Issa Juma Boy

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 162.

  • 8 Mar 2023 in Senate: Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii, ili niweze kuunga mkono Taarifa iliyosomwa na Seneta wa Mombasa. Kusema kweli, ni jambo la kusikitisha kwa Kenya Power kukata umeme katika Hospitali Kuu ya Pwani. Kaunti za Pwani kama vile Kwale, Kilifi, Malindi, Tana River na Lamu zinategemea hospitali hii. Ukiangalia kwa undani, nalaumu sana Kenya Power. Mwaka juzi kabla twende kwenye uchaguzi, sehemu za Kombani, Kwale, waliambiwa mapema kwamba, kuna nguzo iliyoanguka chini na italeta athari ya mtu kufa. Waliwacha mpaka mtoto akapita, akakanyaga hiyo kitu na wakafariki akiwa na mama yake, kwa sababu ya kupuuza. Leo, tunaskia wamekata umeme katika ... view
  • 8 Mar 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 8 Mar 2023 in Senate: Waliofanya kitendo hicho ni lazima wachukuliwe hatua. Tunategemea hospitali hii kutibu watu wetu wa Pwani. Leo tunasikia jambo hili. Kesho itakuwa ni Msambweni au Kilifi, kesho kutwa iwe ni Taita-Taveta na kesho kutwa Tana River. Bw. Spika, tunawakemea, haswa maofisa waliofanya jambo hilo. Lazima nia yao ijulikane? Ilikuwa ni kuua watoto ICU ama watu wakubwa kwenye theatre? Sisi viongozi katika Seneti hili tunalaani kitendo hicho. Naunga mkono Taarifa ya Sen. Faki. Hatua kali inafaa ichukuliwe kwa Kenya Power. Asante, Bw. Spika. view
  • 22 Feb 2023 in Senate: Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Nitachukua dakika moja tu wala sio mbili. Kwanza, ninatoa shukrani kubwa kuona Kiongozi wa Wengi na wa Wachache, wamekaa chini pamoja na Commissioner Omogeni na kuzungumza ili kupata suluhisho. Kusema kweli, huu ni muhula wangu wa pili katika Bunge la Seneti; Bunge la 12 na sasa hili la 13. Kulikuwa na cheche moto sana katika Bunge la 12 lakini sio kama hii ya leo. Nimeshukuru kuona kwamba kuna viongozi wenye busara katika hili Bunge la Seneti. Wamekaa chini wakaona ni vyema watatue hili swala. Wamekaa chini ili kuweza kutatua jambo hilo. Bw. ... view
  • 16 Nov 2022 in Senate: Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia Taarifa hii ambayo imesomwa na Mhe. Sen. Madzayo, Seneta wa Kaunti ya Kilifi. view
  • 16 Nov 2022 in Senate: Suala la ardhi ni donda sugu sana katika nchi yetu. Mwaka uliopita katika Kaunti yangu ya Kwale kulitokea mkasa mkubwa sana kama huu ambapo hata wiki iliyopita niliukemea sana hapa Bungeni. view
  • 16 Nov 2022 in Senate: Pale Ukunda kuna ardhi ya ekari elfu moja ambayo lease yake ilimalizika. Juzi maafisa wa polisi walikuja pale na mabwenyenye wengine wakavunja karibu nyumba mia nane au mia tisa. Ukiangalia, haki iko wapi hapo. Leo hii, tumemsikia Mhe. Sen. Madzayo akileta Statement kama hiyo kutoka Kaunti ya Kilifi. view
  • 16 Nov 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 16 Nov 2022 in Senate: Ninakemea sana jambo hili la kuwafurusha watu wetu kwa nguvu kutoka ardhi wanamoishi. Waacheni tabia hii ya kuvunjia watu nyumba zao na kuzifanya familia zao na watoto kuteseka. Bwenyenye anakuja na title deed na kusema kuwa hiyo ardhi ni yake, amepewa. Sisi kama Maseneta katika Bunge hili tunatakikana tusimame pamoja zote tukemee hili jambo haswa la kuvurusha watu kutoka kwa ardhi yao. Mimi ninaunga mkono Taarifa jhii . Mimi ni mmoja wa Wanachama wa Kamati ya Ardhi. Wakati kulipotokea tatizo kama hili katika Kaunti ya Kwale, nilipeleka Kamati ya Ardhi katika shamba hilo kule Diani. Iwapo Taarifa hii itapelekwa katika ... view
  • 16 Nov 2022 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus