a provision about ensuring that terrorism does not gain foot through financing. I was quite disappointed by that tax although it was anchored on railway development. In my opinion, it ought to have been different from what was proposed. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 25 Sep 2013 in National Assembly: We seem to be looking for money for the poor. Even if they were to come together, as hon. Gikaria has said, in co-operatives, where people are making a largesse, I think that is where we should have taxed most. My disappointment is because I witnessed in this House today Members who come through party listing and demean fellow Members. I do not think we are just an addendum to this House. view
  • 19 Sep 2013 in National Assembly: Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninaanza kwa kushangaa kwamba Wabunge 196 wanaweza kuwa katika kikao cha kumfukuza mbali makamu wa kiongozi wa wachache ilhali tukizungumzia maneno ambayo yanawahusu Wakenya, tunakuwa wachache hata mambo ya tyrany of numbers hayapo. Kwa hivyo, ni jambo la kufedhehesha sana kuona kwamba mambo ambayo tunafaa kuyazingatia hayapigiwi upato vizuri. view
  • 19 Sep 2013 in National Assembly: Jambo la pili, katika Hoja kama hizi, ingekuwa muhimu kama Bunge lingehakikisha kwamba Miswada inanakiliwa wa Kiswahili ndiposa Wabunge waweze kuwazungumzia Wakenya kwa lugha ambayo sasa ni ya kitaifa. Fauka ya hayo, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu unahakikisha kwamba Wakenya wataweza kulipa kodi kwa njia sawia. Tunaona kwamba kutokana na vile vipengele vimependekezwa hapa, itakuwa ni rahisi kwa Serikali kupata ushuru kutokana na kampuni mbalimbali ambazo kwa muda zimekuwa zikikwepa kulipa ushuru na hususan kwamba wale ambao watakuwa wakikwepa kulipa kodi watakuwa wakichukuliwa hatua, hata kama wao ni meneja au wakurugenzi wa makampuni makubwa. The electronic version of the ... view
  • 19 Sep 2013 in National Assembly: Pia, kuna jambo ambalo linashangaza katika kipengele kimoja. Wakenya wana uzoefu wa kutafuta jinsi ya kujiimarisha kupitia mbinu kama vile Charity Sweepstake ama kubonyeza. Huu Mswada unasema kwamba ukibonyeza na ushinde, ni lazima ile kampuni ilipe kiasi fulani cha hizo pesa na pia wewe ambaye umeshinda, ulipe. Tunafaa kuwahurumia Wakenya kwa sababu wakilipa kodi kwa Serikali ilhali wenyewe pia wametumia hela kutafuta hiyo bahati na sibu, hili litakuwa ni jambo ambalo hawatalipendelea kwa kweli. Pia, huu Mswada unahakikisha kwamba ile Benki ya Afrika Mashariki imetiliwa maanani kama benki ya IMF na Benki Kuu ya Dunia. Hili ni jambo la kupigiwa ... view
  • 19 Sep 2013 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ninashangaa kuona kwamba Mswada huu umependekeza kwamba asilimia 1.5 ya pesa ambazo Wakenya wanatuma kutoka nje ya nchi na mahali kwingi ambako wamekwenda kujitafutia riziki, zitozwe kodi. Pia, zile bidhaa za kinyumbani, kwa mfano, kama zimetolewa ngambo hususan na watu ambao wanarudi kutoka mataifa ya kigeni, zinafaa kutozwa kodi. Hili si jambo la kusifiwa. Wakenya wanatuma karibu Kshs1 billioni kila mwaka kuwasaidia wenzao ambao wamewawacha hapa wakienda kutafuta riziki kwingine na kutoza hizi pesa kodi kama vile ambavyo nimeelewa, basi ninafikiri hili si jambo ambalo litaweza kupigiwa upato. Pia, ile asilimia 10 ya kodi ambayo ... view
  • 19 Sep 2013 in National Assembly: Ni jambo pia la kuimarisha moyo kuona kwamba hii sheria inasema kuwa kama mwaajiri anaweza kulipa bima kwa wafanyikazi wake, basi ataweza kupatiwa afueni kupitia mpango wa kodi. Hili ni jambo nzuri sana kwa sababu wafanyikazi wengi wamelemazwa katika shughuli za kikazi. Hilo jambo litahakikisha kwamba waajiri wengi wanatafuta bima kwa wale ambao wanawafanyia kazi. Huu Mswada pia unaweza kutusaidia sana kupunguza ugaidi kwa sababu unaharamisha zile mbinu ambazo zinaweza kutumiwa kutafuta hela za kufadhili shughuli za kigaidi. Pia, haitakuwa rahisi kwa watu kusafirisha fedha ambazo wamepata kutokana na biashara haramu. Kwa mfano, kuuza mihadarati. Hilo ni jambo ambalo limeangaziwa. view
  • 19 Sep 2013 in National Assembly: Pia ni jambo nzuri kuona kwamba mameneja au wadhamini wa halmashauri tafauti ambazo zinafaa kuangazia zile pesa za malipo ya uzeeni kwa wazee wetu, pia wawe na kiasi cha kuangaziwa ili wasiwe watapeli. Wanafaa kuangaliwa elimu yao na kiasi chao cha pesa ili wasitumie nafasi zao za umeneja ama kuwa kwenye halmashauri kunyanyasa watu ambao wameweka pesa zao ili waweze kujifaidi wakati ambao wamewacha kazi. Ukiangalia papo hapo katika hicho kipengele, kinahakikisha kwamba hawa wazee wanaweza kulipwa kwa njia rahisi. Hilo ni jambo ambalo linaweza kutusaidia kusonga mbele. view
  • 19 Sep 2013 in National Assembly: Ni lazima sisi kama Bunge tujionyesha kwamba tuna haki na uwezo wa kuhakikisha kwamba mswala sugu na ambayo yanawaadhiri wananchi wa kawaida yametatuliwa. Pia tunakuwa hapa Bunge ili tuweze kuchangia kwa umahiri na umakini. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus