Issa Juma Boy

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 162.

  • 2 Aug 2023 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, natoa shukrani kwa Waziri kutoka Kaunti yetu ya Kwale. Wiki iliyopita, maandalizi ya kupanda miti na mikoko ilifanywa katika Kaunti ya Kwale. Tunashukuru sana Bi. Waziri kwa shughuli hiyo ya upazi wa miti katika Kaunti ya Kwale, Sub county ya Lungalunga Majoreni. Natoa shukrani sana kwa niaba ya watu wa Kaunti ya Kwale na Gavana wangu, Fatuma Achani. Tunasema asante kwako Bi.Waziri. view
  • 2 Aug 2023 in Senate: Lakini, kuna kilio kimoja. Tulipendekeza sisi viongozi katika Kaunti ya Kwale pamoja na Gavana wetu; kuna miche mingi sana ya mikoko ambayo wananchi wameweza kukuza. Kama unavyojua, watu wetu wako na hali ngumu sana kimaisha. view
  • 2 Aug 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 2 Aug 2023 in Senate: Tulipeana salamu kwa Principal Secretary wako ili muweze kusaidia wananchi hiyo miche iweze kununuliwa na kupandwa katika hiyo mikoko yetu ya sehemu za bahari za Pwani, ufuo wetu wa Kwale; yaani Shimoni, Lungalunga, Vanga na Gasi. view
  • 2 Aug 2023 in Senate: Kwa hivyo, Waziri, tunaomba kama itawezekana, hiyo miche ambayo imepandwa, kwa sababu kuna vikundi vingi vya akina mama na watu kule Kaunti ya Kwale wamepanda mbegu za mikoko. view
  • 2 Aug 2023 in Senate: Bw. Spika, kuna miche mingi sana ambayo haijanunuliwa katika Kaunti ya Kwale. Nadhani juzi alipata ombi hilo kutoka Kaunti ya Kwale. Kuna miche mingi ya mikoko ambayo haijanunuliwa. Tunaomba Serikali inunue miche ile na kupelekea wananchi ili wapande. view
  • 23 May 2023 in Senate: Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Hii Petition imekuja wakati mzuri sana, kwa sababu, kule Kwale Kaunti yangu nina kesi nyingi za walimu kama hawa ambao hawajalipwa pesa zao. Ni jambo la kusikitisha sana haswa kwa walimu. Walimu wamesomesha wanafunzi na wanafunzi wakafaulu. Lakini utakuta kwamba walimu mpaka leo wanalia wakitaka kulipwa pesa zao. Sijui shida iko wapi? Nina kesi karibu tano za walimu. Walimu wawili wameshafariki. Kuna mwingine juzi alipata ajali. Shida iko wapi katika Serikali. Kwa nini hii Tume ya Teachers Service Commission (TSC) hailipi? view
  • 23 May 2023 in Senate: Naunga sana hii Petition ambayo imeletwa wakati huu. Lazima sisi Maseneta tuhakikishe na tusimame imara ili hao walimu walipwe kwa wakati wake. Hiyo Kamati utakayoagiza ichunguze, ifanye kwa haraka sana kwa sababu, it is all over. Jambo hili haliathiri Kaunti ya Kwale peke yake. Hata Mombasa na Kilifi, walimu wananung’unika kwa sababu ya pesa zao. Asante. view
  • 23 May 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 27 Apr 2023 in Senate: Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia suala hili. Maafa ambayo yametokea hivi juzi kule Kilifi ni maafa ambayo yanasikitisha ulimwengu mzima. Runinga zote hapa nchini na ulimwanguni, hasa Cable NewsNetwork (CNN) na Aljazeera zinaangazia maafa yaliyotokea Kilifi. Inasikitisha sana. Mwenyezi Mungu aijalie nchi yetu iwe na amani na watu wawe watulivu kwa sababu imefika pahali ambapo maiti zinafufuliwa kila siku. Ninashangaa maiti hizi zilizikwa namna gani pale Shakahola. Bw. Spika, nina imani na Maseneta waliyochaguliwa katika Kamati hii ambayo itashughulikia suala hili. Nawaomba washughulike na kufuatilia ili tujue shida hii ilianza namna gani? Bw. Spika, sisi ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus