Issa Juma Boy

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 162.

  • 9 Nov 2022 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa hapa ili tuijadili. Eng. Koome ni afisa ambaye amebobea katika mambo ya ulinzi hapa nchini. Siku za nyuma, alichangia sana kuweka nidhamu upande wa trafiki hapa Nairobi. Kuna jambo moja muhimu ningependa kulizungumzia na ninajua Maseneta wenzangu wataniunga mkono. Kuna polisi ambao wako na tabia ya kufanya eviction hapa nchini siku ya Ijumaa au Jumamosi. Wengi hufanya kazi hiyo usiku. Tunaomba Eng. Koome ahakikishe kwamba jambo kama hili halitatokea tena katika hii nchi yetu. Bw. Naibu Spika, siku za nyuma kama mwaka mmoja na ... view
  • 9 Nov 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 9 Nov 2022 in Senate: Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii, ili niweze kutoa shukrani zangu kwa Maseneta waliochaguliwa kuhudumu katika PSC. Bw. Spika, siku ya leo, tumeweza kutatua utata ambao ulikuwa unatukera sana, upande wetu. Hatukujua tufanye nini, lakini hivi leo tumemaliza shida iliyokuwa hapa. Sisi Maseneta tuna shida mingi sana. Ni lazima tupate mtu anayeweza kupigania haki zetu kule mbele. Kama ilivyozungumzwa na Sen. Cheruiyot, Maseneta wako na majukumu makubwa sana katika hali yetu ya kifedha na matatizo mengi. Ni lazima tupate Makamishna ambao watatutetea, ili tupate haki zetu. Maseneta wenzangu, Sen. Omogeni amebobea kisheria. Yeye in Senior Counsel. Niko na imani, ... view
  • 26 Oct 2022 in Senate: Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa ili nimpe mkono kakangu, Sen. Murkomen, na kumtakia kila la heri katika nafasi yake ya Waziri wa Barabara, Usafiri na Ujenzi. Ndugu yangu, Mhe. Murkomen, kuna kitu ambacho ningependa uzingatie sana. Huwezi kutoka Kaunti ya Mombasa hadi ya Kwale, bila kupitia Mombasa. Kivuko pekee ni pale Feri na hapo pana shida kubwa sana. Mwaka juzi kulitokea ajali mbaya sana ambapo gari lilitumbukia baharini. Ni kwa sababu hakuna watu wa kuangalia usalama katika Feri. Mimi ninaomba Mungu akujalie uapishwe, kisha ninakuomba uandamane na viongozi wa Pwani, uje Kenya Ferry uone vile watu wanavyohatarisha ... view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Asante sana Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii niweze pia kuchangia kuhusu shida hii ambayo imewatokea wenzetu, Sen. Madzayo na Sen. Omogeni. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kusema ukweli pia mimi imenifika. Mwezi jana nilikuwa nasafiri na familia yangu kwenda Tanzania. Nilipofika mpaka wa Kenya na Tanzania pale Lunga Lunga na Horohoro, niliwekwa pale for almost one hour, huku passport yangu ikiwa imechukuliwa na nikaambiwa nisubiri kidogo afisa amepigiwa simu anakuja.Sikujua ni kwa sababu gani. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Alipokuja nikashangaa na kujiuliza kulikuwa na shida gani. Aliniambia niende kwa ofisi. Nikaingia kwa ofisi yake na akaniambia ya kwamba anasikitika kwamba sitoweza kuruhusiwa kwenda safari yangu kwa sababu wamepata mwelekeo kwamba Maseneta hawawezi kuruhusiwa kusafiri kwa ule mda. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Sasa nikajiuliza, kwani kuna shida gani? Sisi ni Wabunge na Maseneta ambao tuna uwezo wa kwenda safari wakati wowote kuwakilisha Serikali na pia kama ni safari ya karibu katika nchi zetu za Afrika hapa tunaweza kwenda. Hii tabia ambayo iliyoko, ni lazima tuweze kujua shida hii itatatua namna gani. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Juzi ilikuwa ni mimi; nilikuwa nafikiria ni mimi peke yangu, lakini leo imewafikia Maseneta wenzetu, Sen. Madzayo na Sen. Omogeni. Kesho itakuwa Maseneta wengine na Wabunge wengine. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Kwa hivyo naomba, kama ni Kamati katika Seneti au kamati yoyote ambayo itashughulikia hili jambo, ifuatilie hili jambo ili tuweze kupewa njia mwelekeo ya kufuata. Hii ni kwa sababu kesho, nitasafiri na watoto wangu tena na nikifika naweza rudishwa tena. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus